Je unaijua AMANA Bank, Inayokopesha bila Riba?

hongera kwa Amana lakini pole kwa kuamua kuchanganya wananchi....i have handon experiences on this thing wakubisha abishe kwangu mm mara mia ukope kwenye conventional banks kuliko hawa wazalimu....
 
Nimesoma na kubobea finance and accounting. Nimefuatilia maswala ya Islamic finance and banking mpaka malesyia ila kwa ukweli ni fix flani. Badala ya kutoza interest wao wanataka profit from investment inayotokana na mkopo wao.
Lakini vyote ni surplus.
Ni majina tu.
 
kwa hiyo mkuu profit na interest ni kitu kimoja au tofauti?
 
Riba na Faida Ni Vitu iwili Tofauti. Amana Bank wanachokifanya ni Biashara, Yaani wananunua Mali au Mzigo Uliokusudia Kuupata wewe Pindi Ungepewa Hela Zako Cash. Then wao kama bank wanaweka faida yao kisha unawalipa kidogokidogo kwa kipindi cha kuanzia mwaka 1 hadi miaka 3 kulingana na makubaliano yenu.

Amanabank hawatoi Mikopo ya Cash, wao wana Finance dhumuni au kusudio la mkopo wako, Kufanya hivi kuna faida kuu 2:-
1. ni Kukufanya usitoke nje ya dhamira kuu ya kukopa kwako, mfano ulihitaji milioni 5 ili ununue bajaj mpya basi wao watanunua bajaj mpya then utauziwa kwa milioni 6 halafu uilipe ndani ya mwaka 1 au zaidi.
Hii ni Biashara, hivyo ziada iliyopatikana hapa ni faida.

2. Kwa Mujibu wa Sharia, Riba ni Haramu. riba ni ziada inayopaikana baada ya kubadilishana vitu ya aina moja, mfano nikikupa Chupa 1 ya juice halafu baadae unirudishie chupa mbil za juice hiyo ni Riba na Haikubaliki ki Sharia.

Kinachofanywa na Amana Bank ni kama Biashara zinazofanywa na Watu wengi, kununua mazigo Point A kwa Bei ya Chini ya Kuziuza Ponti B kwa bei ya Juu Kidogo baada ya Kuweka Faida Yao.

Naiman kwa Macheche kidogo nimeweza kufikisha Elimu hii ndogo.
 
Mmmm!!! Mbona naona itakua biashara kichaa.Wafanyakazi wanalipwa? Chanzo mishahara nini? Wameshawahi tangaza kupata faida? Walipataje bila riba za mikopo? Ukifungua account wanakata monthly service charge? Nikijibiwa maswali haya,kesho asubuhi nitakua kwenye foleni kukopa M100 bila riba.
 
Mkuu Kuna ktu haujanipata, ni hivi ikiwa wewe unahitaji kukopa milioni 100 ili ununue nyumba, Amana bank watamlipa muuzaji hiyo nyumba kiasi hicho cha Milioni 100, halafu wao watakuuzia wewe hiyo nyumba lets say kwa milioni 110 ambayo wewe utairudisha kidogo kidogo kwa kipindi cha miaka kama 5 au 7 hivi. so wao watanunua then wanauza(Biashara coz wanaweka faida yao juu) Mpaka sasa ni wafanya biashara wengi na Wafanyakazi wa Kampuni Mbali mbali wameanza kunufaika na mikopo hiyo.

Kuhusu Faida, inapatikana kwani licha ya kufuata Sharia katika Utendaji kazi wake, Bado Kuna huduma wana Charge Mfano Monthly ledger fees, withdraw charges N.k
 
Riba na Faida Ni Vitu iwili Tofauti. Amana Bank wanachokifanya ni Biashara, Yaani wananunua Mali au Mzigo Uliokusudia Kuupata wewe Pindi Ungepewa Hela Zako Cash. Then wao kama bank wanaweka faida yao kisha unawalipa kidogokidogo kwa kipindi cha kuanzia mwaka 1 hadi miaka 3 kulingana na makubaliano yenu.

Amanabank hawatoi Mikopo ya Cash, wao wana Finance dhumuni au kusudio la mkopo wako, Kufanya hivi kuna faida kuu 2:-
1. ni Kukufanya usitoke nje ya dhamira kuu ya kukopa kwako, mfano ulihitaji milioni 5 ili ununue bajaj mpya basi wao watanunua bajaj mpya then utauziwa kwa milioni 6 halafu uilipe ndani ya mwaka 1 au zaidi.
Hii ni Biashara, hivyo ziada iliyopatikana hapa ni faida.

2. Kwa Mujibu wa Sharia, Riba ni Haramu. riba ni ziada inayopaikana baada ya kubadilishana vitu ya aina moja, mfano nikikupa Chupa 1 ya juice halafu baadae unirudishie chupa mbil za juice hiyo ni Riba na Haikubaliki ki Sharia.

Kinachofanywa na Amana Bank ni kama Biashara zinazofanywa na Watu wengi, kununua mazigo Point A kwa Bei ya Chini ya Kuziuza Ponti B kwa bei ya Juu Kidogo baada ya Kuweka Faida Yao.

Naiman kwa Macheche kidogo nimeweza kufikisha Elimu hii ndogo.
Nimekuelewa vizuri sana mkuu.
shukran...
 
Nimekuelewa vizuri sana mkuu.
shukran...
Karibu sana Mkuu, Miongoni mwa changamoto zinaikabili Isamic banking na Whole Lending Process ni Uelewa Mdogo au Watu kukosa elimu sahihi jinsi gani Bank hizi zinazofata Sharia zinajiendesha. Tuombe Mungu watu wazidi kuzielewa kwani ni Miongoni mwa sehemu salama zaidi kukopa.
 
Riba yao inaitwa gharama za kuendesha mkopo.hakuna benk isiyo na riba duniani acheni kupumbazwa kwa kutumia mwavuli wa dini.
 
Riba yao inaitwa gharama za kuendesha mkopo.hakuna benk isiyo na riba duniani acheni kupumbazwa kwa kutumia mwavuli wa dini.
Mkuu Kwa Jinsi Ulivyojibu tuu imeonesha ni kiasi gani Haukipendi na Haukubaliani na Hiki Kitu, So Far Amana Bank Imejitahidi vya kutosha Kufanya Transactions zake kwa Kufuata Sharia Mpaka kutambulika Duniani Miongoni mwa Islamic Bank Institutions.

Mkuu ukiliangalia hili kwa upande wa Kidini zaidi hatuwezi fika mbali coz tayari umeonesha una kitu ushajiamulia, najiribu kukupa facts kadri vile ambayo Mung atanijaalia. Kikubwa ni watu kuelewa kwamba Amana Bank ni Taasisi ya Kifedha ambayo mbali na Kujieendesha kwa Misingi ya Sharia ipo kwa ajaili ya Kupata faida ili iweze kulipa Magawio ya faida kwa Watu waliowekeza fedha zao.

Kwa taswira ya juu juu unaweza iaona sawa na Convectional Banks lakini kwenye ways of Operations ndo kuna mambo mengi wanatofautiana.

Ukiingia kwenye Web au Instagram Account yao utajua mengi zaidi pia kuna Jopo la Wanazuoni wa Sharia ambao wamesoma zaidi na masuala ya Uchumi na Finance wao huwa wanatoa majibu mengi kwa maswali tofauti tofauti. Mimi hapa nasawazisha tu kwa machache.
 
Mkuu Kuna ktu haujanipata, ni hivi ikiwa wewe unahitaji kukopa milioni 100 ili ununue nyumba, Amana bank watamlipa muuzaji hiyo nyumba kiasi hicho cha Milioni 100, halafu wao watakuuzia wewe hiyo nyumba lets say kwa milioni 110 ambayo wewe utairudisha kidogo kidogo kwa kipindi cha miaka kama 5 au 7 hivi. so wao watanunua then wanauza(Biashara coz wanaweka faida yao juu) Mpaka sasa ni wafanya biashara wengi na Wafanyakazi wa Kampuni Mbali mbali wameanza kunufaika na mikopo hiyo.

Kuhusu Faida, inapatikana kwani licha ya kufuata Sharia katika Utendaji kazi wake, Bado Kuna huduma wana Charge Mfano Monthly ledger fees, withdraw charges N.k
Ahsante,hapo nimeelewa.Mwanzoni ulieleza kama hakuna riba kabisa,kumbe ipo ila kidogo.
 
Mfanonataka kuanzisha biashara ,nahitaji ice cream mashine,pop corn ,heavy d juicer nk..nitavipataje na kwa muda gani!
 
Ama kweli fadhila mfadhili mbuzi binaadam...wangesema ni kwa waislam tu ungesema wabaguz na kila maneno..kama hauko interested si uache tu hawajalazmisha wametoa milango kwa yeyote analiyeinterested akajiunge..sio vizuri kuweka choko choko za udini hata pasipostahiki.
Kiongozi kiukweli statically wakristo wengi wameenda Shule. Ila haimaanishi kua wameelimika zaidi kuliko waislam walioenda Shule. Ndio mana hata katika kutoa hoja mtu unaweza ukashangaa kama kweli mtu anaechangia hoja kasoma. Ila kumbuka anataka aonekane kasoma. Sasa kama hapa bila sababu mtu anauliza swali linamdhalilisha yeye mwenyewe kwa kufikiri anadhalilisha mwengine. Kama hii bank inakubali kukopesha hata wasio waislam na wewe si muislam na hukubaliani na nadharia hiyo siunawaacha tu. Ndani ya tanzania si kweli kua waislam ndo watu ambao hawana elimu zaidi mjue. Hakuna watu wenye elimu ndani ya tanzania kwa ujumla. Na ni bora waislam wameelimika na kustaaribika kuliko hao wanaodhani wameelima.
 
Hivi kwa mfano mtu anafanya biashara, ananunua bidhaa kwa 10,000 then anaiuza kwa 13,000 - sasa hapa kuna tofauti gani na riba au neno lenyewe riba ndo halipendwi. Mambo ya imani yanawafanya watu kama wajinga vile
 
Mimi ninaweza kuwa na nyumba ya kupanga nikasema sitozi ''rent'' lakini nikakulamba ''service charges'' kwa kiasi sawa na rent.

Hiyo riba imepewa jina lingine

Mkuu tafadhali tusaidie hilo jina lingine la RIBA tuanze kulifanyia kazi
 
Back
Top Bottom