Blue Icon Consultancy
Member
- Sep 11, 2020
- 9
- 8
Utafutaji wa Fedha (Fundraising) ni kitendo cha Taasisi kutumia vyanzo/njia mbalimbali kwa ajili ya kukusanya fedha ambayo hutumika katika utekelezaji wa shughuli za Taasisi hususani utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo. Taasisi hutofautiana katika uwezo wa utafutaji wa fedha (fundraising), kuna Taasisi zenye uwezo wa kukusanya kiasi kikubwa cha fedha kwa ajili ya utekelezaji wa miradi, pia kuna Taasisi zingine uwezo wake ni mdogo.
Mafanikio ya ukusanyaji wa fedha (fundraising) kwa kiasi kikubwa hutegemea namna utakavyoweza kufanya TATHMINI juu ya amana zinazomilikiwa na Taasisi yako. Hatua ya ufanyaji wa tathmini ya amana za Taasisi hufanyika katika nyanja tatu, ambazo ni;
- Kutambua amana za Taasisi (Identify Organization Assets); Amana za Taasisi si lazima ziwe fedha tu pekee, isipokuwa hata kukubalika/hadhi ya Taasisi katika jamii (reputation), ujuzi ndani ya Taasisi (skills) aina ya watu awaliopo katika Taasisi; kwa mfano unaweza kuwa na mtu ambae ana "personal connection" na mfadhili fulani., au kuwa na muandishi mahiri wa michanganuo ya miradi n.k. Pamoja na uzoefu (experience). vyote hivi huzingatiwa kama amana. Kimsingi hizi amana hupaswa kutumika katika utafutaji wa fedha kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya Taasisi.
- Katika uhalisia, ni ngumu Taasisi kukosa mapungufu katika amana. Hivyo basi hatua ya pili, baada ya kutambua amana zitumikazo katika utafutaji wa fedha, ni kuangalia wapi unakuwa na upungu/udhaifu kwenye umiliki wa hizi amana na kukabiliana na upungufu huo (Face and Embrace Your Organization's Weaknesses). Kwa mfano unaweza kukosa uzoefu wa kiTaasisi katika utekelezaji wa miradi, nk lakini ukawa na muandishi mzuri wa michanganuo ya miradi (Great Writer), hapa njia ya utafutaji wa fedha kutoka kwenye Taasisi (foundations) kupitia maandiko ya michanganuo ya miradi itafaa zaidi.
- Umekwisha tambua amana ambazo hutumika katika utafutaji wa fedha, pia upungufu ulio nao kama Taasisi, hatua ya mwisho sasa ni kuorodhesha amana ambazo zinamilikiwa na Taasisi yako (List Your Assets). Hapa utatengeneza jedwali ambalo litaonyesha aina ya amana (asset type), ufafanuzi wa amana (assets description) na manufaa ya amana (possible fundraising use).Unapofika kwenye amana ya watu ulio nao kwenye Taasisi yako; ni vyema ukawataja kwa majina na kuangalia kila mmoja anaweza leta mchango gani. Kwa mfano "a certain board member" anaweza akasema kwamba rafiki yake/mke wake/mme wake ni Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni X , hivyo Taasisi inaweza kuomba fedha kwenye kampuni hiyo kwa ajili ya utekelezaji wa Miradi (kwa aina ya mtu huyu, tayari imekwishapatikana njia moja ya kutafuta fedha kutoka kwenye kampuni ya kibiashara yaani "fundraising from a business company").
Ahsante
Blue Icon Consultancy (BIC)
Project Management, Strategic Management & Fundraising Management
Mobile: +255 719 518 367, +255 759 629 397
Dar es Salaam
Tanzania