Je Unahudumu Kwenye NGO? Tathmini Amana za Taasisi Yako Katika Kufanya "Fundraising"

Sep 11, 2020
9
8
1599860505946.png

Utafutaji wa Fedha (Fundraising) ni kitendo cha Taasisi kutumia vyanzo/njia mbalimbali kwa ajili ya kukusanya fedha ambayo hutumika katika utekelezaji wa shughuli za Taasisi hususani utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo. Taasisi hutofautiana katika uwezo wa utafutaji wa fedha (fundraising), kuna Taasisi zenye uwezo wa kukusanya kiasi kikubwa cha fedha kwa ajili ya utekelezaji wa miradi, pia kuna Taasisi zingine uwezo wake ni mdogo.

Mafanikio ya ukusanyaji wa fedha (fundraising) kwa kiasi kikubwa hutegemea namna utakavyoweza kufanya TATHMINI juu ya amana zinazomilikiwa na Taasisi yako. Hatua ya ufanyaji wa tathmini ya amana za Taasisi hufanyika katika nyanja tatu, ambazo ni;
  1. Kutambua amana za Taasisi (Identify Organization Assets); Amana za Taasisi si lazima ziwe fedha tu pekee, isipokuwa hata kukubalika/hadhi ya Taasisi katika jamii (reputation), ujuzi ndani ya Taasisi (skills) aina ya watu awaliopo katika Taasisi; kwa mfano unaweza kuwa na mtu ambae ana "personal connection" na mfadhili fulani., au kuwa na muandishi mahiri wa michanganuo ya miradi n.k. Pamoja na uzoefu (experience). vyote hivi huzingatiwa kama amana. Kimsingi hizi amana hupaswa kutumika katika utafutaji wa fedha kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya Taasisi.
  2. Katika uhalisia, ni ngumu Taasisi kukosa mapungufu katika amana. Hivyo basi hatua ya pili, baada ya kutambua amana zitumikazo katika utafutaji wa fedha, ni kuangalia wapi unakuwa na upungu/udhaifu kwenye umiliki wa hizi amana na kukabiliana na upungufu huo (Face and Embrace Your Organization's Weaknesses). Kwa mfano unaweza kukosa uzoefu wa kiTaasisi katika utekelezaji wa miradi, nk lakini ukawa na muandishi mzuri wa michanganuo ya miradi (Great Writer), hapa njia ya utafutaji wa fedha kutoka kwenye Taasisi (foundations) kupitia maandiko ya michanganuo ya miradi itafaa zaidi.
  3. Umekwisha tambua amana ambazo hutumika katika utafutaji wa fedha, pia upungufu ulio nao kama Taasisi, hatua ya mwisho sasa ni kuorodhesha amana ambazo zinamilikiwa na Taasisi yako (List Your Assets). Hapa utatengeneza jedwali ambalo litaonyesha aina ya amana (asset type), ufafanuzi wa amana (assets description) na manufaa ya amana (possible fundraising use).Unapofika kwenye amana ya watu ulio nao kwenye Taasisi yako; ni vyema ukawataja kwa majina na kuangalia kila mmoja anaweza leta mchango gani. Kwa mfano "a certain board member" anaweza akasema kwamba rafiki yake/mke wake/mme wake ni Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni X , hivyo Taasisi inaweza kuomba fedha kwenye kampuni hiyo kwa ajili ya utekelezaji wa Miradi (kwa aina ya mtu huyu, tayari imekwishapatikana njia moja ya kutafuta fedha kutoka kwenye kampuni ya kibiashara yaani "fundraising from a business company").
Baada ya kuwa umefanya yote hayo nilioeleza hapo juu, ndipo unakuja na Mkakati Maalum ya kutafuta fedha yaani "FUNDRAISING STRATEGY" ambao utakuwa na muda maalumu wa utekelezaji. Utekelezaji wake kikamilifu ndio itakuwa sababu ya kukuwezesha kutekeleza mipango/miradi ya Taasisi yako na kutimiza malengo ya kuanzishwa kwa Taasisi yako.


Ahsante

Blue Icon Consultancy (BIC)
Project Management, Strategic Management & Fundraising Management
Mobile: +255 719 518 367, +255 759 629 397
Dar es Salaam

Tanzania
 
Kitu kizuri kuelewesha taasisi kwenye swala la fundraising kwa maana ndio msingi wa uendeshaji wa taasisi haswa hizi NGO.

Lakini naona umelenga sana taasisi zilizojikuza kwa kiwango fulani ukitoa rasilimali watu kuna taasisi hazina asset yoyote na haswa hawa wanastaili kuinuliwa zaidi.
Asset ya rasilimali watu ambao haswa wanawezakuwa ni board members, members wakawaida au volunteers wanausika kwenye fundraising process kwa upande wa kuanda fundraising plan( goals,base, activities,expenses, software).
Pia wanausika kwenye responsibilities na mwisho kwenye kiini cha fundraising ambacho ni cycle of fundraising development.

USHAURI
Binafsi napenda kufanya kazi na NGO changa na ndogo huwa nawashauri hivi .. kutokana na hali ya uchumi wa sasa linapokuja swala la kutafuta pesa wasiconcentrate kwa mashirika ama wafadhiri kiufupi wasilale kwenye kuandika maproposal tu kwa sababu mashirika ya kifadhiri nayo yanakabiliwa na mtikisiko wa uchumi na majanga ya kidunia,, na isitoshe kwenye key fundraising sources zipo zaidi ya 8 ni swala la kuchagua tu kwamba mtoke na source ipi.
Mimi nawashauri kutumia hizi kwanza special events, sales per service/product na peer to peer.

Asante.
Private fundraising consultant
WhatsApp 0759600809
 
Kitu kizuri kuelewesha taasisi kwenye swala la fundraising kwa maana ndio msingi wa uendeshaji wa taasisi haswa hizi NGO.

Lakini naona umelenga sana taasisi zilizojikuza kwa kiwango fulani ukitoa rasilimali watu kuna taasisi hazina asset yoyote na haswa hawa wanastaili kuinuliwa zaidi.
Asset ya rasilimali watu ambao haswa wanawezakuwa ni board members, members wakawaida au volunteers wanausika kwenye fundraising process kwa upande wa kuanda fundraising plan( goals,base, activities,expenses, software).
Pia wanausika kwenye responsibilities na mwisho kwenye kiini cha fundraising ambacho ni cycle of fundraising development.

USHAURI
Binafsi napenda kufanya kazi na NGO changa na ndogo huwa nawashauri hivi .. kutokana na hali ya uchumi wa sasa linapokuja swala la kutafuta pesa wasiconcentrate kwa mashirika ama wafadhiri kiufupi wasilale kwenye kuandika maproposal tu kwa sababu mashirika ya kifadhiri nayo yanakabiliwa na mtikisiko wa uchumi na majanga ya kidunia,, na isitoshe kwenye key fundraising sources zipo zaidi ya 8 ni swala la kuchagua tu kwamba mtoke na source ipi.
Mimi nawashauri kutumia hizi kwanza special events, sales per service/product na peer to peer.

Asante.
Private fundraising consultant
WhatsApp 0759600809

Kwa NGO changa as one of the executive, naamini katika initial project operation hata kwa scale ndogo tu, huu ni mtaji mkubwa sanaa Katika kutengeneza mazingira ya fundraising hasa kutoka kwa wahisani.

Speaking of connections, hili haliepukiki. personally I do believe kwenye personal connection , circle ya NGO yako/yenu iwe na watu wenye watu ambao wana potential kubwa ambao watapelekea kuwapa nafasi nyingi Kupokea funds either from them directly or other stakeholders.


Let's meet at the top, cheers 🍻
 
Great thread for great thinker, kuna watu huu uzi wataupita kama hawauoni.



Let's meet at the top, cheers 🍻
Wenyewe watakuja ila kama mtu ni member au ulishawahi kumiliki NGO ikafa kisa fundraising tia neno hapa tuyajenge tuangalie taasisi zetu kuanzia ngazi ya kata, wilaya, mkoa hadi taifa tunatokaje hapo kwenye dimbwi la pes ya miladi...tusiwaachie wakenya, wanigeria na wazungu ndo ukienda kwenye NGO kubwa zote wapo idara za fundraising management tena kwa vyeo vya director au manager .
 
Nimependa hi mada ila Mimi pia Ni one of the founder wa NGO moja hapa Tanzania tulipata usajili last year,bado ndo tunaanza Ni project mpya tunataka kufanya.Issue Inakuja Kwenye hzo issue za Fudraising hatujui wapi Tunaanzia kupata funds .

Na umesema hapo Asset moja wapo lazma kuwe na Connection na mtu mmoja wapo kwa Taasisi,Sisi Watoto wa Mkulima hatuna connection yoyote tunafanyaje.
 
Nimependa hi mada ila Mimi pia Ni one of the founder wa NGO moja hapa Tanzania tulipata usajili last year,bado ndo tunaanza Ni project mpya tunataka kufanya.Issue Inakuja Kwenye hzo issue za Fudraising hatujui wapi Tunaanzia kupata funds .Na umesema hapo Asset moja wapo lazma kuwe na Connection na mtu mmoja wapo kwa Taasisi,Sisi Watoto wa Mkulima hatuna connection yoyote tunafanyaje.
Maswali ya kijiuliza na kutafuta majibu yake ni haya kwanza....
👉Taasisi yako ipo mkoa gani na unahudumia kwa level gani ?(kata, wilaya, mkoa au taifa)
👉Objectives zako ni zipi na katika hizo objectives zako ni ipi unataka uanze nayo implementation for 2021
👉Unataka fund kwa ajili ya nini, kuarchive hiyo objective ykao kwa mwaka 2021 au kwa kuendesha taasisi(operation cost) au kununua asset ?
👉Kiasi gani kinatosha ?
Tuanzie hapa kwanza... ukijibu tutaendelea..👊👊
 
Mada nzuri hii...ngoja kwanza nitafute jinsi ya kuanzisha NGO maana ndio lengo la kuja kwenye huu uzi
 
Back
Top Bottom