Je, unafikiri kwa kiwango gani pindi unapoambiwa cherehani 4 ni kiwanda

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,243
34,899
Binadamu wote tuko sawa, lakini tunatofautiana katika kufikiri. Tunaweza tukawa tunatazama kitu kimoja lakini kila mtu akaelewa kivyake kulingana na anavyofikiri.

Fikiria ule usemi maarufu wa �"Is a glass half full or half empty?"

Professor maarufu wa Saikolojia katika Chuo Kikuu cha Union College in Schenectady, New York, Prof. Clare Graves, alifanya utafiti wa kisaikolojia na kugundua kuwa binadamu tunaishi katika viwango tofauti vya kufikiri.

Graves aliainisha makundi manane ambayo huwagawa binadamu kulingana na sifa na tabia zinazofanana. Graves anadai kuwa watu wa kundi moja huwa na kiwango tofauti cha kufikiri na kundi jingine. Watu wa kiwango cha chini cha kufikiri hawawezi kufikiri sawa na watu wa kiwango cha juu.

Albert Einstein aliwahi kusema, �"The significant problems we face cannot be solved at the same level of thinking that created them"

Ndivyo ambavyo binadamu huhama kutoka kiwango cha chini cha kufikiri kwenda kiwango cha juu ili kutafuta majawabu ya matatizo aliyoshindwa kuyatatua katika kiwango cha kufikiri alichopo. Mtu yeyote anaweza kuamua kuwa katika kundi lolote lile. Vilevile mtu anaweza kukaa katika kiwango kimoja au akashuka kutoka kiwango cha juu hadi cha chini kutokana na sababu mbalimbali.

Graves anasema katika utafiti huu kuwa mwanadamu hujifunza kuwa mfumo wa maisha ambao humsaidia katika kipindi fulani cha maendeleo yake hushindwa kumsaidia kadri anavyoendelea kukua.

Kifupi ni kwamba kadri binadamu anavyoendelea kukua ndivyo anavyohitaji kiwango cha juu cha kufikiri ili aweze kuyamudu mazingira yake na kutatua changamoto zake. Inapotokea kuwa changamoto zinakuwa kubwa huku kiwango cha kufikiri hakipandi, binadamu huanza kutoa majibu mepesi kwa maswali magumu.

Tutajadili hivyo viwango 8 vya kufikiri baadaye....

Swali la Kujiuliza ni kwa nini watu wengine hushagalia jambo hilo hilo ambalo wakati mwingine hulizomea kwa sababu tu limezungumzwa na mtu mwingine ambaye si wa upande wake? Je, tunafikiri sawa sawa?
 
Kuna siku watasema ukiwa na wake watatu au nne na ww ni kiwanda cha mbegu....

Hawa ndio Chama Chakavu bwana.....
 
Back
Top Bottom