Je unafanya mazoezi kupunguzwa uzito? Wanasayansi wanasema achana na hiyo kazi unapoteza muda wako bure.

Mazoezi yanakufanya unapungua lakini unaimarika, Mfano mimi niliongezeka zaidi ya kilo 9 jeshini lakini kimuonekano nilipungua si chini ya 30% ya nilivyoingia
 
nafanya mazoezi na chakula nimepunguza kwa asilia 60. kwa kua mimi ni mroho wa wali na ugali huwa asubuhi sili, mchana nakula matunda na saa kumi nakula ugali/wali halafu saa moja naenda mazoezi na asubuhi naenda kukimbia uwanjani. Ninachoamini kimenipunguza japo ni kidogo ni chakula. Sababu nimepunguza kutoka milo mitatu kwa siku mpaka miwili ambayo mmoja ni matunda tu na nakunywa maji ya kutosha.
gym naenda kwa ajili ya kuyengeneza shape na kukimbia asubuhi ni kwa ajili ya kuweka afya sawa na kujiweka sawa kwa marathon maana mwaka huu nimejiwekea malengo ya kushiriki marathon nyingi niwezavyo. nina imani nikiendelea hivi mpaka June nitapungua kabisa maana sasa hivi tu nimeshaanza kuulizwa nini nafanya kupungua
 
Mkuu lost id sasa ni vyakula gani ambavyo sana sana vina faa kuliwa kwa mujibu wa afyaa.

Mana kazi sio kujua kwamba tule vyakula bora lakini kazi ni kuvijua hivyo vyakula boraa sasa.
Je wewe ni muumini wa mazoezi katika kupunguza uzito au unene uliopitiliza?(mimi sio), basi unashauriwa kuachana na huo utaratibu maana unakula muda wako bure, unashauriwa kuangalia chakula chako unachokula zaidi.

Pamoja na kua ni wataalam wa miili ya binadam wanashauri zaidi aina ya mlo unaokula ndio uangaliwe zaidi, ni jambo la akili ya kawaida kabisa(common sense) kua kilichokufanya uongezeke uzito mdicho kitakusababisha upungue uzito, kama umeongezeka uzito kwa sababu ya kufanya mazoezi, basi punguza mazoezi ili upungue, hvyo hvyo kama chakula ndio kimekufanya uongezeke hxito basi punguza chakula upungue, just common sense.

Utafiti huo umechapishwa katika jarida la British Journal of medicine and sports.
Exercise Can't Save Us: Our Sugar Intake Is The Real Culprit, Say Experts

Ni jambo la kawaida la kuelewa kua chakula kinafanya mwili ufanye shughuli zake, chakula kilichozidi mwilini hua mwili unakibadili kua mafurta kwa ajili ya siku za mbele imitokea upungufu kiweze kutumika. Kama chakula unachokula kinatumika chote mwilini basi sio rahisi uongezeke uzito kupitiliza.

Mwaka flani nilikua nimeongezeka sama uzito, watu wakawa wananishauri nifanye mazoezi huku blindly wakisahau kunishauri kuangalia chakula, nikafanya kama mwezi, nikitoka mazoezini nakula kama kawaida, sikuona matokeo, ikabidi nijiongeze kwenye chakula, nikapunguza food intake yangu kwa almost 50%, mwezi mmoja tu kila mtu akaniuliza nimefanyaje.

Lose weight in the kitchen and get fit amd inshape in the gym.
 
Mimi napiga vyote
Dah! We jamaa nimekuelewa kama mimi yani. Msosi nakula kibabe na tizi yangu ya kibabe sana.

Msosi ninaogonga utasema huyu jamaa ni mlafi sana. Tizi ninayo gonga utasema huyu mwana hajihurumii kabisa.
 
Nakubaliana na wewe kwa upande mmoja wa kupunguza volume ya chakula,
Lakini kwa upande mwingine ni kuangalia aina ya chakula unachokula; mfano vyakula vyenye wanga na sukari vikitumiwa kwa kiasi kikubwa (excessively) vinasababisha ongezeko la mwili.

Sikubaliani na wewe kwenye suala la kutofanya mazoezi kwa sababu lengo la kufanya mazoezi ni kuburn excess fat ambayo kimsingi ikiwa tu ipoipo mwilini ndoinasababisha ubonge.

Mimi ni ushuhuda wa hiki ninachokueleza, nimefanikiwa kupunguza uzito kwa kiasi cha KG 6 ndani ya mwezi mmoja just for reducing the volume and type ya vyakula na kwa usiku nakula matunda pekee naepuka au kupunguza kwa kiasi kikubwa matumzi ya vyakula vya wanga na sukari lakini nahakikisha ninakimbia asubuhi Km 3. vivyo hivyo jioni Km 3.

So kusema mazoezi ni kupoteza muda sio sawa licha ya kukubaliana na wewe kuwa kupunguza volume kubwa ya chakula kunapunguza uzito.

Na mimi napata maswali kama yako kwamba nimefanyeje hadi nimepungua that much!!!

Nawasilisha
 
Mafuta hayaepukiki ndio maana hata ng'ombe na mbuzi wanakula majani ila still ukimchinja utakuta ana kiwese.

Good diet ni kula mboga za majani na michemsho isio na mafuta wadau. Ikibidi hata mafuta ya kupikia tubadilishe tuwe tunapikia ya nazi ama olive oil kwa wale tulioimarika kiuchumi. Other than that tutachemka tu.
Hivi vyakula utavila mpaka lini, nilijaribu kuvila ndani ya mwezi nikasikia kichefuchefu!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nakubaliana na wewe kwa upande mmoja wa kupunguza volume ya chakula,
Lakini kwa upande mwingine ni kuangalia aina ya chakula unachokula; mfano vyakula vyenye wanga na sukari vikitumiwa kwa kiasi kikubwa (excessively) vinasababisha ongezeko la mwili.

Sikubaliani na wewe kwenye suala la kutofanya mazoezi kwa sababu lengo la kufanya mazoezi ni kuburn excess fat ambayo kimsingi ikiwa tu ipoipo mwilini ndoinasababisha ubonge.

Mimi ni ushuhuda wa hiki ninachokueleza, nimefanikiwa kupunguza uzito kwa kiasi cha KG 6 ndani ya mwezi mmoja just for reducing the volume and type ya vyakula na kwa usiku nakula matunda pekee naepuka au kupunguza kwa kiasi kikubwa matumzi ya vyakula vya wanga na sukari lakini nahakikisha ninakimbia asubuhi Km 3. vivyo hivyo jioni Km 3.

So kusema mazoezi ni kupoteza muda sio sawa licha ya kukubaliana na wewe kuwa kupunguza volume kubwa ya chakula kunapunguza uzito.

Na mimi napata maswali kama yako kwamba nimefanyeje hadi nimepungua that much!!!

Nawasilisha
Hizo km 3 unazokimbia ni non stop?...au unapumzika kidogo?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom