Je unafahamu ni kwa muda gani vyakula vinatakiwa kukaa ndani ya friji?............... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Je unafahamu ni kwa muda gani vyakula vinatakiwa kukaa ndani ya friji?...............

Discussion in 'JF Doctor' started by Gudboy, Oct 7, 2010.

 1. Gudboy

  Gudboy JF-Expert Member

  #1
  Oct 7, 2010
  Joined: Aug 14, 2009
  Messages: 799
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 33
  Inapokuja katika swala la utayarishaji msosi majumbani kwetu hatuwezi kutoikubali kazi ya friji katika mpango mzima wa kuhifadhi chakula. Kwa kuhifadhi vyakula katika jokofu kunaokoa mda pale unapotaka kupika msosi wa haraka.


  Swali la kujiuliza ni vyakula hivi tunavyoviweka katika majokofu yetu vinaweza kuwa salama kwa mahitaji ya mwanadamu ndani ya mda gani? wataalamu wanasema chakula chochote kitakacho hifadhiwa ndani ya nyuzi 0 za Fahrenheit kitakuwa salama kwa kuliwa kwa mda wote lakini ubora wa chakula hautakuwa uleule.

  Tumekuorodeshea baadhi ya vyakula na mda wake unaoruhusu kuhifadhiwa kwenye jokofu.


  Mkate: Miezi 2 mpaka 3

  Nyama iliyopikwa: Miezi 2 mpaka 3

  Matunda: Miezi 8 mpaka 12

  Sausage: Mwezi 1 mpaka 2

  Soupu: Miezi 2 mpaka 3

  Vipande vya nyama ya kuku ambayo haija pikwa: Miezi 9

  Kuku mzima ambae hajapikwa: Mwaka 1

  Mboga za majan : Miezi 8 mpaka 12

  Ni muhimu ukazingatia haya:

  Kama chakula ni chamoto subiri kipoe kwanza ndio ukiweke kwenye jokofu,hiyo inasaidia kukifanya kipate ubaridi mapema ambapo ubora wake hautapotea kwa haraka. Usigandishe vyakula ambavyo vipo katika makopo au mayai hiyo itavifanya kupata nyufa na bacteria kuingia. Ni muhimu ukafuata maelezo kwa vyakula vilivyotengenezwa viwandani.

   
 2. Kunta Kinte

  Kunta Kinte JF-Expert Member

  #2
  Oct 9, 2010
  Joined: May 18, 2009
  Messages: 3,660
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Du! sup ndani ya friji mwezi mzima! Acha niendelee kubaki bongo-asbuhi unaingia kwa mangi unapiga supu inayotokota jikoni na ng'ombe kachinjwa usiku huo huo!
   
 3. Kipala

  Kipala JF-Expert Member

  #3
  Oct 9, 2010
  Joined: Jan 10, 2009
  Messages: 3,537
  Likes Received: 84
  Trophy Points: 145
  Bwana mkubwa unatupa matata kwa kutumia kipimo cha Fahrenheit (Nani anaituma duniani isipokuwa Marekani???) .

  Sawa unamaanisha vyakula vilivyogandishwa kwa -17.8 °C. Kwa hiyo si friji ya kawaida.

  Hatari inatokea hasa katika mazigira ambako umeme unaweza kukatwakatwa. Maana kama vyakula vilivyoganda vinaanza kupoa bakteria kama salmonela zinaweza kuingia, hapa hatari inaanza hata kama baadaye umeme unaudi.
   
 4. upele

  upele JF-Expert Member

  #4
  Oct 11, 2010
  Joined: Mar 3, 2010
  Messages: 365
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  we umejaribu kuweka kuku mwezi mmoja ukamla au vipi hapo hayo huko huko kwao sie hatuna friji na kiporo tunakula
  Conquest-ujanja wao maisha yetu yale yale:hand:
   
Loading...