Je, unafahamu kuwa Tanzania imeshawahi kuwa na katiba 5? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Je, unafahamu kuwa Tanzania imeshawahi kuwa na katiba 5?

Discussion in 'KATIBA Mpya' started by dfreym, Jan 7, 2011.

 1. dfreym

  dfreym JF-Expert Member

  #1
  Jan 7, 2011
  Joined: Oct 14, 2010
  Messages: 337
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Hili ni moja ya mambo ambayo hata mimi niliposikia nilishituka. siyo siri nilikuwa sifahamu.
  ukweli ni kwamba mpaka sasa katiba tunayoitumia ni katiba ya mwaka 77, na ndiyo ya tano kwa kuhesabu.
  Hebu fuatilia mchakato huu,
  Mnamo mwaka 1961 bunge la uingereza lilipitisha katiba ya kwanza,
  katiba hii ilijulikana kwa jina la INDEPENDENCE CONTITUTION
  Kwa mujibu wa katiba hii, mkuu wa nchi alikuwa malkia na waziri mkuu ( ambaye kwa kipindi hicho alikuwa Mwalimu Nyerere)
  na mfumo wa utawala uliiga mfumo wa uingereza.
  bunge lililo kuwepo kwa kipindi kile lilikuwa ni la vyama vingi(*kiutata) ambalo lilikuwa na wabunge 70 wa TANU na mbunge HURU mmoja (aliyeitwa saraba).
  1962 iliundwa katiba ya pili iliyojulikana kwa jina la REPUBLICAN COSTITUTION. Mchakato wa kuipata Ulijumuisha kamati iliyoitaka jamuhuri kukusanya maoni kuhusu jinsi ya kupata katiba ya jamuhuri.
  ndipo bunge liliamua kujichukulia mamlaka yasiyo yake na kujigeuza kuwa bunge maalumu (constituent assembly) na kupitisha katiba mpya.
  1964,(KATIBA YA TATU)
  Jamuhuri ya tanganyika na jamuhuri ya zanzibar ziliungana na kuunda JAMUHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
  Baada ya muungano pande hizi mbili zilikubaliana kurekebisha katiba ili kukidhi mahitaji ya muungano. katiba hiyo ilirekebishwa na kuzaliwa katiba ya jamuhuri ya muungano [THE CONSTITUTION OF UNITED REPUBLIC OF TANGANYIKA AND ZANZIBAR (TANZANIA)].

  1965 (KATIBA YA NNE (INTEL - CONSTITUTION))
  Katika muda wa mwaka mmoja pande zote hizo mbili (tanganyika na zanzibar) wakatunga katiba ya muungano (ya chama kimoja huku nchi ikiwa na vyama viwili) na kuunda tume ambayo ilikusanya maoni ya wananchi.
  baadae kuunda chombo kilicho na mamlaka ya kupitisha katiba mpya kwa niaba ya wananchi ambapo walilichagua bunge la kawaida na kwa sheria ya kawaida walitunga katiba na kuipa namba pamoja na jina la INTEL -CONSTITUTION.
  katika chombo hicho wakachaguliwa wajumbe kwenda kupitisha katiba).
  Hivyo basi katiba ilipitishwa.

  1977 (katiba ya tano)
  mwaka huu chini ya uongozi wa mzee Jumbe, zanzibar na tanganyika waliunganisha vyama vyao vya ASP na TANU na kuanza mchakato wa (CCM) wa kuunda katiba mpya ulioongozwa na Piusi Msekwa na wenzake.
  mnamo tarehe 25/3/1977
  mwalimu Julius Kambarage Nyerere alitoa tangazo la kupitisha katiba mpya ya chama kimoja.
  Tarehe 25 hiyo hiyo kukawa na tangazo la kuunda bunge maalumu (CONSTITUENCY ASSEMBLY)
  na wajumbe wake kutajwa kwa majina na ukiangalia ni wale wale waliokuwa wabunge.
  Bunge maalumu likiwa na wabunge wale wale wa kawaida likapitisha katiba kwa kisingizio kwamba bunge maalum ni chombo kilichokuwa juu kabisa hivyo laweza kuikubali katiba au kuikataa lakini kwa heshima ya chama ilibidi liikubali.(katiba ya muungano ya mwaka 77)

  katiba hii ilikuwa na sifa zifuatazo;-
  1. Mfumo wa chama kimoja
  2. Mfumo wa serikali mbili katika muungano
  3. Uraisi wa kifalme (raisi alipewa madaraka makumbwa mmno)
  TAMBUA:
  Mwaka 1982 CCM ilitoa mapendekezo ya kurekebisha katiba wananchi wakapewa muda wa mwaka mmoja kuijadili lakini baada ya miezi 9, mijadala hii ilisitishwa kwa kisingizio inachafua hali ya hewa.Ila cha kushangaza katiba ilirekebishwa na kuingizwa KIPENGELE CHA HAKI ZA BINADAMU (ambapo hapo awali hakikuwepo).

  mnamo mwaka 1992 nguzo ya kwanza ya mfumo wa chama kimoja kati ya nguzo zile tatu za katiba ya '77 ilivunjwa na kuruhusu mfumo wa vyama vingi.
  hivyo katiba hiyo kubaki na sifa kuu mbili.  MAMBO YA MSINGI
  1. Katika mijadala ya katiba mpya tusijadili kwa jazba tufanye uchambuzi wa kihistoria na kuangalia tunakotoka na tunakokwenda.
  2. katiba ni sheria mama (political document) na pia ni mkataba kati ya watawala na watawaliwa (endapo itahusisha mijadala huru na ipendekezwe na wananchi na waipitishe wao wenyewe)
  3. katiba si mkataba kati ya watawala na watawaliwa (endapo haitohusisha mijadala huru kupendekezwa na wananchi na kupitishwa na wao wenyewe).
  4. katiba ni muongozo unaoweka misingi ya muafaka wa kitaifa yaani mfumo wa utawala, umilikaji wa mali, uchumi vyote hivyo viwe na misingi maalumu wananchi waitakayo.
  5. Ili katiba iwe halali ni lazima ishirikishe wananchi na ifuate misingi ya kisheria( uhalali wa kisiasa {political legitimacy})
  6. katiba endapo itashirikisha wananchi, basi hainabudi kuheshimiwa na wananchi na viongozi.
  7. katiba ndiyo inayoweka dira ya nchi.
  8. bunge linauwezo wa kurekebisha katiba tu na si kutunga wala kupitisha katiba mpya.
  9. wabunge hawana madaraka ya kutunga katiba mpya wala kuipitisha (isipokuwa labda wachaguliwe na wananchi na kuingia katika bunge maalum si kama wabunge wa kawaida bali kama machaguo ya wananchi, ya kushiriki katika bunge maalumu.
  10. ili kuwe na katiba mpya lazima kiundwe chombo maalumu cha kupitisha katiba hiyo na si bunge.
  OMBI
  1. Ninawaomba wasomaji wa makala haya tuwe wa kwanza katika kuzielimisha familia zetu, jamii zetu na hasa wananchi wa vijijini juu ya umuhimu wa katiba mpya.
  2. katiba mpya ihusu mambo tusiyo yapenda na tusiyoyataka ( yabadilishwe na yafutiliwe mbali) na tunayoyapenda (yawekwe na yapitishwe).
  3. katiba kiurahisi kabisa ni mfumo wa maisha, uchumi, najamii tunapenda viweje/.
  PONGEZI ZA PEKEE.
  pongezi za pekee ziwaendee
  Professor ISSA SHIVJI na professor OSAKI walioongoza mdahalo CHUO KIKUU CHA DODOMA (Tarehe 6/01/2011:saa 3:15 mpaka 5:05 usiku).

  Imetayarishwa na mwana jf kutoka udom.
   
Loading...