Je, unafahamu kuwa kufanya Mapenzi katika kipindi cha ujauzito ina faida kwa Afya ya Mama, Baba na mtoto?

Status
Not open for further replies.

JamiiTalks

JF Advocacy Team
Aug 7, 2018
625
938
exs.png
Watu wengi wamekuwa wakijiuliza kuhusu kufanya mapenzi au tendo la ndoa kama ni salama ama si salama katika kipindi cha ujauzito. Makala hii fupi imelenga kukufahamisha faida za kufanya mapenzi katika kipindi cha ujauzito

Faida zake

Kufanya mapenzi kipindi cha ujauzito kuna faida nyingi. Hizi ni baadhi ya faida kwa mama, baba na mtoto
  • Inasaidi kufanya mwili uwe na afya njema: Kufanya mapenzi ndani ya dakika 30 kwa mara moja kunasaidia kuunguza kalori 50 na kupunguza shinikizo la damu. Afya njema kwa mama inasaidia ukuaji wa mzuri wa mtoto tumboni.
  • Inaweza kupunguza usumbufu na maumivu: Hii husababishwa na homoni za oxytocin zinazotolewa kipindi cha mshindo ambazo husaidia kupunguza maumivu. Hivyo huweza kusaidia kupunguza maumivu katika kipindi cha ujauzito.
  • Huimarisha usingizi: Homoni zinazotolewa wakati wa tendo la ndoa husaidia kufanya mwili uwe na hali ya utulivu
  • Husaidia katika kipindi cha kujifungua kwani hupelekea njia kutanuka
  • Husaidi kuweka ukaribu mzuri wa mama na baba, hivyo basi huimarisha mahusiano
Mikao mizuri ya tendo la ndoa katika kipindi cha ujauzito (sex positions)

  • Kulala upande; huu ni mkao salama kwa mjamzito kwa sababu huzuia uzito ama tumbo kukandamizwa. Kama mjamzito atapata maumivu ya mgongo basi anaweza kutumia mto kuweka upande wa magoti na mwanaume atatakiwa kuwa nyuma ya mwanamke.
  • Mwanamke kukaa juu; huu mkao vilevile husaidia tumbo la mjamzito kutopata mihangaiko yoyote.
  • Mwanamke kupiga magoti na kuweka mikono chini; mkao huu humfanya mjamzito asisumbue tumbo lake
  • Mwanamke kushika ukuta. Mkao huu ni salama kwa mjamzito, ila mwanaume anatakiwa kutumia nguvu ya kawaida wakati wa tendo. Epuka kutumia nguvu zaidi ili kuepusha tumbo la mjamzito kujigonga ama kutikisika sana.
Ni wakati gani tendo la ndoa huathiri mimba

- Inategemeana na hali husika ya mjamzito. Inaweza kuwa ni hatari kwa kipindi Fulani ama kwa muda wote wa miezi 9 ya ujauzito

- Baadhi ya sababu za kawaida ambazo mjamzito anaweza kushauriwa na daktari kuepuka kufanya mapenzi kwa muda Fulani ni kam zifuatazo;
  • Kama una historia ya mimba kutoka ama kuzaa mtoto njiti
  • Kama una matatizo ya kutokwa damu kipindi cha ujauzito
  • Ukiwa na mimba ya mapacha
  • Kuvuja kwa maji ya amniotic
- Kuna baadhi ya wanawake huongeza hamu ya tendo la ndoa pindi wakiwa wajawazito. Hii ni hali ya kawaida na isikutishe. vilevile wengine hupunguza hamu ya tendo la ndoa, ni hali ya kawaida pia.

- Kufanya mapenzi katika kipindi cha ujauzito haisababishi mtoto kuzaliwa na matatizo ama kuzaliwa kabla ya wakati (mtoto njiti). Aidha, kama daktari ameshauri uepuke kufanya mapenzi katika kipindi hicho, basi huna budi kufuata ushauri huo.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom