Je, unafahamu kuhusu tabia ya kutaka kujiua?

Status
Not open for further replies.

JamiiTalks

JF Advocacy Team
Aug 7, 2018
625
938
1609930443867.png

Kujiua ni kitendo cha mtu kukatisha maisha yake. Kwa mujibu wa American Foundation for Suicide Prevention, kujiua ni sababu ya 10 ya vifo duniani. Tabia ya kutaka kujiua ni ile hali ya mtu kuchukua hatua zinazohusiana na kukatisha maisha yake. Mawazo na tabia ya kutaka kukatisha maisha inachukuliwa kama dharura ya ugonjwa wa akili. Zifuatazo zinatambulika kama dalili za mtu anayetaka kujiua

Huwezi kutambua kwa urahisi mtu anavyojisikia ndani ya mwili wake, kwahiyo ni kazi ngumu sana kumtambua mtu anayetaka kujiua. Hatahivyo kuna dalili za nje zinazoweza kukutambulisha dalili za mtu anayetarajia kukatisha uhai wake.
  • Kutishia ama kuzungumzia kuhusu kutaka kujiua
  • Kujitenga ghafla na marafiki, familia na jamii
  • Kuongeza kiwango cha matumizi ya pombe na dawa za kulevya
  • Tabia ya ukali ya ghafla
  • Mabadiliko makubwa ya mhemko (mood swing)
  • Kuongelea, kuandika au kuwaza kuhusu kifo mara kwa mara kama njia sahihi
  • Tabia ya ghafla ya uzembe au kusukumwa kufanya jambo
  • Kulala sana au kidogo
  • Kuzungumzia kuhusu kukosa tumaini na upweke
Namna ya kuzungumza na mtu anaetamani kujiua Kama umemtilia shaka ndugu yako ama rafiki wa karibu ana dalili za kutaka kujiua basi unaweza kujaribu kuzungumza nae. Unaweza kuanza maongezi kwa kumuuliza maswali ambayo hayamuhukumu wala kumpinga.
  • Katika maongezi zingatia yafuatayo;
  • Tulia na ongea kwa sauti ya utulivu
  • Tambua ama kiri kwake kuwa hisia zake ni halali
  • Muoneshe hali ya kumsaidia na kumpa moyo
  • Mwambie kuwa msaada wa kile kinachomsumbua utapatikana na atajisikia vizuri pindi atakapotibiwa
Hakikisha haufanyi tatizo linalomsumbua kuwa dogo au kujaribu kumlazimisha aache maamuzi yake. Kumsikiliza na kuonesha msaada wako kwake ni njia njema zaidi ya kumsaidia. Unaweza vilevile kumshauri aweze kupata msaada kutoka kwa mtaalamu.

Vilevile unaweza kumsaidia kupata msaada kwa mtaalamu kwa kupiga simu au kumpeleka kwenda kuonana nae.
 
Somo zuri.

Kwa ugumu ninaopitia sasa, naona 50-60% ya hizo dalili nazipitia japo sijafikia kufikiria kujiua.

Mwenyezi Mungu aniepushie mbali kwa rehma zake.
 
3 Attempts both failed still I can't stop thinking about doing it 🤔
This means it is not the ideal solution to your challenges. The perfect soln to your challenges is around the corner,just be patient.It wont take longer before everything is back to normal
 
Kwa hali ya maisha ilivyo naelewa sana ambacho hawa watu wanakipitia, Maisha yana Changamoto sana
 
3 Attempts both failed still I can't stop thinking about doing it 🤔

Ukitumia right strategy hutomaliza hata masaa mawili mkuu ila kama life bado lipo. Jifunze tu kuishi na chochote kinachokusumbua regardless kinaonekanaje machoni pa watu
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom