Je unafahamu Dunia ina Watu takribani bilioni saba na kila mmoja ana upekee wake ukiwemo wewe?

Victor Mlaki

JF-Expert Member
May 1, 2016
3,469
3,342
Dunia ina mengi ya kushangaza lakini mengine hayahitaji kushangaa tu ila yanahitaji kutumiwa kama yalivyo ili kushangaza.

Tafiti katika masuala ya upekee wa kibaiolojia zinaonesha kuthibitisha kuwa binadamu tumeumbwa kwa pekee sana mathalani mfumo wa alama za vidole "fingerprints and biometric system"unaonesha tunavyotofautiana.

Ni sawa na kuafiki kuwa wanadamu wote wana upekee wa haina ya kustaajabisha sana licha ya kuonekana kwa haraka kama watu wanaofanana.

Saikolojia ya ufundishaji inabainsha upekee huu kwa kudhihirisha uwepo wa matabaka ya wanafunzi wanaoelewa upesi "fast learners na slow learners" hili linatuonesha kuwa upekee siyo tu jinsia ila upo katika mawanda mengi zaidi.

Wataalamu wa Ubongo wamedhihirisha kuwa ubongo wa Binadamu wa kiume hauna ukubwa sawa na ubongo wa binadamu wa kike,pia licha ya upekee huo wa bado inawezekana ukubwa wa sehemu za ubongo zikatofautiana kutoka mtu mmoja hadi mwingine.

Wataalamu wa rangi wanathibitisha kuwa binadamu wa kiume ana uwezo mdogo wa kubaini rangi mbalimbali "colour blind" ukilinganisha na binadamu wa kike.
Msingi ninaotaka kuujenga hapa unatumia neno "HATUFANANI LICHA YA WINGI WETU".

Katika mambo yanayotakiwa kufikiriwa zaidi ni matumizi ya upekee kwa faida ya jamii ya wanadamu na Dunia nzima yanavyopaswa kuangaliwa kwa kina.
Kanuni hiyo ya upekee inatufundisha kuwa kila mtu ana kitu chake cha kuioneshea Dunia na Dunia ipo tayari na inakisubiri.

Kanuni za asili za kiumbaji zinaonesha kuwa tuna upekee wa namna inayoweza kututofautisha Watu takribani bilioni sana tunaoishi katika Dunia hii Leo.

Ulishawahi kufikiri kuwa hayupo mwingine Duniani ambae yupo kama wewe ulivyo?na je unafahamu kuna jambo unaweza kufanya kwa namna ambayo hakuna mwingine anayeweza kufanya kama wewe?

Ulishawahi kujiuliza ni kwa nini hulifanyi huku Dunia inajua kabisa anayepaswa kulifanya ni mtu mmoja (wewe),tunauonesha upekee wetu ndani ya wakati na muda tunaoishi lakini kuna mengi ya kuangalia nyuma ya wakati(nawaza tu).

Dunia bado inatusubiria kwa hamu kuonesha upekee wetu kwa kufanya mambo ambayo siyo tu yatashangaza watu ila yatathibitisha thamani ya upekee.

USIISHI MAISHA YA WATU WENGINE KUMBUKA YAPO YA KWAKO AMBAYO DUNIA INATAKA IONE
 
Na kuna wengine hata uwafundishe vipi elimu dunia hawaelewi...kuna wale waliomaliza chuo kikuu hata hesabu za kugawanya mpaka wamehitimu Masters degree hawawezi...hao nao ni binadamu wa kipekee.

Biblia inasema...

Mithali 27:22

Hata ukimtwanga mpumbavu kwenye kinu, ukimtwanga kama nafaka kwa mchi, hutauondoa upumbavu wake.
 
Uzi mzuri ila wachangiaji hakuna, big up mleta mada. Hakuna haja ya kujiuliza mbona Mimi Niko hivi.
 
Nondo za ukweli, Asante kiongozi
Dunia ina mengi ya kushangaza lakini mengine hayahitaji kushangaa tu ila yanahitaji kutumiwa kama yalivyo ili kushangaza.

Tafiti katika masuala ya upekee wa kibaiolojia zinaonesha kuthibitisha kuwa binadamu tumeumbwa kwa pekee sana mathalani mfumo wa alama za vidole "fingerprints and biometric system"unaonesha tunavyotofautiana.

Ni sawa na kuafiki kuwa wanadamu wote wana upekee wa haina ya kustaajabisha sana licha ya kuonekana kwa haraka kama watu wanaofanana.

Saikolojia ya ufundishaji inabainsha upekee huu kwa kudhihirisha uwepo wa matabaka ya wanafunzi wanaoelewa upesi "fast learners na slow learners" hili linatuonesha kuwa upekee siyo tu jinsia ila upo katika mawanda mengi zaidi.

Wataalamu wa Ubongo wamedhihirisha kuwa ubongo wa Binadamu wa kiume hauna ukubwa sawa na ubongo wa binadamu wa kike,pia licha ya upekee huo wa bado inawezekana ukubwa wa sehemu za ubongo zikatofautiana kutoka mtu mmoja hadi mwingine.

Wataalamu wa rangi wanathibitisha kuwa binadamu wa kiume ana uwezo mdogo wa kubaini rangi mbalimbali "colour blind" ukilinganisha na binadamu wa kike.
Msingi ninaotaka kuujenga hapa unatumia neno "HATUFANANI LICHA YA WINGI WETU".

Katika mambo yanayotakiwa kufikiriwa zaidi ni matumizi ya upekee kwa faida ya jamii ya wanadamu na Dunia nzima yanavyopaswa kuangaliwa kwa kina.
Kanuni hiyo ya upekee inatufundisha kuwa kila mtu ana kitu chake cha kuioneshea Dunia na Dunia ipo tayari na inakisubiri.

Kanuni za asili za kiumbaji zinaonesha kuwa tuna upekee wa namna inayoweza kututofautisha Watu takribani bilioni sana tunaoishi katika Dunia hii Leo.

Ulishawahi kufikiri kuwa hayupo mwingine Duniani ambae yupo kama wewe ulivyo?na je unafahamu kuna jambo unaweza kufanya kwa namna ambayo hakuna mwingine anayeweza kufanya kama wewe?

Ulishawahi kujiuliza ni kwa nini hulifanyi huku Dunia inajua kabisa anayepaswa kulifanya ni mtu mmoja (wewe),tunauonesha upekee wetu ndani ya wakati na muda tunaoishi lakini kuna mengi ya kuangalia nyuma ya wakati(nawaza tu).

Dunia bado inatusubiria kwa hamu kuonesha upekee wetu kwa kufanya mambo ambayo siyo tu yatashangaza watu ila yatathibitisha thamani ya upekee.

USIISHI MAISHA YA WATU WENGINE KUMBUKA YAPO YA KWAKO AMBAYO DUNIA INATAKA IONE

Sent using Jamii Forums mobile app
 
7 Reactions
Reply
Back
Top Bottom