Je Unafaham kuwa gharama za internet Vodacom ni Tsh 282 kwa MB 1 usipokuwa na kifurushi, mara 9 zaid ya Halotel

RobyMi

JF-Expert Member
Mar 4, 2012
848
862
Wadau,
Kweli awamu hii yetu wote

Nimepitia ukurasa wa Vodacom intaneti packages, nikakutana na hii, inamaanisha ukijichanganya ukaweka kivocha chako cha jero hujazima data, hakichukutachukua hata dakika mbili

Hawa jamaa nafikiri ndo wenye gharama kubwa zaid kushinda mtandao wowote hapa TZ, pamoja na kwamba vifurushi vya Halotel ni moto sasa hivi, ila grahama zao ambazo ni Tsh 30.72 kwa MB ni nafuu mara 9 zaid ya vifurushi vya Vodacom.

Bado kidogo malaika anashuka ..! Inaonyesha ameenza kufanya mazoezi Voda kwanza. !

Sijui kuhusu mitandao mingine, kama kuna mwenye vyanzo kwa mitandao mingine atujuze, hawajaweka kwa website zao.

Hilo tu nimependa kuwafahamisha .!

screenshot-vodacom.co.tz-2018-07-27-09-58-28.png

screenshot-halotel.co.tz-2018-07-27-09-58-09.png
 
Last edited:
Nimeona hata mimi, nilikuwa najaza vocha huku sijazima Data,
Mbona nilifurahishwa kwa hayo makato. Japo sasa Halotel ni majizi sana ya vifurushi, juzi nimetumia GB kadhaa za voda na nimekaa nazo mno. Nimeangalia youtube, nimeshusha vitu lakini kiasi hicho hicho cha GB za Halotel hata saa hazikai.
 
Aisee ni balaa, Kwa kawaida huwezi kujua mpaka yakukute. Na sabab hatuambiwi wengi sana wanalizwa wasiojua kuzima data kabla ya kuweka vocha.

Vodacom waliangalie hili
Anyways SMILE ndiyo mpango mzima hapa mjini,
Japo sijatumia muda sasa ngoja nikatafute modem yake
 
Anyways SMILE ndiyo mpango mzima hapa mjini,
Japo sijatumia muda sasa ngoja nikatafute modem yake

Honestly mi binafsi naona Vifurushi virahisi zaid Tanzania sa hivi ni Zuku pamoja na TTCL

Zuku wan vifurushi rais sana, tatizo wame cover maeneo machache sana, ila jamaa wana unlimited ya 10Mbps kwa Tsh 60,000 tu.!

TTCL wote tunajua sabab ni mtoto wa baba. Ila hawa nawapa mwaka mmoja tu, wakishakuwa watakuja kwa tariff za kuumizana huku ..!
 
Last edited:
Back
Top Bottom