Je, unadhani suala la Katiba litashughulikiwa awamu hii ya Magufuli?

Msukuma Msomi

Senior Member
Feb 6, 2017
173
149
Kwa jinsi hali ya Uongozi na Siasa za Tanzania zilivyo kwa sasa, unadhani ajenda ya mabadiliko ya Katiba itapata nafasi tena? maana naona source ya mijadala ya Bungeni imekuwa ni Instagram: yaani Waziri akiona mtu flani asiyependezwa nae Instagram, basi anampeleka Bungeni na kutangaza hatua za kuchukuliwa.

Maoni tafadhali.
 
hii sirikal inayoendeshwa kwa matukio? thubutuu labda makonda akubal
 
Hapana swala la katiba amelitupia mbal, anasema akutoa ahadi ya katiba
 
Hata wakati anaomba kura katiba haikuwa ajenda yake.....tumhukumu kwa viwanda na mahakama ya mafisadi sio katiba mpya.!
 
Kwa jinsi hali ya Uongozi na Siasa za Tanzania zilivyo kwa sasa, unadhani ajenda ya mabadiliko ya Katiba itapata nafasi tena? maana naona source ya mijadala ya Bungeni imekuwa ni Instagram: yaani Waziri akiona mtu flani asiyependezwa nae Instagram, basi anampeleka Bungeni na kutangaza hatua za kuchukuliwa.

Maoni tafadhali.

SI KIPAUMBELE!
 
TUNATAKA MAENDELEO CYO KATIBA MPYA
Maendeleo bila katiba mkuu utajikuta unalia mwenyewe bila kupigwa maana utakuwa unashuhudia mali zinaondoka tu bila udhibiti wowote ule. Katiba ndo mambo yote si vinginevyo.
 
Kwa jinsi hali ya Uongozi na Siasa za Tanzania zilivyo kwa sasa, unadhani ajenda ya mabadiliko ya Katiba itapata nafasi tena? maana naona source ya mijadala ya Bungeni imekuwa ni Instagram: yaani Waziri akiona mtu flani asiyependezwa nae Instagram, basi anampeleka Bungeni na kutangaza hatua za kuchukuliwa.

Maoni tafadhali.
Katiba inaweza kupata nafasi ya kujadiliwa jambo la msingi walio karibu na mkuu watoe hoja zenye mashiko wakionesha faida za Katiba mpya na hasara ya kuendelea kubaki na Katiba ya zamani huku wakimhakikishia matumizi ya gharama za chini katika mchakato
 
Mtukufu wa magogoni keshasema katiba mpya siyo kipaumbele cha serikali yake kwa sasa. Acha 'anyooshe' nchi kwanza.

Cc; Hashim Rungwe
 
Kama uwezekano wa kuendeleza mchakato wa kupata katiba mpya haupo basi tunaomba wahusika wote wa bunge la katiba wachukuliwe kama wahujumu uchumi au wezi wa hela za watanzania, wazirejeshe na mwisho wachukuliwe hatua kwa kulitia Taifa hasara.
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom