Je; una nafasi gani katika swala la matambiko na mila na desturi katika ukoo wako..?

Mgodo visa

JF-Expert Member
Nov 1, 2016
3,590
3,626
Kama kichwa cha habari kinavyo jieleza hapo juu..

Ni ukweli usio pingika... japo wapo watakao pingana na hili.
(naruhusu mjadala "KUPANULIWA" ili kila mtu aweze kupata maoni na UJUZI zaidi)
images.jpg

Hakuna asiye elewa kuwa kila familia katika ngazi ya UKOO wana MATAMBIKO, MIIKO na Mila na Desturi zao...

Kila Mwana Familia baada ya kufikia umri wa KUBALEHE/KUVUNJA UNGO hujikuta akiambiwa ama kujionea baadhi ya mambo ya KIASILI ama KITAMADUNI yanayo fanyika katika/ndani ya UKOO wake..
1464594018904.jpg

Mambo haya yanaweza kujitokeza katika SHEREHE mbalimbali ama katika MSIBA.

Katika Familia au Ukoo wowote lazima awepo Mwana ndugu wanaesema AMEBEBA au AMERITHI Mikoba...

Swali langu Je; wewe mwenzetu umesimamia ama una kipaumbele gani..una umuhimu gani katika Ukoo wako...!!?

Kuna wengine wamerithishwa UGANGA...wengine DINI (hapa unakutana na Mashehe na Maaskofu)

Wengine wamerithi MIKOBA ya uchawi na KADHA WA KADHA.
121004092800-tanzania-witchcraft-roots-horizontal-large-gallery.jpg
.

Kuna familia zikiwa katika Meza ya chakula, hawawezi kula mpaka mtu fulani (mteule) afanye MAOMBI...

121004092800-tanzania-witchcraft-roots-horizontal-large-gallery.jpg

Tiririka hapa tuone ama tujue UNA-PLAY ROLL ipi..?

Karibu sana Broth MSHANA Jr..
 
Attachments

  • Real-witch-pictures-vintage-1.jpg
    Real-witch-pictures-vintage-1.jpg
    60.1 KB · Views: 55
  • 253021_900.jpg
    253021_900.jpg
    55.2 KB · Views: 51
MAMBO ZA MASHETANI HIZI MKUU
Ni muhimu kuwaenzi mababu zako kupitia desturi na mila zenu na usipofanya hivyo utajikuta unawaenzi mababu au mizimu ya watu wengine kama vile kwenda kwa waganga kwani hao waganga baadhi hutumia mizimu yakwao kuagulia na kuwapa watu mazindiko.
Na ni vizuri kutumia both mababu zako na mababu wa wengine.
 
Mimi ktk ukoo wetu ndio kiongozi W shughuli zoote za kimila na kitamaduni.hakuna tukio linafanyika bila me kuwepo.yaaan im the chief
Nimekuelewa Mkuu...you are A Choosen one...vp hukutani na vikwazo toka kwa ndugu na jamaa wanao kuzidi UMRI..!!?

Maana kupewa MIKOBA kuongoza KAYA inataka Moyo.
 
Nadhani kila kabila la Kiafrika lina matambiko. Lakini lazima utambue kwamba kufanya tambiko ni ushirikina. Tambiko linaenda kwa mizimu. Mizimu ni mashetani ya ukoo. Kama wewe unayo dini halafu unafanya tambiko unamshirikisha Mungu na hiyo mizimu. Mungu hapendi kushirikishwa na kitu chochote maana Yeye yuko juu ya vyote.
 
Mbona tunamshirikisha Mungu na Vitabu....

Ama Vitabu hivi havikuandikwa na Watu..!?
 
Nimekuelewa Mkuu...you are A Choosen one...vp hukutani na vikwazo toka kwa ndugu na jamaa wanao kuzidi UMRI..!!?

Maana kupewa MIKOBA kuongoza KAYA inataka Moyo.
Magumu sana.yanataka mda mwingine uwe fyatu
 
Back
Top Bottom