Gemini Are Forever
JF-Expert Member
- Sep 10, 2019
- 1,457
- 2,435
Salaam wakuu.
Tulikuwa maeneo fulani leo mchana, tulienda kucheki mashamba ya jamaa yangu aliweka vibarua.
Tulipofika ktk mizunguko ya hapa na pale shambani, tukaenda kupumzika. Sasa kulikuwa na ndoo ya maji, ikabidi jamaa achukue kikombe anywe maji.
Jamaa kwa vile alishikwa na kiu ikabidi achote maji akaanza kunywa. Kapiga kama mafundo mawili hivi, ghafla akayamwaga maji na akaweka kikombe chini akainama kama anataka kutapika.
Baada ya sekunde kadhaa akaanza kutapika kweli. Kumuuliza kulikoni akasema kikombe kina harufu ya maziwa kitu ambacho roho yake haitaki kabisa. Nikashangaa sana. Yaani Maziwa mi nayapiga hata yakikamuliwa hapo hapo halafu yeye harufu tu anatapika!?
Mi kitu ambacho sikipendi ni bilinganya. Aisee ukinilisha bilingaya natapika hadi nyongo. Kuna jamaa nilisikia akinusa harufu ya nyama ya kondoo anatoa hadi nyongo.
Kuhusu phobia mi naogopa radi jamani duh.
Je, wewe phobia yako au allergy yako ni ipi?