Je, Una Msaada Wowote Katika Upatikanaji wa Viwanja?

Mtanganyika

JF-Expert Member
Jul 18, 2007
1,601
946
Jamani kuna swali naomba nisaidiwe. Mimi ninashida ya kununua kiwanja dar, lakini nashangaa kila nikisearch google nashindwa kupa website hata moja ya mabroker.
Can any one help me.

Kingine nadhani JF tunaitaji kuweka sector ya Uza na Nunua kwenye hii forum yetu.
 
Sidhani kama ni rahisi kupata watu wanaouza viwanja. Ukitaka nyumba kuna National Housing ( sikumbuki web-site yao)na jamaa wengine ambao walikuwa wakijenga kigamboni. Hawa wa kigamboni ni Mutual Developers wako http://www.mutualdevelopers.com. Kuna wakati sheria ilikuwa inakataza kuuza viwanja isipokuwa maendelezi kwenye viwanja. Ndiyo maana hatuna free-hold rights hapa kwetu isipokuwa unakuwa mpangaji kwa serikali. Jaribu kuulizia wizara ya ardhi maana nao walikuwa na mpango wa kupima viwanja na kuuza! kila la kheri.
 
Mtanganyika jaribu www.tzadverts.com, kuna viwanja, nyumba na mazagazaga kibao yanayouzwa bongo. DISCLAMER: siwezi kumu endorse agent yeyote kwenye hiyo site kwa kuwa sijawahi kufanya biashara na yeyoye so be vigilant and do it at your own risk.
 
We kama uko unahitaji kiwanja halali, nenda pale wizara ya Ardhi au manispaa yeyote(Temeke, Kinondoni na Ilala), watakueleza viwanja vilivyopo tayari kwa kuuzwa not permanently, unapewa like right ya miaka kati ya 33 to 99 renewable!
 
Ukweli, Mkuu, kununua kiwanja kupitia mtandao Bongo ni kama kununua mbuzi aliye kwenye gunia. Kama kweli unataka kujenga, tafuta muda, nenda Bongo ukachangamkie. Usitume mtu, nenda mwenyewe. Ndiyo njia pekee ya uhakika kwa bahati mbaya. Ndiyo hali halisi.
 
Mtanganyika, kwa kweli idea yako ya kuwa na Buy & Sell hapa JF nzuri, ila, kwa viwanja nakushauri km wenzangu hapo juu ununue via Wizara ya Ardhi (mradi wa 20,000 plots), I did the same and got a plot in Bunju for a mere 4 mil. Ukinunua kwa agents ni balaa: utapeli, 'cha juu' etc
 
Ukweli, Mkuu, kununua kiwanja kupitia mtandao Bongo ni kama kununua mbuzi aliye kwenye gunia. Kama kweli unataka kujenga, tafuta muda, nenda Bongo ukachangamkie. Usitume mtu, nenda mwenyewe. Ndiyo njia pekee ya uhakika kwa bahati mbaya. Ndiyo hali halisi.

Akinitumia mimi atafanikiwa kwani nina uhakika siwezi kudokoa hata senti moja. Hapa ni kisiwa cha amani najiamini kusema hivyo. Mungu niimarishe zaidi.
 
Akinitumia mimi atafanikiwa kwani nina uhakika siwezi kudokoa hata senti moja. Hapa ni kisiwa cha amani najiamini kusema hivyo. Mungu niimarishe zaidi.

Bubu Msemaovyo! Mbona picha yako umeiondoa? Ingekuwepo nadhani ingekuongezea point kwenye hili usemalo!
 
Thanks guys. Najipanga kurudi nyumbani sometime this year au next year.
Nilikuwa nadhani ni wise kukamata plot na kuanza kupandisha hata msingi. I saw couple of viwanja kwenye website ambazo wadau wemenitumia, sema price zake naona ni nightmare.

I will take your advices, thanks alot. Sema nadhani tunaitaji Buy and Sell dept kwenye Jamboforum. Kama tulivyo na Job Vacancy section.
 
Jamani kuna swali naomba nisaidiwe. Mimi ninashida ya kununua kiwanja dar, lakini nashangaa kila nikisearch google nashindwa kupa website hata moja ya mabroker.
Can any one help me.

Kingine nadhani JF tunaitaji kuweka sector ya Uza na Nunua kwenye hii forum yetu.Mkuu jaribu kutembelea website hizi mbili na labda utafanikiwa utafutacho.

Haya masuala ya kutaka kujenga banda bongo ni magumu mno mpaka sasa, kwani wasanii wapo wengi sana TZ lakini kila kitu chataka wewe mwenyewe ufatilie.

http://www.dar411.com/

Na hii na NHC bongo.

http://www.nhctz.com/default.htm
 
Back
Top Bottom