TUSHIRIKISHANE Je una maoni, ushauri au maswali kwa Mbunge Zitto Kabwe kuhusu maendeleo ya Kigoma-Ujiji?

Aug 9, 2016
13
67
AgrmtKigoma.jpg


Mbunge wa Kigoma-Ujiji, Zitto Zuberi Kabwe Zitto amekuwa akishirikiana na Mamlaka za Serikali za Mitaa, Wananchi na Viongozi wa Manispaa katika kuleta maendeleo jimboni kwake kupitia mradi wa Tushirikishane.

Kufanikiwa kwa maazimio haya ya maendeleo kunategemea pia mchango wa wadau mbalimbali wa maendeleo ndani na nje ya Manispaa ya Kigoma.

Je una maoni yeyote kwa Mbunge kuhusu utekelezaji wa maendeleo jimboni mwake?

Una swali lolote kwa Mbunge? Unapendezewa na namna mbunge wako anafanya kazi?

Kwa mjadala wa Mradi wa Tushirikishane Kigoma, tembelea => TUSHIRIKISHANE - Mjadala wa Mipango ya Maendeleo kwa Jimbo la Kigoma Mjini
 
Actions speak louder than words...
Aige wenye maendeleo kisha atende nasi tutaona.
 
Actions speak louder than words...
Aige wenye maendeleo kisha atende nasi tutaona.
Nashukuru umeongea kitu nilichokuwa nataka kukisema Huyu jamaa shida yake anaongea Sana lakin kiuhalisia sion jipya. Ngoja nitoe mfano mdogo nimeenda moshi cku za Karibun pale mjin aisee nimekuta wale jamaa wameweka lami karibu kila mahali wamejenga masoko na wanaendelea vizur. Mi zitto ningemshaur afanye kaz za kuchochea maendeleo zaid aachane na mambo ya kuonyesha mipango ya kwenye karatas Mbona bungen tuliona vitendo kuliko maneno?
 
Mwambie aache unafiki kwanza. Leo anaseama serekali ya JPM haina demokrasia kesho anaisifia labda watu wa kigoma wanamuelewa zaidi.
 
Nami ngoja nitupie japo kamoja na kengine ka nyongeza;
  1. Je, yeye ni mbunge wa chama cha upinzani kweli?
  2. kwa nini mara nyingi wanasiasa kutoka Kigoma huwa vinyonga wa siasa (Rejea, Kabulu na Yeye mwenyewe)?
 
1. Aimarishe Soko la Buzebazeba maana lipo hovyo
2. Barabara nyingi za Manispaa ziko hovyo. Kibirizi kote barabara mbovu, Mwanga barabara za mitaaani ni mbovu, hakuna taa za barabarani. Je Manispaa ilipata fedha za Sustainable City Projects (SCPs)? Kama ndiyo wamezitumiaje? Kama siyo wanajipangaje?
3.Pale Mwanga SIDO Market wale vijana wanaotengeneza sabuni waliwahi ahidiwa na Zitto kupewa machine mpya za Kisasa kusaidia kutengeneza sabuni bora zaidi na hivyo kuitikia wito wa Rais wa kuboresha viwanda. Je kwa nini hajawatimizia ahadi hiyo?
5. Manispaa haina Hospitali yake, je wana mpango gani kujenga?
6. Viwanda kwa ujumla ni vichache sana , je wana mpango gani maana rate ya kujengwa viwanda na ku create ajira ni ndogo.
7. Kuna haja ya kupanua mji kwa kupima viwanjana kutengeneza barabara mpaka kule Businde ili kuwe na sura ya Manispaa
 
Wa kigoma vinyonga....nazani wale madiwani wa Arusha ni Litmus paper.
Nami ngoja nitupie japo kamoja na kengine ka nyongeza;
  1. Je, yeye ni mbunge wa chama cha upinzani kweli?
  2. kwa nini mara nyingi wanasiasa kutoka Kigoma huwa vinyonga wa siasa (Rejea, Kabulu na Yeye mwenyewe)?
 
Sana ajitambue kwani ninachokiona mm ni mdomo mipango isioakisi kile anacho ongea atambue umbunge tulimpa kipindi kile alipo toa ajadi sasa hatutaki ahadi sasa nivitendo nawala asifikiri uongozi ukiwaridhisha viongozi wadini ndio umemaliza sisi sio wafasi wadini ile MTU mmoja akisema ndio basi niote yeye angalie ahadi zake kwamfano elimu kidato cha 5-6 walisema dhana niwao mbona sio kweli watu wanarudishwa?
 
Kidato cha tank nasita ulisema nibure mbona kijana wangu karudishwa ameambiwa atoe 70000 act mlicho lipia nikipi? Pia ulisema Unataka kgm /ujiji iwe mfano mpaka sasa nikipi unachoweza kuonesha kama fano mpaka sasa?
 
Back
Top Bottom