TUSHIRIKISHANE Je una maoni, ushauri au maswali kwa Mbunge Wilfred Lwakatare kuhusu maendeleo ya Bukoba Mjini?

Aug 9, 2016
13
67
AgrmtBukoba.jpg


Mbunge wa Bukoba Mjini, Wilfred Lwakatare Wilfred Lwakatare amekuwa akishirikiana na Mamlaka za Serikali za Mitaa, Wananchi na Viongozi wa Manispaa katika kuleta maendeleo jimboni kwake kupitia mradi wa Tushirikishane.

Kufanikiwa kwa maazimio haya ya maendeleo kunategemea pia mchango wa wadau mbalimbali wa maendeleo ndani na nje ya Manispaa ya Bukoba Mjini.

Je una maoni yeyote kwa Mbunge kuhusu utekelezaji wa maendeleo jimboni mwake?

Una swali lolote kwa Mbunge? Unapendezewa na namna mbunge wako anafanya kazi?

Kwa mjadala wa Mradi wa Tushirikishane Bukoba, tembelea => TUSHIRIKISHANE - Mjadala wa Mipango ya Maendeleo kwa Jimbo la Bukoba Mjini
 
Bahati nzuri mimi ni mfuatiliaji mzuri wa Maendeleo ya Jimbo la Bukoba Mjini miaka kenda. Kumekuwa na sintofahamu kubwa sana kuhusu miradi mikubwa miwili ambayo ni ujenzi wa Stendi Kuu ya Mabasi na Soko Kuu.

Hii miradi ilipelekea mpaka kukawa na uhasama mkubwa wa mbunge na meya waliopita (Mbunge Kagasheki, Meya Amani). Wametunishiana misuli mpaka kupelekea miradi hiyo kushindwa.

Mbunge wetu sasa naye aliingia kwa mbwembwe na ahadi kedekede ila kadri siku zinavyokwenda anazidi kupunguza kasi. Nazijua kazi za Mbunge,Halmashauri,Serikali za Mitaa na Serikali kuu. Sisemi yeye ndio ajenge ila analisimamia vipi kufanikisha miradi hii miwili mikubwa ambayo ni kitovu cha maendeleo Bukoba?

Masuala la kutuonesha picha za miradi bila utekelezaji ni kutuhadaa. Kumbuka umenufaika kutokana na ugomvi wa Amani na Kagasheki.

Suala jingine, Mbunge wangu naomba uwe unakaa jimboni na wapiga kura wako. Wewe ni mwakilishi wa wanabukoba na sio wanaubungo, Ubungo wana mbunge wao. Muda unaokaa Dar ni mwingi kuliko jimboni. Bata za Coco beach ukazifanyie Kiroyera.
 
Dah ashughulikie masuala ya soko na stand kwanza pia waangalie barabara za halimashauri ya bukuba mjini wamejitahidi kujenga barabara za lami ila zote ziko chini ya kiwango.Barabara hazina mitaro nyembamba kiasi kwamba pikipiki moja na gari zinapishana kwa shida magari mawili hayapishani
 
Back
Top Bottom