Je, una hisi ratiba yako ina mambo mengi sana?

Mtayarishaji

JF-Expert Member
Jan 25, 2012
291
199
Ikiwa ndivyo, hauko peke yako. Gazeti The Economist linasema kwamba “kila mahali, kila mtu anaonekana kuwa na shughuli nyingi sana.”

Mwaka wa 2015, utafiti ulifanywa katika nchi nane kwa watu wanaofanya kazi ya kuajiriwa ya wakati wote, na wengi wao walisema kwamba si rahisi kutimiza majukumu waliyo nayo kazini na nyumbani.

Baadhi ya mambo yaliyotajwa kuwa yanasababisha tatizo hilo ni kuongezeka kwa majukumu kazini au nyumbani, gharama zinazopanda za maisha, na muda mwingi wa kufanya kazi.

Kwa mfano, nchini Marekani, waajiriwa wa wakati wote hufanya kazi kwa wastani saa 47 kwa juma. Pia, karibu mtu mmoja kati ya watano alisema anafanya kazi kwa saa 60 au zaidi!

Kwenye utafiti mwingine uliohusisha nchi 36, zaidi ya robo ya watu waliohojiwa walisema kwamba hata wanapokuwa wamepumzika, wao huhisi wako mbioni!

Watoto pia wanaweza kuathiriwa ikiwa wanapangiwa ratiba yenye mambo mengi mno.
 
Back
Top Bottom