Elections 2010 Je, una hati ya kupiga kura 2010?

Hivi Tanzania kuna mpango wa kuwapatia wananchi walio nje ya nchi nafasi ya kupiga kura? Nchi nyingi wanafanya hili. Au siye ndiyo "no funds available" ?
 
Hivi Tanzania kuna mpango wa kuwapatia wananchi walio nje ya nchi nafasi ya kupiga kura? Nchi nyingi wanafanya hili. Au siye ndiyo "no funds available" ?
ndo maanake!NO FUND AVAILABLE
 
Kama unayo:

1. Ihifadhi vizuri kwenye sefu!

2. Katu usikubali kuwauzia mafisadi!

Na kama huna:

1. Jiandikishe upate hati yako!

2. Kamwe usikubali kutojiandikisha!
---------------------------------

Rejea 'Waraka wa Uchaguzi wa Kuli: Yana Mwisho Haya'!

Zingatia Wito wa Mwanakijiji: '2010 - Ni Mwaka wa Uhuru Wetu'!
Hati ya kupigia kura tunayo. Bahati mbaya wakati wa uchaguzi wengi wetu huwa tuko huku ughaibuni 'tunabeba maboksi' na hakuna utaratibu wa kuwawezesha walio nje kutimiza haki yao kidemokrasia, matokea yake tumewaachia watu wengine watuchagulie viongozi na imebidi tuwakubali kwani 'anayemuoa mama ndiye baba'
 
Wabeba maboksi rudini nyumbani mjiunge na makuli wenzenu kupiga Kura ya Uhuru!
 
Hivi Tanzania kuna mpango wa kuwapatia wananchi walio nje ya nchi nafasi ya kupiga kura? Nchi nyingi wanafanya hili. Au siye ndiyo "no funds available" ?

Kuna mzengwe wa kuwaengua wote waliofikisha umri wa miaka 18 na hawapo kwenye orodha ya awali ya daftari la wapiga kura! Sembuse watukumbuke sisi Wabeba Mabox?
 
Aisee, kuna watu wengi hawana hizi hati, nakwambia kama inawezekana naomba tuanze kupiga kampeni watu waende wakaandikishe. sasa watu hawajui waandikishe wapi, na ccm wanajua kama watu woote hasa huku mijini wataandikisha, watapiga kura kinyume nao na watashindw mwakani. so the only thing they can do ni kuto kuelewesha watu wengi wajiandikishe sasahivi, ili wapiga kura kwa wapinzani waje kuwa wachache.
 
Lakini ukiwa Zenji hiyo haina maana bila kuwa na kadi ya Ukazi.

Sijui ni katiba gani hiyo inayosema hivyo
 
Awamu ya kwanza ya uandikishaji ilipita. Walisema watakuja kwenye pango langu kunipangia siku ya kwenda kujiandikisha. Ila sikuwaona. Awamu ya pili nasikia inakaribia. Tusikubali itupite hivi hivi. Kupiga kura ni haki yako. Pia ni wajibu wako. Piga kura. Na usimpigie fisadi.
 
Mkuu Campanero, hii avatar yako inafanana sana na Mzee wa 'Vijisenti' vipi mnaweza kuwa na uhusiano?
avatar11297_3.gif
 
Nimefurahishwa sana na mwamko huu wa wana JF na kura ya UHURU 2010. Mie ninakoishi nimefanikiwa kuwahamasisha wananchi wenzangu kuandaa kabisa kadi zao kwa ajili ya uchaguzi huu. Nimewasisitizia kwamba itakuwa kura ya UHURU wa kweli ili wasije wakarudia makosa na kujitia kitanzi cha mafisadi. Hamasa ni kubwa kwa kweli...
 
Mzee hongera sana. Hiyo ni hatua muhimu sana. Sasa, je wanawajua hao mafisadi? Kama hawawajui vizuri basi hatua inayofuata ni kuwafanyia uzee punch hao wenye ujasiri wa kifisadi! Tupo pamoja! Uhuru umekaribia!
 
Last edited:
Leo katika ibada nimesikia paroko anasema juu ya mwongozo na watu kujiandikisha na kusema kukaa chini na kuongelea namna ya kuiba kura na kupokea chumvi ili umchague mtu ni against na maagizo ya kristo na ukristo wa matendo.Hamasa ni kubwa na usione Kingunge na wazembe wenzake wanalia bure .

Sasa JF tuwasaidie kama alivyo fanya mzee punch jamani hakuna kulala kabisa .
 
kama unayo:

Na kama huna:

1. Jiandikishe upate hati yako!

2. Kamwe usikubali kutojiandikisha!
---------------------------------

rejea 'waraka wa uchaguzi wa kuli: Yana mwisho haya'!

zingatia wito wa mwanakijiji: '2010 - ni mwaka wa uhuru wetu'!

kwani usipofanya hayo hutapiga kura uchaguzi ujao wa serikali za mitaa na uchaguzi mkuu na utapoteza haki yako ya kikatiba ya kuchagua serikali yako uipendayo.

Kumbuka kuwa haki hii huja mara moja katika kila miaka mitano usipuuze kamwe!!!!!!
 
Samahani kuuliza siyo ujinga.

Hivi kuna tofauti gani kati ya hati na shada ya kupiga kura?? Maana navyofikiria ni kuwa hati ni voters registration card. Lakini huwa nachanganyikiwa ninaposikia kuwa CCM wamenunua shahada za kupiga kura hiyo jamaa hawawezi kpiga kura.

Narudia tena kuuliza siyo ujinga. Mambo ya daftari la kudumu wakati linaanza nilikuwa nje na sijaweza kupiga kura chaguzi tatu zilizopita kwa vile hawataki kutuwekea utaratibu na sisi wabeba mabox tupate haki yetu ya kuchagua.
 
Kwanza mnakumbuka uchaguzi ulifanyika decemba 2005,na pia kwa uchaguzi ujao hakuna kweli kipengele cha katiba vitakavyopingana iwapo uchaguzi utafanyika j'pili ya mwisho ya oktoba mwaka 2010? Maanake kuna kipengele kinachoongelea muda wa Urais.....
 
Samahani kuuliza siyo ujinga.

Hivi kuna tofauti gani kati ya hati na shada ya kupiga kura?? Maana navyofikiria ni kuwa hati ni voters registration card. Lakini huwa nachanganyikiwa ninaposikia kuwa CCM wamenunua shahada za kupiga kura hiyo jamaa hawawezi kpiga kura.

Narudia tena kuuliza siyo ujinga. Mambo ya daftari la kudumu wakati linaanza nilikuwa nje na sijaweza kupiga kura chaguzi tatu zilizopita kwa vile hawataki kutuwekea utaratibu na sisi wabeba mabox tupate haki yetu ya kuchagua.

Kabla sheria ya uchaguzi haijabadilishwa sometime in 2004 kabla ya uchaguzi wapiga kura waliwajibika kujiandikisha kupiga kura na tume ya uchaguzi likuwa inatoa shahada za kupigia kura. Baada ya mabadiliko kilichopo sasa hivi ni daftari la kudumu la wapiga kura ambalo kila mtanzania mwenye miaka 18 na zaidi anatakiwa awe amejiandikisha katika daftari hilo. Akijiandikisha mtu huyo hupewa kitu kinachoitwa kadi ya mpiga kura ambayo humuwezesha mwenye kadi hiyo kuwa na haki ya kupiga kura. Kwa hiyo ili kupiga kura unahitaji kadi ya mpiga kura.Hiyo ikichukuliwa hutakuwa na uwezo wa kupiga kura.

NB: kama hukujiandikisha sheria inaruhusu daftari hilo kufanyiwa marekebisho yenye lengo la kuondoa atu waliokufa, watu waliofikisha miaka 18, watu ambao wana umri huo lakini kwa sababu moja au nyingine hawakujiandikisha, watu waliobadili makazi na au waliopoteza kadi zao.

Kama wewe ni mmoja kati ya makundi hayo yaliyotajwa aya ya juu wahi haraka kujiandikisha kipindi ni hivi sasa
 
Back
Top Bottom