Je, umeweka vitu gani juu ya meza yako ya kulia chakula (dining table)?

Shadeeya

JF-Expert Member
Mar 12, 2014
48,223
115,061
Habarini Wakuu.

Ni muda kidogo kuna nyumba moja niliwahi kufika, hiyo nyumba si nyumba kubwa sana ila sebule ni kubwa hivyo mwenye nyumba akaamua kutenga sehemu ambacho ameweka meza ya kulia chakula.

Muda niliofika haukuwa muda wa kula lakini nilichokikuta pale juu ya meza pana bakuli ya kuonyesha lenye mfuniko ndani lina maandazi, kuna chupa za chai na si moja, hotpot pia si moja, nikaona vijiko, kikopo cha sukari, sahani kadhaa kazibebeshea hapo mezani yaani kiufupi meza ilijaa.

Na hiki ndio kimefanya nije na huu uzi wakuu

- Je meza ya kulia chakula inapaswa kuwa vile muda wote?
- Kama sio inapaswa iwe na vitu gani ule muda ambao si wa watu kupata chakula?
 
meza ya chakula inatakiwa kuwa na chakula wakati wa kula tu na baada ya hapo inawekwa mapambo kama maua au kitu kingine kuipendezesha. Kuiacha na makorokoro sio poa maana meza ya chakula pia inaweza kutumika kwa shughuli nyingine kama kusomea na kadhalika

Kwenye suala ya kupendezesha nyumba watz tuko nyuma sana, utakuta mtu amejaza makorokoro kibao sebuleni au chumbani mpk unakosa nafasi ya kujimwambafy. Sebule au chumbani kunatakiwa kuwa na vitu vichache muhimu na sio vingi visivyo na kazi.

Utakuta mtu amehifadhi jikoni au stoo kreti la soda la double cola wakati kiwanda kilishafungwa to 1982. Au utakuta mtu ana godoro la toka anaanza Maisha kalihifadhi tu utadhani makumbusho. Tubadilike kuendana na wakati

clean-wood-dining-room-table-800x800.jpg
 
Meza yangu ni multipurpose..

Itakuwa na chakula, muda wa chakula tu. Muda mwingine inakuwa empty.

Vitu vingine watu wanakuwa wanaiga tu kutokana na mwendokasi wa utandawazi, ndio maana unaweza kuona wanaweka makorokocho kibao.

Hayo makorokocho yatapendeza(yatakuwa safe) endapo hamna watoto ambao wanaweza kuyaharibu...
 
Safi!

Na hiyo nyumba ina watoto kibao.
 
Nimetandika kitambaa kilicho fumiwa maua ya kuvutiaView attachment 1309897

Sent using Jamii Forums mobile app
Daaah mh mjumbe udenda umenitiririka hapa hatari, umenikumbusha kinywaji fulani chenye mithili ya gongo ila hakileweshi(tunakiita Magae), tunapenda kukitumia msimu wa kulima kule nyumbani.

Ukipiga chipuku moja unakuwa imara zaidi ya kupiga glucose na utaendeleza kuchapa/kuvuta jembe ipasavyo kabisa hatimaye unailaza hekari kwa siku chache kabisa
 
Ahsante mh mjumbe, haya mambo vijana walio zaliwa kwa mipango ya vidonge na sindano hawayajui

Sent using Jamii Forums mobile app
 
8 Reactions
Reply
Back
Top Bottom