Je umewahi....?

Dr Lizzy

Platinum Member
May 25, 2009
30,695
58,770
We all know what power does to a person.....
I mean kuna watu wakipata madaraka..kazi...elimu...pesa zaidi ya walizokua nazo mwanzo wanaruhusu vitu hivyo vitawale hata utu wao na wanabadilika mpaka tabia.Unakuta mtu anaanza dharau/majigambo/manyanyaso kwa wengine/ukorofi na mengine yanayofanana na hayo.

Swali langu....Je umewahi kumsaidia mtu kutoka kwenye ngazi moja kwenda nyingine (kikazi...kielimu n.k) alafu baada ya hapo akabadilika kwa ubaya? Nasema kwa ubaya maana wengine wanaweza kubadilika kwa uzuri. Neway imeshatokea hizo/hiyo tabia yake mpya akailekeza hata kwako wewe uliyemsaidia ...mf kukudharau na kukuona wewe sio kitu???
Je baada ya kujua kwamba ndugu/rafiki yako huyo ni mlevi wa nguvu/madaraka/uwezo ungepewa nafasi ya kurudi nyuma mpaka pale ulipoamua kumsaidia je ungefanya maamuzi yale yale ya kumsaidia ama???
 
power inawafanya watu wajioneshe tabia zao halisi
watu hawabadiliki,bali wanakuwa themeselves wanapopata power....

kujutia kuwasaidia watu hao ni ujinga kwani ni bora uwsaidie ili uwajue walivyo

kuna msemo unasema PATA PESA TUKUJUE TABIA ZAKO..

very true
 
Bado ni mabadiliko.....kutoka kwenye alichokua akionyesha mwanzo mpaka kwenye alivyo kweli (tukitegemea msemo wako wa kwamba power inamfanya mtu aonyeshe alivyo kweli)

Nwy hapo kwenye kujuta binafsi sijapenda kutumia hilo neno kwasababu kujuta hakusaidii. Swali langu ni kwamba kama mtu akipewa nafasi ya kurekebisha na kurudisha balance iliyokuwapo mwanzo atafanyeje?
 
wanasema, ---"regret for what you haven't done...dont regret for the things you have done!"---
tenda wema wende zako,...

usingemsaidia, akaja saidiwa na mwingine na akakufanyia hayo maringo,
ungejilaumu 'labda ungemsaidia wewe asingekuletea nyodo!'
 
Nna rafiki yangu yeye aligeukwa na shemejie (kaka wa mkewe) pamoja na kwamba awali alimtafutia kazi na baada ya kuchanganya mihela pale zain-by then celtel- kaka mtu akamgeuka shemeji yake na kutoa siri zake za kutengeneza hela. Sijui alikuwa hapendi dada yake afaidi kupitia shemejie au vp.

Ilifika mahali jamaa yangu akataka kumpiga chini mkewe ili amkomoe kaka mtu, ila tulimsihi aachane na kaka mtu kwani alikuwa hajui afanyalo.

My take: Mtu wa namna hii wala huitaji kumkabili kinguvu, muache tu uzoefu umeonyesha wengi hurudi ktk umasikini wao wa awali na hapo ndo utakampompasha ukweli na wala usimsaidie tena. Ila inahitaji moyo sana ktk hili suala maana huwa inauma sana mtu uliyemuamini mwanzo anapogeuka kuwa ndio kikwazo/adui ktk maisha yako
 
Ukitaka kujua tabia halisi ya mtu mpe fedha au cheo....kuna watu wanalimbuka sana baada ya kufanikiwa....
 
Bado ni mabadiliko.....kutoka kwenye alichokua akionyesha mwanzo mpaka kwenye alivyo kweli (tukitegemea msemo wako wa kwamba power inamfanya mtu aonyeshe alivyo kweli)

Nwy hapo kwenye kujuta binafsi sijapenda kutumia hilo neno kwasababu kujuta hakusaidii. Swali langu ni kwamba kama mtu akipewa nafasi ya kurekebisha na kurudisha balance iliyokuwapo mwanzo atafanyeje?

mabadiliko ni lazima
tena wana saikolojia wanasema 'mabadiliko yanakuja so natural kiasi kwamba'
hata yeye mwenyewe anaweza asijue kuwa 'amebadilika'
nitakupa mfano mmoja

kuna mtu yeyote anaechelewa kwenda kwenye interview ya kazi
au kwenda kazini siku ya kwanza na wiki ya kwanza??

but ukishazoea ofisi.unajikuta tu unachelewa au unasema 'kulikuwa na foleni leo
na visingizio kibao.....lol
 
Ukitaka kujua tabia halisi ya mtu mpe fedha au cheo....kuna watu wanalimbuka sana baada ya kufanikiwa....

Mbaya sana...especially ulimbukeni huo unapokua unaumiza watu wengine.

mabadiliko ni lazima
tena wana saikolojia wanasema 'mabadiliko yanakuja so natural kiasi kwamba'
hata yeye mwenyewe anaweza asijue kuwa 'amebadilika'
nitakupa mfano mmoja

kuna mtu yeyote anaechelewa kwenda kwenye interview ya kazi
au kwenda kazini siku ya kwanza na wiki ya kwanza??

but ukishazoea ofisi.unajikuta tu unachelewa au unasema 'kulikuwa na foleni leo
na visingizio kibao.....lol

Boss acha weee....
Mabadiliko tunayanotice sana sema tatizo ni kuya-acknowledge.

Mfano kama huo uliotoa unadhani mtu hafanyi kwa makusudi???Anajua kabisa kwamba sasa hivi kazi nimeshaipata sina haja ya kuheshimu muda na kazi anymore. Ni kitu kinachofanyika kwa makusudi kabisa!
 
Mbaya sana...especially ulimbukeni huo unapokua unaumiza watu wengine.

Boss acha weee....
Mabadiliko tunayanotice sana sema tatizo ni kuya-acknowledge.

Mfano kama huo uliotoa unadhani mtu hafanyi kwa makusudi???Anajua kabisa kwamba sasa hivi kazi nimeshaipata sina haja ya kuheshimu muda na kazi anymore. Ni kitu kinachofanyika kwa makusudi kabisa!

nafikiri umeelewa pointi hapa
pointi hapa ni kuwa bbaada ya kuajjiriwa
amekuwa na tabia zake halisi..za kutojali kuwahi kazini'
na sio kwamba amebadilika.....ni kwamba ile kuwahi haikuwa tabia yake halisi......
 
ni kweli watu wengi huwa tunasahau tulikotoka. lakini pia na sie tunaosaidia watu huwa tunataka wakati mwingine mtu akusujudie kama mungu kisa tu ulimsaidia! kuna mtu kama alikutaftia kazi, basi anataka hata small house zake (bila kujali implications zake kwa mahusiano yako kazini na ktk jamii pia) uwatafutie kazi na pia kuwapa favor zisizo na maana. 'heshima' is a relative term, same as 'dharau'. sio kwa sababu umemsaidia mtu kitu flani ndo kila j1 aje kujipanga na familia yake kukusalimia. ama ukiwa na besdei kwako mkewe aje kufanya u-housigeli. inabidi kujifunza ku-take it easy wakati mwingi...
 
nafikiri umeelewa pointi hapa
pointi hapa ni kuwa bbaada ya kuajjiriwa
amekuwa na tabia zake halisi..za kutojali kuwahi kazini'
na sio kwamba amebadilika.....ni kwamba ile kuwahi haikuwa tabia yake halisi......

Kwanini isiwe kwamba tabia yake ilikua kuwahi ila baada ya kujikuta kwenye sehemu tofauti na aliyokuwapo mwanzo akadevelop tabia mpya ambayo ni kutokujali???

Wakati mwingine watu wanabadilika kutokana na mazingira.
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom