Je, umewahi kupitia bullying kwenye maisha yako?

XII Tz

JF-Expert Member
Aug 16, 2020
4,293
6,956
Habari wakuu

Je, umewahi kupitia bullying kutokana na maumbile au muonekano wako, ni namna gani iliathiri saikolojia na maisha yako kiujumla na je ni namna gani ulipambana na tatizo hili.

Binafsi kuna kitu hakipo sawa kwenye mwili wangu ( siwezi taja ) imekua ikiathiri sana saikolojia na maisha yangu in general, shule niliiona chungu kipindi nipo primary, nimekua nikitaniwa sana na kuchekwa.

Imedidimiza my self esteem siwezi hata kusimama mbele za watu, unfortunately only surgery can correct that. Mimi ni muumini wa dini ya kiislam hivyo nilijaribu kufuatilia kama ni sahihi kufanya surgery but luckily enough nimeambiwa it's permitted if only done to correct any deformity in the body be it a birth defect or an acquired one, most especially if it causes either psychological or physical pain.

Japo wazazi wapo against jambo hili kwa kisingizio eti dini, itoshe tu kusema hiyo dini hawajui inasemaje kuhusiana na hili na mbaya zaidi hawataki kuelimishwa ( much know ) .. kwa hili watanisamehe tu, maisha yenyewe mafupi haya kwanini ukose raha kwa kudhikakiwa yet there's a solution na dini imepermit ?? ..

Mwisho wa yote, kama na wewe mdau wa JF ni Ile aina ya watu wenye kupenda kucheka ama kudhiaki watu kutokana na muonekano please acha mara moja, hujui tu ni namna gani inaathiri saikolojia ya mtendewa na mara nyingi hupelekea hata kujitoa uhai sababu wengine mioyo yao mepesi hivyo vitu kama hivi vinaweza kumtoa kabisa kwenye reli ..wanasema kushare na watu yanayo kutatiza kunaweza saidia kuleta relief moyoni hivyo basi yangu ni hayo tu naomba kuwasilisha.

Mwisho kabisa kama kuna mtu anataka kunipinga nasema hivii nipe mkono tushindane nipeeee (jokes)
 
Ukitaja hiko kitu na sie tutataja ila kama unaficha, tegemea watu kutokusupport sredi yako.. N'way niko na shemeji yako hapa na enjoy nae kimtindo.
tapatalk_747766044.jpg
 
Fid Q aliwahi kusema katika ngoma ya Kiberiti "usipende kuchukulia vitu personal"

Kwenye maisha kila wanachozungumza watu juu yako usitake kukibeba. Wengine wanaweza kukubully sio kwa sababu ya kasoro yako ila chuki zao tu, wengine utani tu etc. Wakina Manara wanatukanwa tena matusi mazito mara nguruwe sijui misukule lakini wanadunda tu bila shida.

Tafuta hela mkuu acha kuhangaika na vitu vidogo vidogo.
 
Fid Q aliwahi kusema katika ngoma ya Kiberiti aliwahi kusema "usipende kuchukulia vitu personal"

Kwenye maisha kila wanachozungumza watu juu yako usitake kukibeba, wengine wanaweza kukubully sio kwa sababu ya kasoro yako ila chuki zao tu, wengine utani tu etc. Wakina Manara wanatukanwa tena matusi mazito mara nguruwe sijui misukule lakini wanadunda tu bila shida.

Tafuta hela mkuu acha kuhangaika na vitu vidogo vidogo.
Yah! Endapo hakutakuwa na solution, ila kama solution ipo basi huna budi kurekebisha kwanini uteseke ..
 
Back
Top Bottom