Je, umewahi kujiuliza nia ya Rais Samia kusamehe wafanyabiashara kodi za nyuma?

The Evil Genius

JF-Expert Member
Mar 21, 2014
5,456
17,193
Je, umewahi kujiuliza kwa nini Rais Samia aliamua kuwasamehe wafanyabiashara kodi za miaka ya nyuma, ambazo ni kodi halali kabisa wanazodaiwa na mamlaka ya kodi? Kumbuka mwezi June Rais Samia aliwaagiza TRA wasiwasumbue wafanyabiashara kwa kuwadai kodi za miaka ya nyuma isipokuwa za mwaka jana pekee.

Jibu ni moja tu, Samia aliamua kuwasamehe wafanyabiashara, halafu akaamua zile kodi walizokua wanadaiwa wafanyabiashara, wafanyakazi wawasaidie wafanyabiashara kulipa kwa kukatwa tozo kwenye mishahara yao ambayo tayari imekashakatwa kodi.

Tozo ni fidia ya kodi ambayo Samia aliamua kuwasamehe wafanyabiashara. Samia anajali tabaka la juu na anakamua tabaka la chini kwa maslahi ya tabaka la juu la wafanyabishara!

bibi kazidi, anachokifanya ANAZINGUA TU. Mafuta upande wa zanzibar hakuna kilio tangu enzi za magu, huku bara tangu magu afariki bibi na genge lake anatupandishia madude. Bibi anazingua
 
Huyu mtu ni Muhuni tu, hamna kitu kabisa.

Amekuja Kurudisha mfumo wa Kunyang'anya Masikini alichonacho na kumpa Tajiri .

Mfumo aloutumia kikwete ambapo ulizalisha CHUKI kubwa na hasira Kwa Raia walio Wengi

Ukitaka kujua huyu mtu Muhuni, URAIS wake anaona ni wa kushikiliwa nawatu fulan ambao inabidi awalambe ili aendelee kuraisikika.

Kashindwa kupambana na Inflation inayozidi Kupanda , kaja kwenye TOZO .

Huku akijua kwamba HAMNA MFANYABIASHARA ANAYEPENDA KULIPA KODI

Kwa hakika , inawezekana kabisa Nchi hii ndo ikawa inaongozwa na watu wa hovyo hovyo
 
Je umewahi kujiuliza kwa nini Rais Samia aliamua kuwasamehe wafanyabiashara kodi za miaka ya nyuma? Ambazo ni kodi halali kabisa wanazodaiwa na mamlaka ya kodi...
Ukiwa mjinga jaribu kujielimisha kwanza.
Kodi halali ni zipi?

Anatokea mtu wa TRA anakuambia kwa vile una duka la mtaji wa milioni 10 basi nakukadiria kodi ya milioni 3 kwa mwaka.

Na kwa vile ulianzisha duka miaka mitano iliyopita kwa hiyo kodi ni milioni 3 mara 5 ni milioni 15.

Na kwa vile kuna fine ya kutolipa miaka yote hiyo, fine ni milioni 10.
Sasa na riba ya kutolipa kwa wakati kila mwaka, riba ya kodi ya milioni 15 ni milioni 4.5

Kwa hiyo mfanyabiashara unadaiwa milioni 15+10+4,5 jumla 29.5 milioni.
Mtaji wako ni milioni 10 katika duka.

Ni mjinga tu hawezi kuelewa kuwa huo ni wizi wa kiserikali na kodi hailipiki maana hata ukiuza mtaji hiyo kodi huwezi kulipa.
 
Ukiwa mjinga jaribu kujielimisha kwanza.
Kodi halali ni zipi?
Anatokea mtu wa TRA anakuambia kwa vile una dua la mtsji wa milioni 10 basi nakukadiria kodi ya milioni 3 kwa mwaka.
Na kwa vile ulianzisha duka miaka mitano iliyopita kwa hiyo kodi ni milioni 3 mara 5 ni milioni 15.
Na kwa vile kuna fine ya kutolipa miaka yote hiyo, fine ni milioni 10.
Sasa na riba ya kutolipa kwa wakati kila mwaka, riba ya kodi ya milioni 15 ni milioni4.5
Kwa hiyo mfanyabiashara unadaiwa milioni 15+10+4,5 jumla 29.5 milioni.
Mtaji wako ni milioni 10 katika duka
Ni mjinga tu hawezi kuelewa kuwa huo ni wizi wa kiserikali na kodi hailipiki maana hata ukiuza mtaji hiyo kodi huwezi kulipa.
Msamehe bure kaka, mtoa mada hajui biashara na kampuni za kawaida kabisa za wazawa zinavyo kandamizwa na TRA. Tax examinatio ile ya miaka 5 nyuma inaumiza sana.
 
Kwani wafanyabiashara hawaguswi na tozo mbalimbali zilizoanzishwa na Mh. Samia?

Mfanya biashara anaweza kukwepa Kodi au akalipa kidogo sana tofauti na mfanyakazi. Kumbuka mfanyakazi anakatwa Kodi kabla hajaikamata pesa yake, Kwa Sasa ikiingia benki napo anakatwa Tena tozo.

Mleta Uzi hoja yake ni Je, kwanini wafanya biashara wamesamehewa Kodi Halali walizotakiwa kulipia huko awali?
 
Ukiwa mjinga jaribu kujielimisha kwanza.
Kodi halali ni zipi?

Anatokea mtu wa TRA anakuambia kwa vile una duka la mtaji wa milioni 10 basi nakukadiria kodi ya milioni 3 kwa mwaka.

Na kwa vile ulianzisha duka miaka mitano iliyopita kwa hiyo kodi ni milioni 3 mara 5 ni milioni 15.

Na kwa vile kuna fine ya kutolipa miaka yote hiyo, fine ni milioni 10.
Sasa na riba ya kutolipa kwa wakati kila mwaka, riba ya kodi ya milioni 15 ni milioni 4.5

Kwa hiyo mfanyabiashara unadaiwa milioni 15+10+4,5 jumla 29.5 milioni.
Mtaji wako ni milioni 10 katika duka.

Ni mjinga tu hawezi kuelewa kuwa huo ni wizi wa kiserikali na kodi hailipiki maana hata ukiuza mtaji hiyo kodi huwezi kulipa.
Na ndiyo sababu biashara nyingi ziliyumba na kufungwa awamu iliyopita
 
Kuna usawa gani kama mfanyakazi anakatwa kodi kwenye mishahara halafu bado anakatwa tozo halafu mfanyabiashara halipo kodi anakatwa tu tozo?
Aliekwambia wafanyabiashara Hawalipi kodi Nani.... Mama aliona aachane na Yale mambo unakuta TRA anakuja kukudai Leo kodi ya mwaka 2015 Unajiuliza kwann hawakuja kufanya hii assessment huo mwaka au basi 2016 lakini wanakuja Leo 2022 wanakufanyia assessment ya 2015 huo ni uzembe wa mamlaka na umerudisha nyuma Sana wafanyabiashara wengi Sana nyuma... Biashara zinapanda na kushuka 2015 ulimclear mtu unarudi tena Leo unasema anadaiwa hawakumkadilia vizuri
 
Na ndiyo sababu biashara nyingi ziliyumba na kufungwa awamu iliyopita
Yaani usilipe kodi miaka mitano...nije madarakani nakwambia lipa unaanza kusema oh tusameane. Hamna kiyu kama hicho mie naingia mwenye account yako nachukua changu basi. Kwanza washukuru hawakutiwa ndani. Hawa wafanya biashara waliokwepa kodi ni kuwalazimisha walipe basi. Kwenye kodi hakupaswi kuwe na mjadala.
 
Back
Top Bottom