Je umewahi kujiuliza kama maombi yanaweza kubadili chochote katika maisha yako?

The Assassin

JF-Expert Member
Oct 30, 2018
4,355
17,320
Je hua unaomba, unategemea maombi? Je maisha yako yamewahi kubadilika sababu ya maombi?

Juzi timu yetu ya mpira wa miguu Taifa Stars ilicheza na Lethoso ili kutafta nafasi ya kufuzu kushiriki michuano ya mataifa ya Afrika.

Kabla ya mechi watu walihimizwa kuomba na kuiombea timu yetu Taifa Stars ili Mungu aibariki iweze kushinda, watanzania wote wapenda mpira na tusio penda mpira tulihimizwa kua wazalendo na tuiombee timu yetu ya taifa ifanye vizuri.

Hata wachezaji pia waliomba sana Mungu awape nafasi, waliandika sana kwenye kurasa zao katika mitandao ya kijamii, wakimsihi Mungu awape nafasi hii adimu ukizingatia tuna miaka 38 hatijawahi kushiriki.

Naamini watu walimwaga maombi, sio wachezaji, sio mashabiki, sio wananchi wa kawaida hadi viongozi wa kisiasa na kidini wote walimwaga maombi ili timu yetu ishinde.

Lethoso ina wananchi wasiozidi milioni 2 na laki 3. Tanzania ina watu wanaokaribia milioni 60. Katika hali ya kawaida ukihesabu idadi ya maombi ya watanzania wazi kabisa yalikua mengi kuliko ya walethoso, lakini cha ajabu Lethoso iliitwanga taifa stars goli moja zito.

Je ni maombi yetu hayakua mengi vya kutosha, au hayakua na uzito wa kutosha. Je maombi yanaweza kubadili chochote? Maombi yanaweza kukusaidia kupata upenyo? Nini kilisababisha hatukushida pamoja na maombi yetu yote kuanzia kwa viongozi wa kisiasa hadi wananchi wa kawaida?

Lazima ujiulize, je maombi yana msaada wowote?!
 
Maombi yanakuandaa kupokea matokeo
 
Maombi yanaambatana na Imani.

Mafanikio yanaambatana na juhudi na mipango chanya katika kuenendea kile unachohitaji kukifikia/kukipata.

Kikipungua kimoja kati ya hivyo nikujidanganya.

Tafakari.
 
Kwa akili yako hata bacelona ikicheza na lipuli fc utategemea maombi lipuli ashinde?
 
Serikali inaminya sana raia wake,kodi lukuki,watu kufukuzwa kazi kiholela, sheria kandamizi za mafao ya mifuko ya jamii unategenea nchi ifanikiwe kwa lipi? Mioyoni watu wamejawa na majonzi hivyo ni mgumu Mungu kusikiliza maombi ya Tanzania.
 
Back
Top Bottom