Je, umewahi kufanyiwa visa kisa kumkatalia mtu kuwa mpenzi wako?

Habari wa JF members.

Leo nilikuwa nimekutana na rafiki yangu niliyewai soma naye shule moja hivi ambayo baadae nikaja kuhama tulikua tukielekezana habari za baada kutengana muda mrefu, baadaye mazungumzo yakahamia ishu moja kipindi nasoma iyo shule kabla sijahama

ishu yenyewe ilikuwa inahusu demu mmoja hivi nilikuwa nasoma darasa moja kipindi hicho nipo form two,stori yenyewe hipo hivi

Kipindi cha mwezi wa nane tukifanya mitihani ya mock huyu rafiki niliyekutana leo aliniletea barua ya mapenzi ambayo aliniambia ilikuwa imeandikwa demu alikuwa akijulikana kwa jina la carleen, nakumbuka rafiki yangu alinisihi sana nimkubalie maana demu ilisemekana mtoto kalewa na mimi harafu alikuwa ameanza kutangaza bwenini kwao kuwa mimi na date naye, sasa baada ya taarifa hiyo shida ilikuja kipindi kile mimi nilikuwa na wenge jingi plus utoto, basi kesho yake baada ya kupokea hiyo barua mimi nikaanza kuhisi kukosa amani maana watu walianza kunitania "baba carleen baba carleen" kutokana taarifa kuenea form two nzima na vidato vingene kwa sababu demu alikuwa famous kutokana kuwa kiongozi wa mazingira halafu kingine demu alikuwa pisi zile advance.

Bwanaee ishu ikawa inanipa ukakasi maana ilikuwa ndio mara yangu ya kwanza harafu pia nilikuwa nahisi kukukosa amani maana karibia shule nzima ilianza kunitania ovyo ovyo japo ya demu nilikua sijawai hata kuongea naye wala sikua nimempenda ila shida inakuja kadamnasi inashinikiza brigadier nitie saini ya kukubali.

Basi bana kuna siku ndio tulikua tumemaliza mtihani nakumbuka kuna jamaa mmoja lilikua likubwa halafu lina sifa likaenda kuwaambia form two wenzangu waje watukutanishe mbele ya form two wote eti kisa tuna viziana sana ,kweli nao watu wakarespond waka tukutanisha mbele ya dalasa.

Nakumbuka ilikuwa wakati mgumu sana kwangu maana ukicheck watu wamewazunguka wakiwatazama naye demu yuko mbele yangu anatazama chini kwa aibu ikanibidi na mimi ninyamaze kimya kwa sababu nilianza kusikia hasira kwa nini watu wanilazimishe kufanya kitu ambacho sitaki baada ukimya kupita kidogo bila mtu yeyote kumtamkia mwenzake yule jamaa lenye sifa likaniuliza kwamba je, nampenda carleen nikajibu hapana

Daah baada ya jibu hilo nilisikia mngurumo wa sauti za boys ukisema aaaaahhh naye demu akatoka pale akilia kuelekea bwenini kwao

Baada ya kama wiki moja kupita nikaanza kuexpiliance visa vizito kutoka kwa yule demu ukiachana shutuma za kuitwa hanithi Pia kuchafuliwa na propaganda et mimi sio riziki😂

Kwa vile demu alikuwa kiongozi akatumia nafasi hiyo kushawishi nipangwe kila siku morning speech na kila alhamisi niwepo kwenye debate yote hayo ni kunikomesha huku anajua fikra mimi english sijui pia ni muoga😂

Bado haikutosha akaanza kukamia siku ya dhamu yangu ya kufagia darasa alikuwa anafanya juu chini kupatikane kosa ili niadhibiwe na mwalimu bado hakuridhika na matokeo akahamia kwa marafiki zangu akamchukua mmoja wapo na kutangaza kuwa yeye ni bora kuliko mimi hapa ikafika kipindi hadi nikawa nataka nihame hata shule maana ule ugomvi nikama nilikuwa nimegombana na umoja wa NATO maana sio kwa vikwazo vile.

Ansante kwa kusoma mimi tayali nimeshare stori yangu basi kama kuna mtu wa jinsia yeyote aliyewahi kukutana na visa baada kukataa kuwa mpenzi wa mtu fulani wewe tuambie hili ni eneo free just mwaga udambwi tukumbushane kale

-good night-
Yaani noma mpaka uchawi ulihusika.
 
Umenikumbusha mipira ya utotoni uwanja umefurika fulu watu kushangilia, nikichezewa faulo kidogo utasikia sauti za walimbwende "msituumizie" Basi hapo mie HARUFU fulu kulewa sifa atakaekuja mbele yangu yaani fulu midaliz, mara mtu kavishwa, mara mtu kavuliwa.

Jamani
 
Back
Top Bottom