Je, umesikia nini cha nje ya Uwanja (Kamati za Umafia na Uchawi) kuelekeaa 'Mtanange' wa leo wa Simba SC na Kaizer Chiefs FC?

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
42,992
2,000
Nilizonazo hadi Asubuhi hii ni kwamba Wachezaji wa Kaizer Chiefs FC Usiku hawakulala Mbezi Beach bali wamelala Ubalozini Kwao na kule Hotelini Mbezi Beach wamebaki wale wasiocheza leo.

Nilizonazo hadi Asubuhi hii ni kwamba kuna aliyekuwa Kiongozi Mmoja wa Simba SC (sasa yupo Yanga SC) kwa Kushirikiana na baadhi ya Viongozi wa Timu nyingine Kubwa wanawapa Siri zote za Mbinu za Simba SC.

Nilizonazo hadi Asubuhi hii ni kwamba huenda kuanzia muda huu, kabla ya Mpira kuanza au Mpira ukiwa unaendelea kukatokea Tukio Kubwa (la Kutisha) likiwa ni sehemu ya ' MKAKATI PINDUA MEZA ' hivyo tujiandae Kisaikolojia na wala msishtuke nalo.

Nilizonazo hadi Asubuhi hii ni kwamba kumbe hata wao Kaizer Chiefs FC nao katika Mambo ya 'Kimafia' na 'Ushirikina' hasa Michezoni wako vizuri sana hivyo leo ' Majini ' ya Afrika Kusini na Tanzania ' yataumana ' vilivyo Benjamin Mkapa Stadium.

Nilizonazo hadi Asubuhi hii ni kwamba kama kuanzia Saa 5 Asubuhi hadi Saa 7 Mchana Mvua itanyesha Mkoani Dar es Salaam au Jiji kuwa na Wingu Kubwa mpaka muda wa ' Mtanange ' Kuanza Saa 10 Jioni basi MEZA ITAPINDULIWA KIBABE zaidi.

Nilizonazo hadi Asubuhi hii ni kwamba kuna Basi liliandaliwa ' Kimkakati ' ili liwabebe Wachezaji wa Kaizer Chiefs FC ambalo ' Mtaalam ' wa Morogoro ' alishalinuwiza ' vilivyo ( Jamaa ) wamelikataa baada ya huyo ADUI yetu Simba SC ( aliyewahi kuwa Boss wetu ) kuwaongoza kila sehemu na kuwapa SIRI zote.

Nilizonazo hadi Asubuhi hii ni kwamba kutokana na kwamba hata Wao Kaizer Chiefs FC kuwa wazuri Kiumafia na Kiushirikina ( huku wakisaidiwa na kuongozwa vyema ) na aliyewahi kuwa Boss wa Simba SC ( sasa yupo Timu Pinzani ) Mchezo huu unaweza kuwa Mgumu kwa Simba SC na hata tukishinda basi ni hizo tu Goli (Bao) Tatu (3) ambazo hadi sasa zipo ( zinaonekana ) Kiutabiri.

Hata hivyo wana Simba SC tusikate Tamaa kwani muda bado upo na Kamati mbalimbali za Kimafia na Kindumba ( Uchawi ) zipo Kazini na lolote linaweza kutokea kwani Simba SC ikilitaka Jambo lake hata iweje huwa linakuwa na Mifano ipo mingi hivyo nami GENTAMYCINE pia wala sina wasiwasi ( hofu )

Kama na Wewe una lolote ulilolisikia Asubuhi hii kuelekea ' Mtanange ' huu wa baadae tafadhali karibu Utiririke na Userereke nalo hapa ili nasi tujue na huenda tutatoa na Ushauri wa Kuboresha kutokana na Uzoefu wetu na hatimaye tuisaidie Simba SC yetu na Vita yake hii ya baadae.
 

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
47,934
2,000
Mganga kutoka Senegal amedai apewe kichwa cha mzungu pori meza itapinduliwa kipindi cha kwanza tu.

Hingera mkuu Genta kwa kutupa yanayojiri!
 

Asam

JF-Expert Member
Oct 11, 2011
237
500
Nizozisikia asubuhi hii ni,Simba wameroga ili mvua inyeshe kusaidia kupindua meza kibabe lakini Kaizer Chief wanazuia mvua isinyeshe.

Ni kweli muda huu nipo Mitaa ya Karume jijini Dar jua linaanza kutoka. Nimeambiwa eti Simba wakitengeneza mawingu,Kaizer Chief wanayapeperusha. Ama kweli leo itakua balaa.
 

Sibonike

JF-Expert Member
Dec 23, 2010
17,111
2,000
Simba anaweza kushinda lakini hazitafika nne. Kaizer nao watatupia moja au mawili.

Kwa mbinu hizi Africa tunashindwa nini kubeba kombe la Dunia?
 

KAGAMEE

JF-Expert Member
Dec 20, 2013
1,661
2,000
Nizozisikia asubuhi hii ni,Simba wameroga ili mvua inyeshe kusaidia kupindua meza kibabe lakini Kaizer Chief wanazuia mvua isinyeshe.

Ni kweli muda huu nipo Mitaa ya Karume jijini Dar jua linaanza kutoka. Nimeambiwa eti Simba wakitengeneza mawingu,Kaizer Chief wanayapeperusha. Ama kweli leo itakua balaa.
Hahaa mimi nishawaambia Kaizer ni wachawi kuwazidi wabongo watu hamuelewi.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom