Je, umeshawahi kusikia mtu anashitakiwa kwa kuzini na mke wake wa ndoa...? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Je, umeshawahi kusikia mtu anashitakiwa kwa kuzini na mke wake wa ndoa...?

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Mtambuzi, Jun 16, 2012.

 1. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #1
  Jun 16, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
  Hakimu akasema ndoa ya Mohamed ilikuwa na shangwe na zaidi ya hapo ilifanyika baada ya matangazo ya siku 21
  (Picha haihusiani na habari hii.)  Je, umeshawahi kusikia mtu anashitakiwa kwa kuzini na mke wake wa ndoa? Ni swali la kuchekesha kidogo, lakini ukweli ni kwamba, jambo hilo, limeshawahi kutokea.

  Wapi na kwa nani? Ilikuwa kwenye kesi ya Ramadhani dhidi ya Mohamed ya mwaka 1983 ukurasa wa 309 wa ripoti za sheriaTanzania (Tanzania Law Report).

  Kesi hii ilianzia mahakama ya mwanzo ambapo mtuhumiwa alishitakiwa na Mohamed kwa kuzini na Mwanaidi wakati mwanaidi alikuwa ni mke halali wa ndoa wa Ramadhani. Katika kesi hii Ramadhani alishinda, lakini Ramadhani alikata rufaa katika mahakama ya wilaya na rufaa hiyo alishinda.

  Lakini hata hivyo kwa uchungu wa kuporwa mkewe, Ramadhani naye alikata rufaa katika Mahakama kuu. Je, hukumu ilikuwa ni nini? Hebu tupate kwanza historia kamili ya kesi hii.

  Hukumu katika mahakama kuu ilitolewa tarehe 29 mwezi Julai mwaka 1983, na katika hukumu hiyo, jaji alisoma historia ya kesi na historia hiyo ilianzia Desemba 1978 ambapo Ramadhani alimuoa Mwanaidi Mwiru na walikuwa wanakaa wote kwa wazazi wa mwanamke na Ramadhani alimlipia mkewe mahari ya ng'ombe wawili.

  Mwaka 1980 Ramadhani alipata safari ya kibiashara na kwenda Endasak (bila shaka mkoani Arusha). Lakini mara tu bwana Ramadhani alipoondoka ndugu wa mke waliingiwa na tamaa na wakaamua kumwoza kwa mwanamume mwingine aliyeitwa Mohamed na ndoa ilifanyika tarehe 9 Julai 1980 kwa mahari ya ng'ombe watatu. Hata hivyo, ndoa hiyo haikudumu kwani mwezi Oktoba, 1980, walishindwana na Mwanaidi alirudi kwao na Mohamed aliahidiwa kurudishiwa ng'ombe wake.

  Mwezi wa Novemba, mwaka 1980, Ramadhani alirudi nyumbani kutoka katika safari yake ya kibiashara na alishangaa kuambiwa kuwa ndani ya miezi kadhaa aliyokuwa hayupo, mkewe alishaozwa kwa bwana mwingine. Ramadhani hakutaka maneno mengi, bali alichofanya ni kwenda nyumbani kwa kina Mwanaidi na akamchukua Mwanaidi na kuondoka naye hadi nyumbani kwake.

  Mwezi Aprili, mwaka 1982, Mohamed alimshitaki Ramadhani kwenye mahakama ya mwanzo, akidai kuwa Ramadhani alizini na mkewe (Mwanaidi)na hivyo anamdai fidia ya ng'ombe saba.Hata hivyo, madai yake hayo yalitupiliwa mbali na Ramadhani alishinda kesi hiyo na hakimu wa mahakama ya mwanzo alidai sababu ya kumpa ushindi Ramadhani ni kuwa ndoa yake ilitangulia, ingawa ndoa zote ni halali.

  Mohamed hakupendezwa na kushindwa kwake katika kesi hiyo, hivyo alikata rufaa kwenye mahakama ya wilaya na katika mahakama hiyo mambo yaligeuka na Mohamed alishinda kesi na sababu ya kushinda, hakimu alisema ni kuwa ndoa ya Ramadhani ilikuwa ya kimyakimya yaani haikuwa na "shangwe za harusi," hivyo ilikuwa ni batili na hata jamii haikufahamu kama Ramadhani alimwoa Mwanaidi, wakati ya Mohamed ilikuwa na shangwe na zaidi ya hapo ilifanyika baada ya matangazo ya siku 21 na ilifuata taratibu zote na hivyo ikajulikana na jamii nzima.

  Katika kipindi hiki kulikuwa na mvutano kati ya wanasheria, kama ili ndoa itimie ni lazima kuwe na sherehe. Wapo waliosema kuwa, sherehe ni lazima ili ndoa iwe ndoa, lakini wengine walisimamia zaidi vifungu vya sheria na kusema shangwe si lazima alimradi tu kuwe na makubaliano huria na ndoa iwe kati ya jinsia mbili tofauti zilizodhamiria kuishi maisha yote pamoja.

  Ramadhani hakufurahishwa na maamuzi hayo ya kuporwa mke wake yaliyofikiwa kwenye mahakama hiyo ya wilaya, hivyo naye alikata rufaa Mahakama Kuu.

  Katika mahakama kuu suala lililokuwa katika mgongano lilikuwa ni ndoa ipi ni halali kati ya ile ya Ramadhani na ya Mohamed? Na katika kufikia maamuzi, Jaji alitumia sheria kama inavyosomeka, ‘literal meaning' na hakuruhusu au hakutazama mazingira mengine katika kutafsiri maana ya ndoa.

  Katika sheria ya ndoa ya mwaka 1971 aliyotumia Jaji, kifungu cha 9 (1) ndoa inatafsiriwa kama muunganiko huria kati ya mwanamume na mwanamke waliodhamiria kuishi pamoja kwa maisha yao yote. Zaidi ya hapo Jaji alisema kwamba katika jamii ambazo zinafuata sheria za kimila, ndoa halali huweza kufungwa kwa kutumia sheria za kimila na kutokuwepo shangwe za harusi na kutokufuata milolongo mingine, hakuwezi kubatilisha ndoa hiyo kama viini vyote vya ndoa halali halalikama ilivyotafsiriwa kwenye kifungu cha 9 (1) cha sheria ya ndoa ya mwaka 1971 vipo.

  Jaji aliendelea kusema kuwa Ramadhani na mashahidi wake, akiwemo mshenga wake walithibitisha kuwepo kwa ndoa kati yake na Mwanaidi. Zaidi ya hapo Mwanaidi mwenyewe pia alikiri kuwa walifunga ndoa ya kimila na Ramadhani. Kwa kuongezea Mwanaidi alisema kuwa ndoa kati yake na Mohamed ilifanyika baada ya kulazimishwa na wazazi wake.

  Hivyo, kutokana na sababu hizo hapo juu, Jaji alisema kwamba, ndoa kati ya Mwanaidi na Ramadhani ilikuwa halali japokuwa haikuwa na shangwe na aliibatilisha ndoa kati ya Mwanaidi na Mohamed.

  Kwa kuongezea Jaji alisema kuwa sheria zetu haziruhusu mwanamke kuolewa na wanaume wawili kama inavyoonekana kwenye vifungu 15 (3) na 152 (1) vya sheria ya ndoa ya Tanzania ya mwaka 1971.

  Kwa kumalizia Mahakama Kuu ilisema kwamba mahakama ya mwanzo haikufanya makosa kwa uamuzi iliyotoa, ingawa ilikosea pale tu iliposema ndoa zote ni halali. Hivyo, rufaa ilikubaliwa na Ramadhani alirudishiwa mkewe na Mohamed alitakiwa kulipa gharama za kesi hiyo.  Naomba MODS kwa hisani yenu musihamishe habari hii kwa sababu inahusu sana mambo ya mahusiano na ndoa kwa ujumla.........
   
 2. Blaine

  Blaine JF-Expert Member

  #2
  Jun 16, 2012
  Joined: Jan 11, 2012
  Messages: 2,285
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  sijawahi. ila nimesikia mtu aliyembaka mkewe wa ndoa na akafungwa
   
 3. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #3
  Jun 16, 2012
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Ipo ile ya kumbaka mke wake wa ndoa
   
 4. Mwita Maranya

  Mwita Maranya JF-Expert Member

  #4
  Jun 16, 2012
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 10,569
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Tatizo ni ndugu/wazazi wa mwanaisha kumgeuza kitega uchumi. Baada ya kumaliza ng'ombe wawili wa Ramadhani wakaona bora wavute wale watatu kutoka kwa Mohamed.

  Hukumu ya hakimu wa mahakama ya mwanzo na mahakama ya wilaya zote zinaonyesha uwezo duni sana wa mahakimu katika kufikia judgement. Na huu ndio ushahidi wa wazi wa namna watanzania masikini wanavyokosa haki zao katika mahakama zetu kutokana na umbumbumbu wa mahakimu.
   
 5. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #5
  Jun 16, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,873
  Likes Received: 6,226
  Trophy Points: 280
  duh.....hapo ndo umuhimu wa kufuta mahari unapoonekana....
   
 6. Bazazi

  Bazazi JF-Expert Member

  #6
  Jun 16, 2012
  Joined: Aug 18, 2008
  Messages: 2,029
  Likes Received: 560
  Trophy Points: 280
  Hii nimeipenda sana. Vipi Ramadhani aliendelea na mkewe kweli au vipi.

  Nyie wanawake alichokifanya mwenzenu ni sawa kweli au ndio mlitaka kuanzisha POLYANDRY (polygamy in which a woman has more than one husband. Compare with polygyny).

  Wazazi wa mwanamke ni PAMBAF.

  Bazazi ni Bazazi!
   
 7. MadameX

  MadameX JF-Expert Member

  #7
  Jun 16, 2012
  Joined: Dec 27, 2009
  Messages: 7,847
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  Hii kesi ingewahusu zaidi wazazi wa mke maana alifanywa ni kitega uchumi. Pili waliozeshwa kivipi, kimila au kidini, kama ni kidini kuna masharti yake baada ya mke kutaka ndoa ivunjike. Mimi nahisi wahusika wote mataahira, hao waume, mke na wazazi wa mke.
   
 8. E

  Elizabeth Dominic Platinum Member

  #8
  Jun 16, 2012
  Joined: Dec 7, 2007
  Messages: 4,547
  Likes Received: 52
  Trophy Points: 145
  Yaani hawa hawakufuata protokali kabisa.................hawa wazazi hawafai, kwa kuona Ramadhani kaondoka kitambo ndio labda wakaona wajitengenezee kipato wamemkuta Rama naye ngangari kwa kujua haki zake bwana Mohamed naye msumbufu tu mke si alikuwa ashashindwana naye
   
 9. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #9
  Jun 17, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,305
  Likes Received: 418,552
  Trophy Points: 280
  Mohamed was a victim of circumstances.................siyo kubaka huko kama mhusika kadanganywa..........inakuwaje wakati yeye hajui linaloendelea
   
 10. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #10
  Jun 17, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,305
  Likes Received: 418,552
  Trophy Points: 280
  [MENTION]
  Elizabeth Dominic[/MENTION] tusisahau na huyo mke kwa kisa kipi alikubali kuolewa mara mbili mbili kama siyo tamaa ya kipande cha mkate?
   
 11. M

  Mwanaweja JF-Expert Member

  #11
  Jun 17, 2012
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 3,576
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  alitakiwa kutembeza kichapo kwa wazazi wa mwanamke
   
 12. farkhina

  farkhina Platinum Member

  #12
  Jun 17, 2012
  Joined: Mar 14, 2012
  Messages: 12,831
  Likes Received: 775
  Trophy Points: 280
  hee hiyo ndo suluhu?
   
 13. HorsePower

  HorsePower JF-Expert Member

  #13
  Jun 18, 2012
  Joined: Aug 22, 2008
  Messages: 3,617
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 145
  Duu hii ni kali. Ni jambo la kawaida kwa mwanaume kuoa mke zaidi ya mmoja ila kwa mwanamke mmoja kuolewa na zaidi ya mwanaume mmoja, hii sijawahi sikia.

  Hapa nizungumze kipuuzi kidogo, Labda kwenye hiyo kesi, wangewauliza kama hao wanaume wote wako tayari kuishi na huyo mwanamke mmoja na kama wako tayari basi vifungu vya sheria virekebishwe na mke apewe nafasi ya kuolewa na mume zaidi ya mmoja kama ambavyo mwanaume anavyooa mwanamke zaidi ya mmoja! Hapo haki sawa za beijing zingekuwa zimeshika hatamu! Just a joke!!!

  Lakini nimejifunza kuwa kumbe kwenye ndoa ni muhimu kutangaza na kufanya sherehe japo ndogo ili mradi upate mashahadi wa kukutolea ushahidi wakati wa migogoro ya ndoa kama hivi, na si kuwaalika kwa ajili ya kuja kula tu na kufurahi pamoja nawe, hili sikulitambua kabisa, loh!
   
 14. NATA

  NATA JF-Expert Member

  #14
  Jun 19, 2012
  Joined: May 10, 2007
  Messages: 4,516
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Mh matatizo ya kumfanya mwanamke bidhaa ndio haya.lol!

  Baba kaona stock iko ndani japo ilishalipiwa kaamua kuiuza kwa bei zaidi.
  Labda alijua mwenyewe akija atadai arudishiwe mali, angepewa ng`ombe wake wawili mzazi angepata cha juu wale watatu.

  Wakishtakiwa hapa walikuwa wale wazazi kwakosa la kujipatia mali kwa udanganyifu
  Yule dada kama kweli alilazimishwa pole zake..
   
 15. Ronn M

  Ronn M JF-Expert Member

  #15
  Jun 19, 2012
  Joined: May 2, 2012
  Messages: 1,283
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Kuna wakati ' marriage ceremony' was a big issue. But now the law is settled!
   
 16. sinafungu

  sinafungu JF-Expert Member

  #16
  Jun 20, 2012
  Joined: Feb 13, 2010
  Messages: 1,406
  Likes Received: 569
  Trophy Points: 280
  duuuh hii kali, ila inaonekana huyo mwanaidi alikua bomba kwelikweli, kwa upande mwingine neno KUZINI mara nyingi linatumila ni tendo nje ya ndoa , kwa hiyo mkeo huwezi kuzini naye bali UNAMUINGILIA AU MNAINGILIANA
   
Loading...