MNDEE
JF-Expert Member
- Jul 10, 2009
- 491
- 68
Kijana wa umri wa miaka 17, mweusi na mrefu amepotea toka saa kumi jioni jana Jumanne June 4. Mara ya mwisho alikuwa amevaa kaptura nyeusi na flani yenye mistari. Jina lake ni Junior, ana matatizo na haongei (autistic), lakini anaelewa ukimuita jina na pia anaweza kufuata maelekezo rahisi.
Alitoweka toka nyumbani kwao maeneo ya Science Kijitonyama jana. Mara ya mwisho alionekana Tandale uwanja wa mpiria.
Polisi wamekataa kutoa msaada wowote wanadai mpaka yapite masaa 24, tatizo mtoto ni mgonjwa sio mtu mwenye uwezo wa kufanya maamuzi mwenyewe au kurudi nyumbani. Kama kuna kiongozi wa Polisi hapa, au kama unaweza kutusaidia tutashukuru.
Kama utamuona kijana huyu maeneo ya Tandale, Kijitonyama, Sinza, Mwenge au popote pale tafadhali toa taarifa kituo chochote cha polisi pia unaweza kuwasiliana nasi kwa namba hii xxx-xxxx-xxx unaweza au niPM.
Tunahitaji maombi na tunatanguliza shukrani zetu. RB ya hii issue ni XXXXX
UPDate

Wanajamii, naona niwapatie details zaidi muelewe kilichotokea napengine itakuja saidia mtu mwingine.
Kijana alipatikana hivi - mama mmoja msamalia mwema jana alikwenda hospitali ya Amana kumjulia hali mgonjwa , akiwa pale akasikia manesi wanamuongelea mgonjwa mmoja kuwa atapelekwa jela ya watoto kesho ( leo Jumamosi) kama ndugu zake hawatamchukua. Alipomuona kijana anayeongelewa akakumbuka aliwahi muona Kijitonyama. To cut the long story short yule mama akampiga picha kijana, akaanza safari ya kusaka wazazi wake nyumba hadi nyumba akionyesha picha kila alikopita hatimae akafika nyumbani kwa sister.
Unofficial report kijana alifikishwa pale na polisi siku aliyopotea, ana majeraha kichwani na miguuni assumption atakuwa alipigwa. Amana ni moja ya hospitali ndugu walipita zaidi ya mara moja kumtafuta, kila walipokwenda waligomewa kuingia wodini na kuishiwa kuambiwa kijana hayupo pale.
Baba kijana alirudi mara nyingi kituo cha polisi alichoripoti kupotea kwa kijana wake kuona kama kuna aliyeripoti kitu. Kila alipofika kituoni ilibidi aanze story upya. Hii ina maanisha nini – unapotoa ripoti polisi wakiandika ile ripoti chances are inaishia kwenye droo, hivyo wanapobadilishana shift hiyo ripoti yako si sehemu ya makabidhiano. Hivyo atakapokuja mtu kutoa taarifa itakayokusaidia haitakufikia.
What to take from this - juhudi binafsi na kujitoa kwa raia vinahitajika katika masuala ya jamii na matukio ya namna hii. The system is broken, branch za serikali haziko connected. Most probably ukiripoti kitu au kufuatilia kitu kwenye branch ya serikali mfano ukiambiwa jaza form, or ngojea ‘RB' masaa 24 ni fomality tu. Pia persistence inahitajika sana, usikate tamaa na uwe na imani na Mungu wako.
Ahsanteni sana kwa maombi na kwa kutia moyo.
Mndee