Je umekuwa ukidai risiti pindi ukiuziwa mafuta ya gari

NgomaNzito

JF-Expert Member
Jan 10, 2008
559
26
Kumekuwepo tabia ya watu wakifika kwenye kituo cha mafuta ni kuvuta kifuniko cha tank na kujaziwa mafuta baada ya kupimiwa huondoka.
Jambo hili ni la hatari sana kwani kama ukipata madhara kwenye gari lako hutaweza kudai gharama ya matengenezo iwapo huna kidhibitisho hata wale mafisadi EWURA wametoa tangazo hili

"Pia inaelekeza mnunuzi kuhakikisha anapata stakabadhi ya malipo inayoonyesha jina la kituo, tarehe na aina ya mafuta aliyonunua na bei kwa lita kwani ndiyo kidhibiti endapo yanajitokeza malalamiko ya ama kuuziwa kwa bei ya juu kuliko ya kikomo au kuuziwa mafuta yasiyokuwa na kiwango."

Je wewe huwa unadai risiti????
 
watanzania hawana utamaduni wa kuchukua risiti, sio katika mafuta tu bali kila kitu
 
Kumekuwepo tabia ya watu wakifika kwenye kituo cha mafuta ni kuvuta kifuniko cha tank na kujaziwa mafuta baada ya kupimiwa huondoka.
Jambo hili ni la hatari sana kwani kama ukipata madhara kwenye gari lako hutaweza kudai gharama ya matengenezo iwapo huna kidhibitisho hata wale mafisadi EWURA wametoa tangazo hili

Je wewe huwa unadai risiti????

Nimeifurahia sana hiyo `red` hapo juu.

Ukiona mtu anadai risiti ujue ni gari la serikali au la anawajibika kwa mwenye gari, lakini katika hali ya kawaida, hakuna mtu anadai risiti, na wengi wao hata wakiharibikiwa magari hawana ujasiri wa kurudi Petrol
station.
Mimi binafsi huwa nadai.
 
Naamini ni vyema petrol stations zote wakawa na elctronic ticket machine kama za supermarket, ili kupunguza msongamano wa magari kwa watu wanaotaka risiti......
Naamini kama ingekuwa hivyo, watu wengi wangechukua risiti.
 
aah wapi kwa wanaodai ni mmoja katika watu 20 mi nashuhudia kila leo ukiona anadai basi ujue ni serikali au anawajibika na ofisi au ni yule ambaye anatumia gari yake lakini mafuta analipiwa na kampuni zaidi ya hapo hakuna mwenye utaratibu huo,tena hata yule anayelipiwa mafuta na kampuni akiwa kazini lakini akiwa kwenye shughuli ake binafsi anawea kuweka mafuta bila kudai risiti kisa ni pesa ambayo haiwezi kurudi kwake.! LABDA WAWEKE TANGAZO KWENYE PAMPU TENA LIWE JIRANI NA ILE READING METER UKINUNUA MAFUTA DAI RISITI.
inashangaza san hili jambo.
 
Hata hivyo wale wanaodai risiti mara nyingi huwakatia ganji wauza mafuta waandike kiwango kisicho halisi wakarudishiwe hela nyingi huko maofisi kwao

Sasa wakikuwekea mafuta yaliyochakachuliwa gari likiharibika ujue limekula kwako
 
Nimeifurahia sana hiyo `red` hapo juu.

Ukiona mtu anadai risiti ujue ni gari la serikali au la anawajibika kwa mwenye gari, lakini katika hali ya kawaida, hakuna mtu anadai risiti, na wengi wao hata wakiharibikiwa magari hawana ujasiri wa kurudi Petrol
station.
Mimi binafsi huwa nadai.

PakaJimmy, kwahiyo wewe unaendesha gari la serikali au umeajiriwa na unawajibika kwa mwenye gari?

Ni kweli watu waliowengi huwa hawadai risiti ila mimi sijawahi kununua mafuta ya gari langu hata siku moja na nisidai risiti.
 
Au anataka kuongeza cha juu kwenye mafuta apate pesa kukamilisha siku! lakiikila mtu akidai risiti patakuwa hapatoshi. either bei itapanda maana wenye vitu watadai gharama za uendeshaji zipo juu. Risist ni muhimu sana maana hi chakachua inaua sana magari
 
Kuchukua risiti ni optional na wala si lazima, hakuna sheria inayomtaka mnunuzi achukue risiti). Isipokuwa kuandika risiti (kuweka mauzo katika leja ya mauzo) kwa muuzaji ni lazima kwa mujibu wa sheria za kodi ya 1973.

Hilo la pili juu ya kufidiwa kama kama gari limpata matatizo, lipo 50/50 au kinadharia sana, kwani utahitaji zaidi ya uthibitisho wa kitaalam zaidi na si risiti. Madai hayo kwa kutumia risiti ni mepesi sana.
 
Hayo ulioandika hapo juu ni kweli? Sheria ya kodi haimtaki mnunuzi kuwa na risti? Hivi sheria za VAT, ukiachilia mbali hiyo sheria ya kodi ya mwaka elfu moja mia tisa sabini na tatu haimuhitaji mtu kuwa na risti ya manunuzi mara anunuapo kitu?
Nadhani umetudanganya!
 
Mkuu soma vizuri post yangu. Hakuna sheria yeyote inayomtaka mnunuzi KUCHUKUA risiti, kama ipo basi ilete hapa tunufaike sote.
Ninarudia kuchukua risiti ya mauzo ni 'optional' ukitaka unachukua kama hutaki hakuna atakayekulazimisha kuichukua. Isipokuwa muuzaji anatakiwa kwa mujibu wa sheria kuingiza mauzo yote kwenye leja yake.
 
Bahati mbaya ni kuwa ingawa TRA wamekuwa wakituhamasisha kudai risiti mara tu baada ya kufanya manunuzi lakini mila hii kwetu haipo matokeo yake siyo hayo tuu ila hata serikali kukosa mapato stahili na sisi wananchi kulalamika maramara barabara mbovu, shule zetu ziko katika hali mbaya serikali haifanyi hivi au vile . Eboo hela sirikali itapata wapi? na kama ulichonunua kimekuletea hasara inakuaje?? Nadhani wengi wetu tuna PHD katika kulalamika lakini katika kutimiza wajibu ni matatizo [na huu nao ni ufisadi??]
 
Naamini ni vyema petrol stations zote wakawa na elctronic ticket machine kama za supermarket, ili kupunguza msongamano wa magari kwa watu wanaotaka risiti......
Naamini kama ingekuwa hivyo, watu wengi wangechukua risiti.

BIGBON KARIAKOO ZINATOKA ELECTRONICALLY MUUZAJI AKIKATA AMKABIDHI MPOKEA MAFUTA ANA AAMBULIA MOSHI....SI UHARIBIFU WA MAZINGIRA HUO ATIMAE ZINATUPWA
 
Back
Top Bottom