Je, ulishawahi kushuka na begi/mzigo wa abiria mwenzio kwa bahati mbaya? Mtu aliyeshuka na box langu la samaki mwaka 2012 sasa ni family friend

Mwaka 2016 haraka haraka na furaha ya kufika home salama,nikabeba begi la mdosi pale Jnia,nafika home nafungua nakutana na tambuu na zagazaga zingine za kidosi Duu nikapagawa mbaya,begi langu lilikuwa na mazaga yangu kibao na zawadi za madogo!.
Wadosi kwa pilipili ni shiiiida. Haukukutana nazo humo mkuu?...
 
Niliingia kanisani kusali nikaweka baskeli nje ila nilisahau kuifunga baada ya sala kumaliza kutoka nje naiona baiskeli ipo na nikashangaa sana haikuibiwa maana ni nilisahau kuifunga ,basi nikaamua kurrudi kanisani kwenda kushukuru kwa mungu kwa kuikuta basikeli yangu ipo salama, wandugu kutoka baiskeli haipo, ,.
Alafu hapo ni nyumba ya ibada (Kanisani), sasa jenga picha ingekuwaje kama huko uswahilini. Ifike wakati watu wawe wanaheshimu pahala patakatifu.
 
mim
Habari za wakati huu kaka na dada zangu wote wa hapa JamiiForums.

Ndugu zangu watanzania;

Je, ulishawahi kushuka na begi/mzigo wa abiria mwenzio kwa bahati mbaya? Mtu aliyeshuka na box langu la samaki satto mwaka 2012 sasa ni family friend.

Kuna kamsemo kamoja huwa kanatamba sana huku mitaani uswahilini kwetu kwamba kuibiwa mume inauma sana kuzidi maumivu ya jino.

Kwa mfano labda ningekuwa nimemuoa Bushmamy alafu aje kugundua mimi mumewe Soldier ninaibwa na jimama kama witnessj vile eti maumivu yatakuwa makali kuzidi jino linavyouma nyakati za usiku.

Wooote wanaosema na kuushadadia msemo huu mimi ninawaona kama hawajui nini maana ya maumivu. Hivi unayajua maumivu ya mtu kushuka na mzigo wako wa thamani katika safari?

Yaaani umechaguliwa kujiunga na chuo cha SAUT huko Mwanza alafu unapokuwa safarini kwenda ku-report abiria mwenzio anashuka na begi lako uliloweka vyeti vyako vya form four na form six.

Hivi unayajua maumivu ya mtu kushuka na mtoto wako wa miaka 2 njiani baada ya kumuomba akubebee ndani ya daladala ya Mbagala - Kariakoo?

Mimi yalinikuta mwaka 2012. Baada ya kupata taarifa za kifo cha baba yangu mdogo nikiwa Dodoma ikanibidi kufunga safari mpaka Wilaya ya Rorya mkoa wa Mara.

Shughuli za mazishi zilienda kama zilivyopangwa hakika Mungu alikuwa ni mwema katika hilo lakini kwa bahati mbaya mama yangu hakuweza kufika kwa sababu kadhaa za kiafya kama ujuavyo watu wazima.

Kabla sijaanza safari ya kurudi Dodoma nimalizie michoro yangu alafu niende Dar kupumzika mama akanipigia simu akinisisitiza kwamba nipitie Bunda kwa shangazi mdogo wake na baba nimbebee samaki wake satto waliokaangwa vizuuuuri kabisa.

Sawa, nikasema isiwe kesi mimi huuyooo kutoka Tarime mpaka Bunda nikabeba samaki kisha nikasepa mpaka Mwanza nikalala siku moja pale guest moja ya Buzuruga kisha asubuhi huyo na bus la kuja Dodoma.

Bus ilikuwa inakuja mpaka Dar sasa mimi nilikata tiketi ya Dodoma kwa maana nina issues zangu huku. Nimeshuka ninapewa kondakta anatoa mizigo ya abiria kuangalia box langu halipo.

Daaaaah aiseee moto ulitaka kuwaka. Samaki hawapo? Nitamwambia nini bi mkubwa nikirudi Dar? Kumbe baada ya ukaguzi mzuri ikaja kugundulika kuna abiria mmoja alishukia huko Singida alikuwa na box kama langu ndio akaondoka nalo lakini yeye box lake likawa limebaki pale kwenye bus.

Alichokifanya kondakta akachukua lile box la abiria mwingine kisha akalipeleka ofisi zao kuu pale Dodoma akaniambia wewe nenda home ukalale kisha njoo baada ya siku mbili tutakupigia simu na utalikuta box lako la samaki hapa.

Sawa kwa kuwa ilikuwa ijumaa nikaenda jumapili asubuhi mida kama ya saa tano kasoro hivi nikakutana na yule yule jamaa aliyechukua box langu akiwa pale pale ofisini.

Baada ya kupiga story kadhaa nikaja kugundua kumbe anafundisha shule moja na mtoto wa mama yangu mkubwa pale pale Singida. Nilikereka lakini nikapata funzo moja.

Nikiwa ninasafiri begi/mzigo wangu unakaa katika boti ya pembeni inayotazamana na dirisha nililopo kiasi kwamba hata watu wakiwa wanashuka njiani ninakuwa ninaona ni nani anateremka na mzigo upi.

USISAHAU: ENDELEA KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USICHAFUE TASWIRA NJEMA YA TAIFA LAKO. USTAWI WA NCHI YETU UNAANZA NA WEWE. TIMIZA WAJIBU WAKO IPASAVYO.
i nilishawahi kuibiwa demu kwenye daladala
 
Niliwahi kuchukua begi la Mwanafunzi mmoja aisee mpaka huruma kizuri ni kuwa kulikuwa na mawasiliano ya Mama yake hivyo nilimtafuta Kisha akalifuata.
 
Niliwahi kuchukua begi la Mwanafunzi mmoja aisee mpaka huruma kizuri ni kuwa kulikuwa na mawasiliano ya Mama yake hivyo nilimtafuta Kisha akalifuata.
Daaah, noma sana mkuu. Begi la mwanafunzi si unakutana na madaftari na penseli tu humo mzee baba
 
Kuna siku Songea tumekesha bar Planet sijui bado ipo! Asubuhi nikaunganisha na superfeo hadi Njombe. Wakati natoa bag nikachukua ambalo sio langu, nikapanda bus za kwenda Ludewa.
Kufika milima ya gangitoroli nikapokea simu kuwa tumechanganyana mabag, mwenye langu kaliweka ofisi za superfeo kwa hiyo nitalikuta pale.
Nilivyofika kituo cha nyumbani nikaliacha tu stand kwa jamaa then nyumbani nikaenda kama le baharia yaani sina kitu mkononi hata peni.
Siku ya pili nikalipitia na kwenda kubadilishana Njombe.
Mkuu, hivi Njombe mpaka Songea ni kama KMs ngapi hivi?
 
Huu ni uzembe mkubwa sana, iweje usijue begi/mzigo wako ulivyo?

Unatakiwa kuweka alama na uwe macho gari linaposhusha watu/mizigo njiani.
Kuwa macho inakuwaga ngumu kwa maana kuna muda mtu anakuwa amesinzia au yupo dirisha la upande tofauti na boot ya gari ilipo
 
Mwaka 2016 haraka haraka na furaha ya kufika home salama,nikabeba begi la mdosi pale Jnia,nafika home nafungua nakutana na tambuu na zagazaga zingine za kidosi Duu nikapagawa mbaya,begi langu lilikuwa na mazaga yangu kibao na zawadi za madogo!....fasta nikarudi airport nikalikuta begi langu pale lost and found kwa Swissport....kumbe mdosi alivyoona begi sio lake akaliacha pale....kwa mazaga yale ingekuwa mbongo mhh sijui....
Mkuu, Mdosi hakuweka hata dollars kadhaa katika begi? Ungezikuta ungerudisha begi?
 
Mimi katika harakati zangu. Nilitoka Unguja kufika bara. Kushuka kwenye boti pale bandarini. Vijana wa Azam wameniambia mizigo yote unayifwata mbele ya mlango wa kuelekea Custama. Mie nimetii naelekea sehemu iliomwaga mizigo ya abiria... Vijana wa pale bandarini wanachagamkia kugombania mizigo ya kubeba. Vijana wawili wamejitokeza wamechagua begi langu. Moja kati yao amesema ndo hilo livute. Na mimi nimenyamaza nawangalia kwa jicho la huruma ila aliekuja kuharibu shoo yote ndo ule niliefwatana nae.
Hii ni shiiiiida mzee baba...
 
2020 nko kati ya mikoa ya kanda ya ziwa nasubr prvate kuja mwanza nko na mtoto wangu wa kiume nmebeba beg lake la nguo mgongon ikaja noah ile kupanda nkaona beg nlweke kwa nyuma kumbe kule nyuma kuna beg pia lnafanana na langu vile vile tumefka mwanza jamaa kasema anaenda kulala hotel mabatin nkaona sio mbaya ntashuka apo npande hais mpaka buzuruga tukafka apo kwenye hotel nkashuka kuchukua beg na kusepa na mtoto ile nafka hom kama saa nne na nus iv usku mtoto ashaoga fungua beg nakutana na masurual makubwa balaaa smart phone kama 20 iv na n mpya walkua wanaproject ya kukusanya data mwanza nkaona apa kulko nkabak na hz cm n bora nfate nguo za mwanangu mana uez jua akili za walimwengu ikabd nrud usku uo uo mpka kwenye io hotel jmaaa wameshaingia kulala mm nakomaa kugonga hata hawajui kama wamebak na vipens vya mtoto wale jamaa wakashukuru tukapeana namba wkend n kutafutana na kula bia mpka kuziangalia
 
Back
Top Bottom