Je, ulishawahi kukutana na kitu cha kutisha usiku? Pita hapa tupeane uzoefu

Da'Vinci

JF-Expert Member
Dec 1, 2016
35,789
107,270
Je ulishawahi kutana na kitu cha kutisha usiki kama mchawi, jini, mnyama basi share na sisi tukio lako hapa. Nianze mimi;

Iikua mwaka 2007 nipo na washkaji wawili tumetoka kucheki muvi za usiku saa saba, katika tembea yatu ana kwa ana tunakutana na "JOGOO" nikisema jogoo jogoo kweli kwa ukubwa alikua kimo cha kondoo. Bwanaa wee mbio tulizokimbia kushinda zile za kwenye muvi ya KUNG FU HUSTLE jogoo alituunganishia mpaka karibu na nyumbani kabisa, mpaka leo hua najiuliza sijui atakua yule aliyembeba Pazi shule ya msingi? Toka siku hiyo nilikoma kutembea usiku.
Hiyo ilikua Kigoma.

Tukio la pii.
2012 tukiwa tumetoka kwenye magroup yetu ya kujisomea usiku tunawasindikiza majamaa gheto kwao wakati tunarudi tukakutana na Ndama wa mguu mmoja aisee tulikimbia mlango wa nyumba tuliufungua kwa Buti la Shaolin soka. Toka siku hiyo kuanzia saa nne usiku hunitoi nyumbani hata kwa dawa.

Please share na wewe.
 
Hii iliwakuta washkaji zangu, walikua wanakatiz makaburini, walichokiona sio mchezo, ni mbio za Usain Bolt
 
vitu vya kutisha havipo usiku tuu ,hata mchana kweupe vinaweza kukutokea,miaka flan tulipata tenda ya kupeleka mzingo kigoma/kakonko na tulipofika ili bidi tukae kama wiki hivi tukingoja mzigo wa kuludi dar es salaam bhas kuna siku tukaingia Bar flan ilikuwa mapema tuu asbuh dah ilipofika mchana tukawa tushakolea vyombo kichwani ikiwa ni mixer ya safari lager na the kick tukaona tukaona madada poa tukapumzike ila kwa mchana ule hawakuwapo so tukabahatika kutongoza akina mama waliokuwa wamekaa pembeni yetu na tukakubaliana bei then tukaanza safar ya kuelekea guest....dah kufika guest kila tulipotaka kuwaingilia vitendea kazi vilisinyaa kabisa,kwakuwa na sisi tulikuwa wahuni kuna mambo tulikuwa nayo yakasaidia viungo kuinuka ila kilichofata jinsia zao zimekuwa za kiume aisee tulitoka guest bila viatu na mashat tulivalia nje.........1998
interesting
 
Ha ha ha ha ha. Duh!!! Sisi tulikuwa tukitembea tunatishana tu nyoka huyo aisee mnakimbia halafu aliewashtua anabaki anacheka tu. Sijawahi kutana na vibweka usiku may be kwa sababu sitembeagi late hrs
 
1997 Vi-form 1 wenzangu wananitambia kuiona movie ya PREDATOR (Anorld ya jini) kwenye kibanda umiza,nikailaani sana mifugo (mbuzi)waliosababisha niwe malishoni wakati wenzangu wako wanafaidi mikwara ya akina BILLY DUKE...ikapita kama wiki hivi hiyo muvi ikawa inaoneshwa tena ila bahati mbaya inawekwa usiku kuanzia saa 4 mara tu baada ya trela la Alain Kounkou....
Home- ruhusa kama hiyo sahau kupewa (kutembea usiku?!)....nikajiapiza kutoikosa siku ya leo hata iweje,....Ili nifanikiwe lengo mzee nikalihujumu dirisha la chumbani kwangu kwa kung'oa nondo moja ili nipate pa kutokea pale familia nzima ikiwa imelala...
Saa 3 tayari raia wote wanakoroma,starling nikalinyatia dirisha nikajikuta niko nje,...ndani ya dk 5 nikawa nimejumuika na watu wazima holini tunamalizia album ya R.A.S (Alain) ili muvi lianze...muvi likaanza, muvi likaisha,nikaridhika...
Kutoka nje giza totoro....njia ya kwenda home mwendaji ni mimi tu,sina kampan coz tulikuwa tunakaa kwenye kota za shule alafu zimejengwa mbali na kijiji (Kunaitwanga Mahuta-Mtwara)...
Kijiji usiku huu kiko kimyaa,nyayo zangu tu ndo zinatoa sauti...kuna kipande cha msitu kinachotenganisha eneo la shule na hiki kijiji (hilo ndo eneo pekee nililolihofia kabla hata sijalifikia)....sasa wakati nazimalizia hizi nyumba za mwisho-mwisho ili niukabili huu msitu,mita kama 7 hivi kulia kwangu,kati ya nyumba moja na nyingine (zote zimeezekwa kwa nyasi) nikaona kundi la watu wako uchi,wako wima, wametengeneza kamduara hivi,wako kimya...BWANA BWANA wee...
Kuna kitu kama shoti ya umeme hivi iliyonifanya mwili,nywele visisimke kwa pamoja na nikauona mwili kama hauko na mimi vile...huku nikiwa nimesimama,moyo unataka utoke nje kwa mapigo ya KUDU-KUDU,nikiwa sijui la kufanya maana lile kundi nahisi lilikuwa bado halijaniona 'mwana mzurura usiku'... (vyote hivyo ni ndani ya kama sekunde 5 hivi)...
Mara kwa pamoja (utadhani waliambiana) kundi lote lile wakageuza vichwa vyao na kunitazama fwaaa......
Nakumbuka nikasema "Mawee" bila kutoa sauti (nikijua saasaa nyama ya mtoroka kwao inaenda liwa punde) na kufuatia na mbio za kukimbilia vidole/kama sio kucha pasipo kugeuka nyuma...nyumbani nikapitiliza,mbwa wa home akaanza kubweka na yeye akaniungia tela kimyakimya akijua tunacheza,nikajua hapa naenda chaka,nikageuza...mbio hadi dirishani...sikujali nani atasikia ninavyoingia au lah,...narukia dirishani,mbwa naye anavuta suruali kwa chini(huyu dog alikua best angu sana)baada ya zile kukuru-kakara za kuingia ndani...nikajikuta niko kitandani nahema kwelikweli, tena kwa nguvu,koo limekauka, huku mguu mmoja unaning'inia dirishani suruali inaendelea kuvutwa na mbwa nje......
 
Ila hiyo imenitisha na ninavyoisoma usiku huu..
Ila kigoma mambo hayo ni hatari..
 
Ha ha ha ha haaaaaaaa.... Noma sana!!!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom