Je, ulishawahi kukutana na Ambulance kwenye kituo cha mafuta (Sheli)

radiation

JF-Expert Member
May 28, 2013
241
254
Nimeendesha gari kwa miaka kadhaa sasa lakini sijawahi kubahatika kukutana na gari la wagonjwa likiwa sheli, ni mimi tu au kuna aliyewahi kuona Ambulance ikiwa sheli?
 
Nimeendesha gari kwa miaka kadhaa sasa lakini sijawahi kubahatika kukutana na gari la wagonjwa likiwa sheli, ni mimi tu au kuna aliyewahi kuona Ambulance ikiwa sheli?
Unalenga kusema nini haswa ?
Kutobahatika kuiona sheli ikijaza mafuta haina maana kwamba magari hayo huwa hayaingii sheli
Ni magari kama yalivyo magari mengine
Yanaenda garage
Yanaingia sheli kunywa mafuta
N.k
 
mm nimewai kuona mwaka jana mwanza
nje ya bugando hospital kuna petrostation,,nilionea hapo ikinywa mazutu(mafuta)
Nimeendesha gari kwa miaka kadhaa sasa lakini sijawahi kubahatika kukutana na gari la wagonjwa likiwa sheli, ni mimi tu au kuna aliyewahi kuona Ambulance ikiwa sheli?
 
Nimeendesha gari kwa miaka kadhaa sasa lakini sijawahi kubahatika kukutana na gari la wagonjwa likiwa sheli, ni mimi tu au kuna aliyewahi kuona Ambulance ikiwa sheli?
Kwa yeyote anayefanya kazi halmashauri anaweza kujua mfumo wa utoaji mafuta kwa magari ya idara mbalimbali ikiwa ni pamoja na ambulance ambazo ziko idara ya afya au zikiwa chini ya hospital husika. Kunakuwa na tank za mafuta stoo za halmashauri au kwenye hospital ili kuwa na uhakika wa mafuta, lakini pia kuratibu matumizi ya mafuta ktk magari.
 
Kila leo tunaweka pamoja nayo mafuta binafsi nimeshaona sana tu,sema walio wengi utakuta jioni sana kuelekea usiku baada ya kutwa nzima huenda kujazilizia tena full tank kiasi kwamba mchana wote litapiga mishe zake za full tank aliyoweka jana usiku na ikifika tena usiku anaenda kuweka ili kua tayali muda wote..kitu kingine wewe siyo mtu wa magari kiviiiiile kama madereva,ungeshaona tu
Nimeendesha gari kwa miaka kadhaa sasa lakini sijawahi kubahatika kukutana na gari la wagonjwa likiwa sheli, ni mimi tu au kuna aliyewahi kuona Ambulance ikiwa sheli?
 
mwingine akauliza eti umewahi kuona paka wakipigana mzigo?
Ukawajibu vipi?
FB_IMG_1570910823758.jpeg
 
Nishaona.Yanaenda sema kwakuwa sio nyingi ndio inaonekana kama ni nadra.
 
Back
Top Bottom