Je, ulishawahi kuaibika katika mazingira mabaya?

Daby

JF-Expert Member
Oct 26, 2014
33,648
75,729
Sometimes huwa tunafanya mambo kimazoea na kujitia ujuaji mwingi.
Najua mwana JF kuna siku uliaibika Aidha kwa ushamba ulionao, kujitia mjuaji ama kutokuwa na ufahamu juu ya Mambo fulani fulani.

Mimi: kipindi cha nyuma tulienda hotel moja kuogelea/swimming. Tulikuwa mobb ya watu kama 12(ke&me). Sasa kiubaridi cha saa 12 kikanipiga nikasema isiwe kesi ngoja nibugie hata tuvikombe tuwil twa kahawa nipunguze baridi. Washkaji waka ni alert ila nikasema liwalo na liwe walet ina 15000tsh bhana! haiwezi kuzidi hapo. Nikaitisha kahawa yangu... ile namalizia mhudumu/mama anakuja kukusanya vyombo vyake na sukari yake nyeupe( maana niliibakiza) nikapewa bill ya tsh 22500 . sheee tabala roi. Mimi nilijua mbalauni kama kwa mama clareee kumbe nauli ya chuga- moro kbs???

Na mmaza wa watu anataka kuondoka na pesa yake. Ikabidi washkji wajichange kimya kimya 6500 ikapatikana. Ila nilikiona cha moto kutembea kwa miguu kutoka hapo mpaka nyumbani. Na Nashukuru mamy siku hiyo sikuongozana naye.

Msinicheke wengi yametukuta. Je na wewe yalikukuta yapi???
 
Form 4 hyooo.mwana kaniambia twende tukamsalimie maza ake kariakoo.tukaenda.kivumbi ilikuwa mlangoni.kuvua viatu sitaki.maana vinanuka balaa.yaani sijavua lakini harufu naisikia.nikaingia navyo sebuleni kiubishi ubishi.bahati nzuri kulikuwa na tiles tu.ila shuhuli waliipata.
 
Kesi ngoja nibugie hata tuvikombe tuwil twa kahawa nipunguze baridi. Washkaji waka ni alert ila nikasema liwalo na liwe walet ina 15000tsh bhana! haiwezi kuzidi hapo. Nikaitisha kahawa yangu... ile namalizia mhudumu/mama anakuja kukusanya vyombo vyake na sukari yake nyeupe( maana niliibakiza) nikapewa bill ya tsh 22500

Chai zingine bana dah!

Mi hii imenishinda kunywa, nirudishie chenji mkuu.
 
Sitasahau for rest of my life ,nikiwa std 1 Mwananyamala Primary tulikuwa tunagombania namba bila kutegemea kifungo cha Pensi kikakatika na kwa kamwili kautoto pensi ikashuka chini nzima nzima watoto wakashangilia! Ikawa end of the day nikatimua home sikurudi mpaka zilipopita 5 days!
 
Form 4 hyooo.mwana kaniambia twende tukamsalimie maza ake kariakoo.tukaenda.kivumbi ilikuwa mlangoni.kuvua viatu sitaki.maana vinanuka balaa.yaani sijavua lakini harufu naisikia.nikaingia navyo sebuleni kiubishi ubishi.bahati nzuri kulikuwa na tiles tu.ila shuhuli waliipata.
Hahaha...lakini now umebadilika mkuu! !! Au unalisongesha bado
 
kuna binti aliagiza mabia bar kwa kunikomoa .sasa mfukoni nikawa na buku ten tu bill ikaletwa kama 35 elfu.enzi hizo ni ela mingi. nikavizia kaenda toilet nichukue handbag yake nichomoe ela tushare pamoja bill.akanifuma naingiza mkono kwenye mkoba.nilipata aibu ya mwaka.nafwaaa
Pole mkuu. Ungedanganya kuna vitu vilidondoka ulikuwa unaviwahi
 
Back
Top Bottom