Je, ulishawahi fika kwenye Interview ukaghairi kufanya?

wa zion

JF-Expert Member
Mar 23, 2013
222
476
Nitaanza kwa kushare my own experience, miezi kadhaa iliyopita niliitwa kwenye shirika moja kubwa sana hapa Tanzania kwa ajili ya kufanyiwa usahili wa nafasi fulani waliyoitangaza, kwa kutokujua nikafanya maandalizi ya kutosha ili siku ikifika nikapambane.

Bahati nzuri mmoja wa wafanyakazi wenzangu niliofanya nao kazi hapo awali alitokea kwenye hii taasisi tulifanya nae kazi kwa muda na akaitwa kurudi kwenye hili shirika alipotokea, kwa furaha nikampigia simu kumuambia nimechaguliwa kufanya interview kwenye shirika lao, Jibu nililokutana nalo sikuamini masikio yangu " omba Mungu hizo ni formalities tu maana tayari kuna mtu wa ndani "

Nilikosa nguvu lakini nikajipa moyo kwamba acha niende nitapambana hata kama wana mtu wao, siku ikafika mapema nikafika eneo la tukio ndani ya dakika chache nikapelekwa chumba cha kufanya mtihani wa kuandika jamani ule ulikua sio mtihani bali kukomoana waliweka kabisa kwamba kila swali hakikisha unajibu kwa 2 page, maswali yalikua matatu kila swali moja lilikua lina page mbili hadi tatu za kusoma tu swali na kuna kipengele A na B ukiangalia uwe umeandika(type kwenye laptop) almost 12 pages ndani ya saa moja. kwa kweli nilikaa mule ndani kama 20 minutes nikitafakari nakanyanyuka nikamuita HR wao nikamwambia nimeahirisha kufanya akaniambia fanya basi hata oral interview nikagoma maana bado nilikua msindikizaji tu wa yule walienae.

Je, yalishakukuta? ulifanyaje?
 
Pole sana mkuu,hapo ndipo akili ya ujasiriamali inapozaliwa.Kwa nini usifungue magenge yako kumi ukawa unayasimamia?
 
Jana nilikuwa na interview wilaya ya kongwa nafasi ni 7 wameita watu 600+ nikapiga garama za kwenda na kurudi ni kam laki.
Nilichofanya nimenunua mitetea 10 ya elfu 8 na pumba za mayai kwanzia next week nianze vuta mpunga
ha ha ha ha
 
Nilipangwa interview na rafiki angu alienipita kila kitu (sema miezi ya interview ilikua tofauti)

Tukiwa chuo alikua konki kiakili mpk matokeo (upper class za maana),

wazazi wake pesa ilikuepo tena si ktoto

Ukifanya interview leo (in two days mnapokea email) usipopata mail yoyote ujue Hujapita

Alianza yeye akaenda akafanya (baada ya siku mbiili kimyaaa)

Ki ukweli mimi sikujisumbua kwenda tena maana niliona ni kwenda kujichoresha tu
 
Nilipangwa interview na rafiki angu alienipita kila kitu (sema miezi ya interview ilikua tofauti)

Tukiwa chuo alikua konki kiakili mpk matokeo (upper class za maana),

wazazi wake pesa ilikuepo tena si ktoto

Ukifanya interview leo (in two days mnapokea email) usipopata mail yoyote ujue Hujapita

Alianza yeye akaenda akafanya (baada ya siku mbiili kimyaaa)

Ki ukweli mimi sikujisumbua kwenda tena maana niliona ni kwenda kujichoresha tu
hahahah wewe jamaa pimbi kweli
 
Jana nilikuwa na interview wilaya ya kongwa nafasi ni 7 wameita watu 600+ nikapiga garama za kwenda na kurudi ni kam laki.
Nilichofanya nimenunua mitetea 10 ya elfu 8 na pumba za mayai kwanzia next week nianze vuta mpunga
Kazi gani hiyo mkuu ilikuwa na watu wengi hivyo?
 
Nilienda kwenye interview moja, nafasi zinazohitajika 10 interviewer 2000. Nikajisemea tu kimoyomoyo hapa hamana kitu. Kabla hata ya kuingia kwenye written interview Nikajiondokea mdogo mdogo.
 
Niliienda kwenye interview moja kulikuwa kuna nafasi 7 waliita watu mia mbili, tukaingia kwenye kuandika, wakachuja ,tukabaki hamsini, tukaenda kwenye vitendo, sasa cha ajabu kuna watu pale walikuwa wanajitolea na wenyewe walikuwa pamoja na sisi, nikasikia wanaambizana ,hawa wanapoteza mda wao tu,hizi nafasi zina watu mda mrefu.

Nilikaa nikajiuliza, hapa nakula hoteli na nalala gest, hii gharama ya nini yote, nafasi 7 na watu wapo walikuwa wanajitolea na sisi wageni tumebaki 43 ,huyu mwenyeji walie kaa nae siku zote akijitolea kwa uchungu wote wamuache wanichukue mimi ambaye ndo kwanza wananiona leo, nitakuwa na upepo gani??!, Sikukaa sawa bwana mmoja akanifata kama utani akaniambia hii interview ni kutimiza wajibu tu, nafasi walishakaba watu kitambo, niliangaria hali nikaona utoboaji si mrahisi. Nikarudi gect kuchukua vyangu na baada ya mda nikafatilia nikaambiwa waliokuwa wanajitolea walipewa kipaumbele chapo watu wote walikuwa na sifa.
 
Sasa mkubwa hebu tuwekane sawa hapa, kilichotokea hapa ni kughairi kufanya interview au interview ilikuona, I mean pepa ilikuwa ngumu? Kilichofanya ughairi na kuondoka ni ile hali kuambiwa wana mtu wao au ugumu wa maswali?
 
Niliwahi kuitwa interview bodi ya kahawa moshi, nikapiga hesabu zangu za gharama, idadi ya watu wanaohiajika na idadi ya watu tulioitwa nikaona hapa napoteza muda nikapotezea.

Ya pili interview utumishi, asubuhi kufika nimekuta watu kibao, katika harakati za kujiandaa ikaingia email nikareport kazini mkoani. Nikabeba vyeti vyangu huyo nikawahi gheto kwenda kujiandaa na safari.
 
Back
Top Bottom