Je, ulimi ungekuwa na mfupa watu wasingekosea kutamka?

Oct 14, 2011
49
44
Wadau Habari za jumapili,

Kwa miaka mingi sana huu msemo "Ulimi hauna mfupa" umekuwa ukitumika hususani pale mtu anapoteleza kuzungumza jambo, nimekuwa nikijiuliza aliyetunga msemo huu alikuwa anakusudia nini na endapo ulimi ungekuwa na mfupa; je, watu wasingekosea matamshi?

Wataalamu mnaweza kusaidia hili ili pia iwe fundisho kwa vizazi vijavyo.

Shukrani
 
Ebu tuangalia kwanza viungo vya mwili vilivyo na mifupa je vinafanya sahihi au? Je, havikosei? Mfano Miguu, Mikono?
 
Ebu tuangalia kwanza viungo vya mwili vilivyo na mifupa je vinafanya sahihi au ? Je havikosei? Mfano Miguu, Mikono?
Swali la msingi sana, uwa vinakosea wakati mwengine, swali la kujiuliza imekuwaje kutumia kigezo cha ulimi kutokuwa na mfupa kuwa ndio sababu ya sisi kukosea matamshi?
 
Alikuwa hajajua (bado) kama kinachoamua unachoongea ni Ubongo na siyo Ulimi!
 
Maanake ulimi ni mwepesi utenda mambo kwa wepesi kuliko viungo vye mifupa ni vizito kitendaji ndo maana uta ambiwa Ulimi umeteleza coz ni mwepesi
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom