Je, ulianza ujenzi ukiwa katika hali gani kiuchumi/ kipato?

Dah huu uzi. Ndio niko hapa nataka nianze msingi wiki hii. Kila nikiwaza hela haitoshi hata robo ya makadirio. Fundi anapiga simu kila siku kuuliza "boss tunaanza lini...". Namwambia tulia nimetingwa na kazi ntakucheck. Hajui boss mwenyewe nimepalala. Sema one day...
 
ramani tayari?
 
Naombeni ushauri Jamani napokea 740k take home Nina mwaka mmoja kazini mpaka Sasa nimepanga nimefanikiwa kununua vitu vya ndani tu TV, godoro ,kitanda na n.k na vile vile nilikua nimeanza ujenzi kumjengea bi.mkubwa nyumba yake nimeshapaua

Sasa napata hamasa Sana kuona mwaka unaisha Sina hata kiwanja na akiba yoyote benki naombeni ushauri nataka nipumzike kumalizia nyumba ya mama. Nijikusanye nitafute kiwanja nianze kujenga yakwangu siko comfortable kwenye nyumba za kupanga

Matumizi yangu baada ya kupata mshahara;: Niko dar!

1. Usafiri kwa mwezi 50,000
2. Kula kazini mwezi mzima: 150,000
3. Nyumbani: jioni na weekend: 100,000
4. Kwaajiri ya ujenzi wa nyumbani natuma Laki3 kila mwezi

Kodi kwa Mwezi laki 1 nalipa kwa miezi 6

Napokea hela nzuri kibongobongo! Hata hata inavyoisha sijui!

Naombeni ushauri

740k ni hela nzuri? Au sijaelewa
 
Laki7 sio mshahara mzuri ni average mno. Ila kwa hesabu hizo unajitahidi mno. Hapo kazi ni kusave mpk upate hela ya kiwanja cha kueleweka ndio kimbembe ila kujenga utajenga tu na itaisha. Zichange karata vizuri.

Ndogo Sana tu mbona....kibongobongo hazitoshi
 
Back
Top Bottom