Je Ukizaa Mtoto Wa Jinsia Mbili Utafanyaje? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Je Ukizaa Mtoto Wa Jinsia Mbili Utafanyaje?

Discussion in 'JF Doctor' started by Ab-Titchaz, Nov 9, 2008.

 1. Ab-Titchaz

  Ab-Titchaz Content Manager Staff Member

  #1
  Nov 9, 2008
  Joined: Jan 30, 2008
  Messages: 14,702
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 135
  Mama akataa kuua mtoto wake mwenye jinsia mbili


  *Familia yadai auawe kwa kuwa ni mkosi

  *Ampeleka kwa mama yake kulinda ndoa yake

  Na Mwandishi Wetu

  MKAZI mmoja wa Kijiji cha Matare Kata ya Mugumu mjini, wilayani Serengeti, Anna Samson [22] anakabiliwa na wakati mgumu katika ndoa yake, baada ya kukataa kumuua mtoto wake aliyezaliwa na sehemu mbili za kiume na kike kwa madai kuwa ni mkosi kwa mila za kabila la Wakurya.

  Uamuzi huo wa kikatili unadaiwa kutolewa na mume wa mwanamke kwa kushirikiana na mama yake mzazi, mara baada ya kuzaliwa kwa mtoto wao Baraka Marwa mwenye umri wa miaka miwili sasa. Mtoto huyo alizaliwa katika Hospitali ya Wilaya ya Nyerere akiwa na jinsia mbili ya kike na ya kiume.

  Akizungumza na Mwananchi Jumapili kwa huzuni kubwa, Anna alisema kuwa matatizo hayo yalianzia hospitalini mara baada ya kujifungua na kwamba mume wake kwa kushirikiana na mama mkwe wake, waliamua mtoto huyo auawe kwa madai kuwa ni mkosi kwa familia hiyo na kuwa hatakiwi kukanyaga katika nyumba yao.

  "Kwa kweli iliniwia vigumu kutekeleza uamzi huo wa kuua mtoto wangu kutokana na maumbile hayo,nilikataa na kuzuiwa kufika nyumbani kwangu kwa kuwa ni mkosi mkubwa kuwa na mtoto wa namna hiyo kwa mujibu wa mila na desturi za Kikurya,” alisema huku akibubujikwa machozi.

  "Niliamua kwenda nyumbani kwa wazazi wangu na kuwaeleza hali halisi ambako mama yangu alikubali kukaa na mtoto huyo, baada ya kumwachisha kunyonya ili niweze kurudi kwenye ndoa yangu ambako pia nina mtoto mwenye umri wa miaka minne,"alisema.

  Alisema walikuwa wakiendelea kumpeleka hospitali kwa ajili ya matatizo yake, kwa kuwa wakati wa kukojoa anapata taabu sana kiasi cha kumvuta kwa mpira, ndipo wakafikia hatua ya kumtahili sehemu ya kiume kwa kuwa ndiyo iliyoonekana kufanya kazi kuliko ya kike.

  "Pamoja na kumtahiri bado akinywa chai au vitu vya majimaji hupata shida kukojoa, nimempeleka Hospitali ya Bugando mjini Mwanza, mara mbili na wamesema watamfanyia upasuaji, nimepangiwa nirudi tena mwishoni mwa mwezi huu, tatizo ni kwamba sina fedha kwa kuwa mume wangu hayuko tayari kutoa fedha kwa ajili ya kazi hiyo,” alisema na kuongezea; "Katika upasuaji unategemewa kufanywa kuondoa sehemu ya kike na kubakiza ya kiume kwa kuwa ndiyo imeonekana kufanya kazi,"alisema Anna.

  Alisema mtoto huyo kwa sasa yuko kwa mama yake Matare alikomuacha huku yeye akiwa ameamua kurejea kwa mume wake ambako baada ya kurejea bila ya mtoto huyo alipokelewa bila shida yoyote.

  Aliomba watu wenye uwezo na mashirika mbalimbali, wamsaidie ili aweze kufanikisha matibabu ya mtoto huyo na kunusuru ndoa yake iliyoko majaribuni kwa kuwa hakuna amani ndani ya ndoa baada ya kukataa kumuua mtoto Bahati.

  Uchunguzi wa Mwananchi Jumapili umebaini bado baadhi ya jamii wanaendekeza mila ambazo zinakiuka haki za binadamu na kibaya zaidi ni kwamba mila hizo zinatekelezwa na vijana wadogo ambao wanatakiwa kuleta mageuzi katika jamii.

  Akizungumza na Mwananchi Jumapili Mratibu wa Wasaidizi wa Kisheria na Haki za Binadamu Wilaya ya Tarime, Bony Mato kuhusiana na tukio hilo alisema mila kama hizo zinatakiwa kufanyiwa marekebisho kwa kuwa zinakiuka haki za binadamu ambazo mtu anazaliwa nazo.

  "Nilistushwa sana na uamzi huo baada ya kuambiwa na Anna yaliyomkuta kwa kweli inasikitisha sana kuona watu wa karne hii bado wanaendekeza mambo kama hayo, niliamua kumtuma kuja ofisini kwako kwa msaada zaidi,"alisema

  Mwananchi Read News
   
 2. Mshiiri

  Mshiiri JF-Expert Member

  #2
  Nov 9, 2008
  Joined: Jun 16, 2008
  Messages: 1,893
  Likes Received: 66
  Trophy Points: 145
  Ni surgery tu kuondoa ile jinsia iso active. Au mnasemaje? Tatizo hapa ni fedha. That is according to me.
   
 3. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #3
  Nov 9, 2008
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  Mama huyu alifanya jambo jema kumnusuru mwanaye na kifo.
  Mzazi yeyote angependa kupata watoto wasiokuwa na kasoro za kimaumbile.Inapotekea kinyume na matarajio basi huo ni mtihani na inahitaji busara na subira kupata ufumbuzi.Njia moja wapo ni kupata msaada wa kitabibu kama alivyofanya huyu mama lakini maranyingi msaada huo haupatikani kirahisi kwa vile labda kuna gharama kubwa au utaalam haba.Pia imani potofu huchangia katika kutafuta suluhishao rahisi na pengine lenye madhara.Alivyofanya huyu mama japo ni jambo jema, sidhani amepata suluhisho.Mtoto huyu kukaa na mama wa mwanamke inaweza kuchelewesha huduma za kitabibu, kama angebaki na mwanawe ingekuwa rahisi yeye mwenyewe kufuatilia kwa ukaribu zaidi maana uchungu wa mwana aujuaye ni mzazi.
  Hapa kuna suala lingine linajitokeza kwa wanawake.... hivi ni kipi muhimu kujali maslahi ya mwanao kwanza au ndoa?
   
 4. Tonga

  Tonga Senior Member

  #4
  Nov 10, 2008
  Joined: Jul 8, 2008
  Messages: 175
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Nakuelewa katika hili, ila swali lako hapo chini limenifanya nifikirie sana ni swali zuri ila sio rahisi sana kulijibu ukizingatia mila zetu za kiafrika ambazo mwanamke ndio mhimili wa ndoa japokuwa mara nyingi hana sauti katika maamuzi muhimu yaihusuyo ndoa hiyo (is too sad). Kwa mimi binafsi mtoto hasa mwenye matatizo ya kiafya kama huyu ndio kipaumbele katika familia regardless baba yake anasema nini; ila kama nilivyosema hapo mwanzo inategemea huyo mwanamke ana sauti kiasi gani katika hiyo ndoa.
  Namtakia Bi Anna kila la kheri katika hili, ni jambo zito na gumu katika familia pia linahitaji busara,uvumilivu na ujasiri wa hali ya juu. Huyu ni mwanamke shujaa sana kuamua kulitekeleza hili bila ridhaa ya mumewe; Mungu atakupigania katika kulifanikisha jambo hili umeokoa roho ya malaika asiye na hatia.
   
 5. H

  Hofstede JF-Expert Member

  #5
  Nov 10, 2008
  Joined: Jul 15, 2007
  Messages: 3,584
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 0
  Utajuaje jinsia isiyo active na wakati huyu ni mtoto?, Kuna mtoto wa hivyo alizaliwa morogoro akaachwa na jinsia zote mbili ila kwa wakati ule walidhania kuwa ya kike ni active wakampa jina la kike, alipokuja kubarehe ya kiume ndiyo ikaanza kucharge na hivi sasa ana mke na watoto watatu, baada ya kumpatia mimba mwanafunzi wake na kuamliwa amuoe ndiyo watu wakajua kuwa kumbe bibie ni kidume?.
   
 6. Kang

  Kang JF-Expert Member

  #6
  Nov 10, 2008
  Joined: Jun 24, 2008
  Messages: 5,123
  Likes Received: 618
  Trophy Points: 280
  Nchi ina mambo ya ajabu sana, yaani mtu anasugest mtoto auliwe freely kabissa??
   
 7. Y

  Yassin JF-Expert Member

  #7
  Nov 11, 2008
  Joined: Jul 23, 2008
  Messages: 326
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Sasa wewe uliyeanzisha hii mada kama ni mwanamke je wewe unaweza kukubali mtoto wako auliwe???Jibu kwanza hili swali
   
 8. Kilbark

  Kilbark JF-Expert Member

  #8
  Nov 11, 2008
  Joined: Feb 25, 2008
  Messages: 558
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Unajua miaka ya hivi karibuni mimi nasikia haya matukio. Na ni ngumu sana katika miaka ya zamani kasikia hivi vitu kwa sababu kama hizo. Nakumbuka hata muungwana katika hotuba yake ya Maalbino alisema kitu kama hicho kuwa huko kwao enzi hizo akizaliwa Albino wakunga wa jadi walikuwa hawana discussion ni kuua tu. Umeshawahi kumuona mmasai Albino? Utamaduni na mambo ya mila za jadi vinachangia sana hii hali. Sayansi na Teknolojia imewawezesha watu kujua haki zao za kuishi lakini bado kuna mila na tamaduni wati wanazienzi hawaziachi japokuwa wamesoma they call it CALVINISM. Kwa nini mchaga bado anakwenda kwao wakati wa Krismas au watu wengine wana msemo wa kwenda kusafisha makaburi? Mila bado zinaenziwa. Sasa inawezekana jamaa kweli alishauriwa na akaamini ni mkosi kwa sababu ya imani zake za kimila.
   
Loading...