Je ukitaka kurudi nyumbani kwa mkeo/ mchumba wako huwa unampa APPOINTMENT

Raymanu KE

JF-Expert Member
Jan 20, 2022
6,730
12,429
Habari zenu wanamjavi? Natumai mpo salama na mnaelendea vyema na shughuli zenu.Leo naomba tuongelee hili saula la kurudi nyumbani kwa mpenzi wako ukitoka kazini.Hii thread ipo applicable Sana kwa wanaume maana wao ndo wahanga wakubwa wa hili suala.Ila wanawake pia mnaruhusiwa kuchangia hoja zenu.

Katika ndoa nyingi za siku hizi utakuta mtu na mkewe hawaishi sehemu Moja kwa sababu ya kikazi.Tuseme mume anafanya kazi mjini na mkewe Yuko vijijini.Kwahyo mume atakuwa anakuja vijijini kuitembelea familia yake Mara Moja Moja tuseme labda Mara tatu kwa mwaka.

Sasa ishu kuu ipo hapo kwenye "mume kumtembelea mkewe/ mchumba wake huko vijijini" aidha kwa kutoa appointment ama kwa kushtukiza tu bila kumpa taarifa yoyote.Hili la kushtukiza watu wengi huwa hawalipendi maana huenda anayekuja nyumbani akakuta mambo Ni tofauti kbsa na jinsi alivyotarajia.

Yuko rafiki yangu mmoja aliamua kumtembelea mkewe kijijini impromptly kbsa yaan bila kumpa taarifa zozote kwa sababu alijua anaenda nyumbani kwake kwahyo hakuwa na haja ya kumtaarifu mkewe.Jamaa alifika kwake saa tano usiku ila Cha ajabu akamkuta mkewe Yuko na mwanaume mwingine chumbani kwao.Jamaa akaamua kumpa talaka mkewe.

Kwa utafiti niliofanya Mimi,nimegundua kwamba Kati ya ndoa 10 nne huvunjika kwa sababu ya hizi " impromptu visits".Yaani mtu anaenda kwake akijua atakuta Kila kitu kipo sawa kumbe Ni vice versa.Anakuta nyumba Ni chafu,vyombo vichafu,mke mwenyewe amevaa mavazi ya ajabu ajabu,au labda hayupo nyumbani na amewaacha watoto bila chakula au yupo na mwanaume mwingine.Mambo Kama hayo huleta mfarakano kwenye ndoa za watu na kupelekea talaka.

Mimi binafsi siwezi kwenda nyumbani kwa mke wangu bila ya kumpa taarifa maana Hawa Wanawake Ni viumbe wa ajabu Sana na imeandikwa tuishi nao kwa AKILI.

Je,wewe unaweza kumtembelea mume/ mke/ mchumba wako without an Appointment?
Nawasilisha.
 
nitoe taarifa kuwa naenda kwangu, mi siyo taahira aisee. hiyo sifannyi
tena hata akiniuliza unakuja namwambia siji, anashtukia tu nipo getini
 
Wazee wetu enzi zao hawakuwa wajinga hata wakitoka tu kazini, walikuwa wanapiga kelele jirani au kumpatia Mtoto mdogo zawadi atangulize kwao.

Wakati mwingine unaweza kujiepusha kununua gunia mbili za mkaa maana huwezijua kipi kinachoendeleaga nyumbani kwako wakati ukiwa haupo na Mkeo.
 
Ewaa...mzee yuko nje huko anaanza kuimba imba zake ili kama kuna zari huko ndani mlirekebishe mapema yani,
 
Hahahahah kwahio uanze kumuomba ridhaa ya mkeo kwenda kwako? Maana kwa vyovyote pale ulipompangishia lazima patakuwa panamuhusu kwa namna moja au nyengine
Kuomba ridhaa? Hiyo ni lowest level ya ujinga.
Mimi kwangu huwa nakuja anytime nataka.

Kwako halafu bado upangiwe?
 
Jamani toeni taarifa.Hakuna surprise Africa.Utajisuprise yourself
Kama kweli bado unampenda mkeo lazima umtaarifu ujio wako ili ajiandae, ila unapomchoka na kumtafutia sababu ya kumuacha ndio unamfanyia surprise.
 
Natoaga taarifa kama narud na mgeni incase kama hakupika afanye mambo mapema nje na hapo narud mda naotaka. Nyumba yangu na bado nitoe taarifa never
 
Mimi huwa natoa taarifa kwamba nakuja kwa sababu najua haya mambo ma3 yatafanyika
1. Namuandaa kisaikolojia kwamba ninarudi na ugwadu hivyo awe tayari kwa match.

2. Ataniandalia misosi mitamu, ikiwa ni pamoja na kuadjust ratiba zake na za wanafamilia ili nipate muda wa kujiachia.

3. Kwa mazingira ya nyumbani hawezi kuleta mtu, labda aende kwa hoteli au huko kwa jamaa. Na kwa vile ni ngumu kumkamatia huko, ni heri nimpe taarifa kama nakuja ili kama alikuwa na mpango wa kando aupange upya. Trust me, kinachouma sio kugongewa, unaumia ukijua umegongewa. Jitahidi usijue kama unagongewa
 
kama ni mkeo hakuna haja uhuni ni hulka ya mtu tu hata asipowaleta home watakutana huko vichocholoni,ila kama ni gf toa taarifa ova
 
kuna wanaume kama wamelogwa vile na wanawake zao sasa mtu hata kwenda kwako mpaka utoe taarifa?

au unakuta mtu eti anakwambia usishike sim ya mwenzio utakufa na presha huo ni ujinga
 
Mimi huwa natoa taarifa kwamba nakuja kwa sababu najua haya mambo ma3 yatafanyika
1. Namuandaa kisaikolojia kwamba ninarudi na ugwadu hivyo awe tayari kwa match.

2. Ataniandalia misosi mitamu, ikiwa ni pamoja na kuadjust ratiba zake na za wanafamilia ili nipate muda wa kujiachia.

3. Kwa mazingira ya nyumbani hawezi kuleta mtu, labda aende kwa hoteli au huko kwa jamaa. Na kwa vile ni ngumu kumkamatia huko, ni heri nimpe taarifa kama nakuja ili kama alikuwa na mpango wa kando aupange upya. Trust me, kinachouma sio kugongewa, unaumia ukijua umegongewa. Jitahidi usijue kama unagongewa
Kufumba macho ili usione wakati unajua kinachoendelea ni ujinga
 
Back
Top Bottom