Je, ukistaajabu ya Spika Ndugai na Utanganyika utayaona ya Rais Samia na Uzanzibar?

seedfarm

JF-Expert Member
Feb 9, 2020
260
2,654
Hakuna kauli ya bahati mbaya au jambo la bahati mbaya, Haya yote humtoka mtu moyoni kwani ndio moyo wake umeyajaa yamtokayo

Refer:Uzi wa Pascal Mayalla Unaoongelea Powers of karma na Nguvu za uvutano( Newton's laws of Motion)

Kauli ya Spika Job Ndugai kuwa pesa za korona za msaada wa IMF zigawanywe kwa kufuata idadi ya watu na sio majimbo ilikuwa inailenga Zanzibar na kutaka kuisaidia Tanganyika wengi wanaiita Tanzania bara

Zanzibar ina idadi ndogo sana ya watu hawafiki hata laki sita lakini wana majimbo zaidi ya 20,Ukigawa pesa za korona kwa kufuata majimbo Zanzibar watapata pesa nyingi sana kuliko majimbo ya bara yenye idadi kubwa ya watu

Takribani nusu ya watu wa Zanzibar yaani zaidi ya watu laki tano wanaishi Tanzania bara(Tanganyika) wakijishughulisha na shughuli mbalimbali za Kilimo na biashara , Hivyo wakazi waliopo Zanzibar kama Zanzibar hawazidi laki sita

Je Ndugai sasa somo la katiba mpya linaanza kumuingia kwani kwa miaka mingi Bungeni pesa ziligawanywa kwa kufuata majimbo na Yeye alishiriki kama Spika kupitisha

Kauli ya Rais Samia kuwa Yeye ni mzanzibar ilikuwa ni kutuma ujumbe kwa wale wanaoona sasa anaipendelea Zanzibar kwa kulazimisha kila kitu kinachofanyika bara kifanyike Zanzibar huku watu wa Tanganyika wakitambua Zanzibar ina idadi ndogo ya watu sana


Jimbo la kawe Dar es Salaam lina watu zaidi ya Zanzibar

Jimbo la Mbeya mjini ambalo Spika Ndugai alilitolea mfano lina watu zaidi ya Zanzibar, Jimbo la Mbeya mjini lina watu zaidi ya Milioni moja huku Zanzibar watu hawafiki laki sita

Pesa za msaada wa korona za IMF zikigawanywa kwa kufuata majimbo basi zitasaidia Zanzibar zaidi kuliko Tanganyika,

Pesa za msaada wa korona za IMF zikigawanywa kwa kufuata idadi ya watu wa eneo husika basi zitasaidia zaidi hata kwenye Jimbo la Kongwa la Ndugai

Mtifuano huu wa kauli kuna siku kila mtu atadai nchi yake, Tayari watu walishaanza kuona hali ya upendeleo inaanza kutamalaki kati ya Zanzibar na Tanganyika

Rais Samia amethibitisha kwa kauli yake kuwa Katika teuzi wanaotumbuliwa wanalalamika kuwa ukabila unatumika huku suala la udini Rais Samia akilificha na kutotaka kuliongelea ambayo ndio msingi mkuu wa malalamiko ya watu kwa sasa

Muda ni wakati na Muda ni mwalimu, kuna siku suala la katiba mpya na la kupunguza mamlaka ya Rais litaanzishwa na wana ccm wenyewe Bungeni akiwepo Spika Job Ndugai

=====

Screenshot_20211012-003759.png
 
Sii hasa siku zote ni matatizo au mafanikio katika Dunia hii , inategemea tu jinsi ilivyotumika.
 
Hii zanzibar mliiendekeza wenyewe, chukulia mfano wa hongkong ambapo kuna kiongozi mkuu (chief executive).....huwezi kusikia watu wa jimbo la hongkong wakidai haki sawa na watu wa mainland China linapokuja swala la uongozi na kugawana rasilimali, kwani hongkong pamoja na kuwa semi-autonomous bado ni sehemu ndogo sana ya china. Sasa nyinyi endeleeni kuendekeza huu uzwazwa eti mnalinda muungano......
 
Back
Top Bottom