Je, ukishikiliwa Kituo cha Polisi unaweza kupata dhamana?

Status
Not open for further replies.

JamiiTalks

JF Advocacy Team
Aug 7, 2018
625
938
Nini maana ya hakimiliki.png

Inategemea umekamatwa kwa kosa gani, kwa mfano ukikamatwa kwa makosa ya mauaji, Uhaini, makosa ya kutakatisha pesa, kunajisi, wizi wa kutumia silaha kufanya biashara ya madawa ya kulevya au ugaidi miongoni mwa makosa mengine huwezi kupata dhamana.

Ikiwa umekamatwa kwa tuhuma za makosa mengine ni lazima Polisi wakujulishe kuwa unayo haki ya kupata dhamana kwa mujibu wa sheria.

Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai inasema kuwa unayo haki ya kupata dhamana ya Polisi kwa kuzingatia vigezo vifuatavyo:-

• Ukubali kwa maandishi kufika katika Kituo cha Polisi, siku, tarehe na muda utakapohitajika;
• Ukubali kwa maandishi kuzingatia masharti yatakayotajwa katika hati ya dhamana;
• Mtu mwingine anayekubalika na Polisi akiri kwa maandishi kwamba anakufahamu na ana ahidi kukuleta wewe mtuhumiwa katika Kituo cha Polisi au kuhakikisha kuwa unafika Mahakamani tarehe na muda wowote atakapohitajika; na
• Wewe au mtu mwingine anayekubalika na Polisi, anaweka ahadi ya maandishi ya kulipa kiasi fulani cha fedha kama dhamana iwapo utashindwa kufika katika Kituo cha Polisi wakati utakapohitajika.

Vilevile, Askari Polisi msimamizi wa kituo cha Polisi anaweza pia kukuachia kwa dhamana kama:-

• Ulikamatwa bila kibali; na baada ya uchunguzi wa kina, kwa maoni yake, anaona kuwa hakuna ushahidi unaojitosheleza kuendelea na mashitaka;
• Kosa unaloshitakiwa kwalo siyo kosa kubwa; au
• Inaonekana kwamba uchunguzi zaidi utatakiwa kufanywa na hauwezi kukamilika ndani ya muda mfupi. Hata hivyo, polisi wanaweza kukunyima dhamana endapo mtuhumiwa aliwahi kufungwa kwa zaidi ya miaka mitatu au kama mtuhumiwa aliwahi kukiuka masharti ya dhamana.
 
Kanuni na taratibu hizi zikisimamiwa kwa weledi na kutekelezwa katika uhalisia wake , jamii itapona na mengi
 
Hizi haki zinafahamika,tatizo ukifikishwa polisi,kwa jinsi watakavyokuwa Wana ku intimidate,kwa maneno makali,matusi,unaingiwa na woga,polisi nao huwa wanaangalia mtu mwenyewe status yake,kule vijijini wananchi ni waoga na polisi ni kama miungu watu,
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom