Je ujumbe aliokuwa nao lipumba uliwafikia walengwa.

Byendangwero

JF-Expert Member
Oct 24, 2010
871
56
Baada ya kutangazwa kwa matokeo ya urais, Prof. Lipumba kwaniaba ya wagombea wenzake alipewa fursa ya kutoa neno; katika nasaha zake, alianza kwa kumpongeza JK kwa kutangazwa kuwa mshindi na akamalizia kwa kumkabidhi ilani ya uchaguzi ya chama chake. Kwa wadadisi wa mambo, kitenda cha kusema kuwa alikuwa anampongeza rais mteule kwa kutangazwa kuwa mshindi, na wala siyo kwa kuchaguliwa kuwa rais, kilikuwa kinarejelea ujumbe ule ule uliotolewa na Maalim Seif huko Zenj, wakati aliposema ya kuwa, kati yake na Shein apakuwepo mshindi. Kwa maneno mengine, viongozi wote wawili wa CUF walikuwa wanatoa ujumbe ya kwamba ushindi iliupata CCM katika chaguzi zote mbili ulikuwa ni wa mezani na wala siyo wa wapiga kura, na hivyo chama hicho hakina uhalali wowote wa kwenda kifua mbele.
 
Kwa jinsi nilivyovhukia hypocrisy ya Lipumba, naona kama ni mwanasiasa goigoi

sorry about that
 
Baada ya kutangazwa kwa matokeo ya urais, Prof. Lipumba kwaniaba ya wagombea wenzake alipewa fursa ya kutoa neno; katika nasaha zake, alianza kwa kumpongeza JK kwa kutangazwa kuwa mshindi na akamalizia kwa kumkabidhi ilani ya uchaguzi ya chama chake. Kwa wadadisi wa mambo, kitenda cha kusema kuwa alikuwa anampongeza rais mteule kwa kutangazwa kuwa mshindi, na wala siyo kwa kuchaguliwa kuwa rais, kilikuwa kinarejelea ujumbe ule ule uliotolewa na Maalim Seif huko Zenj, wakati aliposema ya kuwa, kati yake na Shein apakuwepo mshindi. Kwa maneno mengine, viongozi wote wawili wa CUF walikuwa wanatoa ujumbe ya kwamba ushindi iliupata CCM katika chaguzi zote mbili ulikuwa ni wa mezani na wala siyo wa wapiga kura, na hivyo chama hicho hakina uhalali wowote wa kwenda kifua mbele.
Some truth!
Japokuwa kuna picha humu ndani ambapo jamaa kavaa full ccm!
 
Back
Top Bottom