Je, ujenzi holela mijini ni kipimo cha akili ya Mwafrika?

Manelezu

JF-Expert Member
Feb 6, 2015
1,510
2,000
Nimebaharika kufika baadhi ya miji mbalimbali duniani, ikiwamo baadhi ya miji africa na Tanzania karibu yote! Kitu nachoona ni tofauti kabisa na sisi, ni jinsi wenzetu wanavyothamini suala zima la makazi,
Ukiangalia makazi yetu hasa kwenye miji mikubwa kama vile Dar es salaam, Mwanza, Mbeya etc imejengwa hovyo na unajiuliza tu tatizo ni nini? Kwanini suala la makazi lisipewe kipaumbele na serikali? Naamini itasaidia sana hata kupunguza uharifu,.
Miji ya wenzetu kwakweli ni mizuri sana hata ukipiga picha tu upo mtaani unatokelezea. Naamini bado sisi ni nchi changa lakini suala la makazi naona binafsi lipewe kipaumbele kama standard gauge sababu hata huko mbele uchumi ukikuwa itakuwa tabu sana na gharama kubwa kulekebisha miji yetu!

Mh. Lukuvi naamini wewe ni ntu makini sana na una exposure kubwa, kwann nyumba zetu na ramani ya nyumba zetu zipo karibu sana na barabara? Hatuoni umuhimu wa kuwa na front yard and back yard? Kwanini ramani za nyumba zinabanana kiasi kwamba hamna space ya nyumba moja hadi nyingine? Why are our houses so close to the street roads or main roads? Hili nalo ni pesa au maamuzi? Sababu nchi hii haina tatizo la ardhi kwanini tubanane? Ebu serikali na wizara husika chukulieni suala la makazi na mipango miji very seriously! Muanze angalau na vibrant cities kama Dar es salaam, Mwanza, Dodoma, Mbeya etc,

May God bless our great country!!
 
mulwanaka

JF-Expert Member
Feb 19, 2017
3,965
2,000
"No political will" hawana utashi wa kisiasa bora wanunue ndege zitakazo wapa umarufu wa kisiasa kuliko hilo.....jiulize dodoma ni jiji tena mji mkuu kwanini hawaufanyi uwe na mpangilio wakima taifa why do we rush to call it a city wakati na mahitaji muhimu kama running water, sewage system underground power system modern rubish dumps....nk tunaharaka unafikiri tz inaisha baada ya miaka 10. Tunachekwa sanaa tukiona magorafa ya wahidi na waarabu Dar tunafikiri ndo maendeleo wakati hayana hata parking space emergence exits fire extigasher nk.
 
Adharusi

JF-Expert Member
Jan 22, 2012
13,891
2,000
Tena wasomi wanaongoza huku mjini kwa kujenga hovyo hovyo.. Nimepita vijijini wengi wanajenga kwa mpango, barabara, mtaa, vijijini Wana akili sana
 
mulwanaka

JF-Expert Member
Feb 19, 2017
3,965
2,000
"No political will" hawana utashi wa kisiasa bora wanunue ndege zitakazo wapa umarufu wa kisiasa kuliko hilo.....jiulize dodoma ni jiji tena mji mkuu kwanini hawaufanyi uwe na mpangilio wakima taifa why do we rush to call it a city wakati na mahitaji muhimu kama running water, sewage system underground power system modern rubish dumps modern bus terminal public transport and emergence roads....nk tunaharaka unafikiri tz inaisha baada ya miaka 10. Tunachekwa sanaa kamji kodogo kama Nowrch UK kame pangiliwa vizr kuliko dar na Mwz tukiona maghorafa ya wahidi na waarabu Dar, tunafikiri ndo maendeleo wakati hayana hata parking space, emergence exits, fire extigasher, njia za walemavu nk.
 
FUSO

JF-Expert Member
Nov 19, 2010
18,895
2,000
Siwezi kuendelea kupanga nyumba wakati familia inaongezeka na matumizi yanapanda, kodi juu kila kukicha. Ardhi imejaa tele; nitajenga popote pale hata kama bila kibali cha ujenzi as long as sivunji sheria.

Siwezi kuisubiri Serikali mpaka pale itakapokuja kunipimia kiwanja, ndiyo nasema hivi nimeshajenga kwenye kishamba changu, wakija na ramani zao watanikuta hapa hapa.
 
ZEE LA HEKIMA

JF-Expert Member
Aug 10, 2015
1,298
2,000
Watanzania kwa ujumla kuanzia viongozi wa kitaifa mpaka wa vitongoji hawaonyeshi kabisa kwamba kuna anayejali hii nchi itakuwa wapi miaka 20 ijayo. Kila mtu anataka chap chap cha sasa hivi. Ndio maana hakuna anayejali elimu inavyoporomoka. Hakuna anayejiuliza kwamba vijana watakaomaliza shule na vyuo katika miaka kumi ijayo watakuwa wanafanya nini. Tunabaki kujisifu tuna amani wakati amani haiwezi ikawepo ikiwa watu wengi mno watakuwa wana njaa na hawana ajira. Badala ya kuhakikisha vijana wasomi ambao wamekoda ajira wanajiajiri kwenye kilimo na kuhakikisha masoko ya mazao hayo yanapatikana, nchi inatumia nguvu na rasilimali nyingi kwenye miradi ambayo hata kama itaendeshwa kwa faida kubwa namna gani, kamwe hiyo faida haiwezi kufikia faida ambayo ingepatikana kwa kuwezesha vijana laki mbili kujiajiri kwenye kilimo ambacho mazao yake yatauzika haraka. Tunashindwa kuelewa kwamba ni rahisi sana vijana waliokata tamaa (maana hawana ajira wala hawajui kesho yao ikoje) kutumiwa na maadui wa nchi kuleta machafuko. Mungu atusaidie tu maana kwa hali ya uchumi wa sasa ilivyo, na kwa vile hayaonekani matumaini ya haraka, sijui tutakuwa wapi miaka kumi ijayo
 
Kwakweli mipango yetu ipo shortsighted sana!!
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom