Je uhuru wa mahakama na kinga ya mihimili imezaa kichaka cha kuminya demokrasia | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Je uhuru wa mahakama na kinga ya mihimili imezaa kichaka cha kuminya demokrasia

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mghaka, Jul 17, 2012.

 1. M

  Mghaka JF-Expert Member

  #1
  Jul 17, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 320
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Mimi napata taabu sana, na leo niwe mkweli kwenu wote wanajf, sikupendezwa kabisa na kuingiliwa kwa hotuba ya upinzani rasmi Bungeni kwa hoja ya kuingilia mwenendo wa kesi zilizoko mahakamani, kiasi kwamba inanibidi kuibua mjadala wa hoja nini maana ya "kuingilia mwenendo wa kesi iliyoko mahakamani".

  kwa kuchokoza niwaalike wataalamu wa sheria watuongoze sis mbumbumbu. Kutoka katika kona ya umbumbumbu mimi nadhani na naendelea kuamini kuwa kuingilia mwenendo wa kesi iliyoko mahakamani ni kutoa kauli ambazo zinanguvu ya kushawishi uamuzi au kutoa maoni nje ya utaratibu wa kimahakama kwa lengo la kushawishi mwelekeo wa kesi iliyoko mahakamani. Mfano wa kauli ambazo zinaweza kuingilia uhuru wa mahakama ni kama zile ambazo maoni yake yanashambulia au kulinda upande moja ambao unahusika na shauri lililoko mahakamani.


  Mheshimiwa Vicent Nyerere leo alizitaja kesi zenye uhusiano wa vurugu za kisiasa ambazo polisi wamehusishwa ambazo kwa maoni ya kambi ya upinzani zinaonyesha udhaifu wa jeshi la polisi na matumizi ya nguvu ya ziada ya jeshi hilo. Hakuna hata kesi moja iliyofunguliwa against the police ni kesi za mauaji ambazo zinalihusu jeshi la polisi, kuna ubaya gani kuwambia polisi ebu jiangalieni na mambo ambayo yanawanyemelea hayajengi amani yetu wala taswira ya nchi hata kama si ninyi mliyoshitakiwa.


  Kesi hizi zingekuwa zinalihusu jeshi la polisi wasingejichunguza. Wasiwasi wangu ni kwamba mahakama kamwe isiruhusu uharakishwaji wa polisi kufungua kesi zisizombele wala nyuma ili kuminya demokrasia, unawezaji kupeleka mwehu mahakamani ili kuzuia suala nyeti lisijadiliwe bungeni? Nasikitika sana, ebu Wana CCM wenzangu tukumbuku yafuatayo, hapa tulipo leo watakuwapo wao kesho, yale tuyafanyayo leo tujiandae kufanyiwa kesho, niwaombe wale wenye dhamana ya kutuongoza kufanya hivyo kwa dhana ya kujenga demokrasia ya kesho. Wapinzani hawapaswi kufundishwa kuja kuwa wakatili bali wafundishwe kuwa wema, tusiwafundishe kudhalilisha, kesho watatudhalilisha, tusiwafundishe kubeza kwani kesho watatubeza, tuliwafundisha kuomba muongozo kwa kuwadhalilisha leo wanatumia fimbo hiyohiyo kutukomoa. Mkuki isiwe kwa nguruwe kwa binadamu uchungu.

  Tuwalazimishe kesho wakikaa hapa tulipo wasijiangalie wakakumbuka tulivyowanyamazisha na kuwakejeli wakumbuke mema tunawatendea leo.


  kwa asilimia miamoja najua CDM wataendelea kupata kura za huruma zaidi kwa uma unaona kama wanaonewa. MwaCCM wa kweli anajiuliza yafuatayo katika maeneo ambayo tumefanya chaguzi mwaka huu majimbo yetu ya udiwani na jimbo moja la uchaguzi yameenda CHADEMA, tujiulize kwa nini? mbona daftari la uchaguzi hatujarekebisha? ina maana kuna uasi katika kura tulizokuwa tumezipata? kwanini? Sasa tukirekebisha daftrai la uchaguzi chaguzi zote zitakazoitishwa tutapoteza tu kwani katika kila vijana kumi CCM 1-5 na CDM 5-10 UWIANO HUU NI MKUBWA MNO NI HATARI SANA?
   
 2. T

  Think Tank JF-Expert Member

  #2
  Jul 17, 2012
  Joined: Nov 16, 2010
  Messages: 234
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Hii ni mbinu mpya povu ya Ccm ya kujificha mahakamani,ssa hoja zote kali watazfungulia kesi!Chukulia ishu ya Kovu na mkenya ni kutengenezwa ili ishu ya Ulimboka isizungumzwe kwenye bajeti ya Mambo Ndani na Mchakato wa Katiba nao wakibanwa watatuma watu wao kufungua kesi..Wakiletewa hoja mbio mahakamani..Rais apunguze safari mbio mahakamani..Sasa waitwe Chama Cha Mahakamani!
   
Loading...