Je, Uhuru wa kutoa maoni kwa Watanzania umerudi?

Kodi zenyewe zinaishia kuibiwa, kufisadiwa au kwenye ubadhirifu. CAG akiandika kuhusu wizi, ufisadi ná ubadhirifu husika anatishiwa kuuawa.




1632854228013.jpeg


Kulipa Kodi inauma huenda, Watanzania wengi hawapendi kuumia
 
Baada ya mwendakuzimu kuondoka, uhuru wa habari ulitaka kurejea, ila baada ya wapinzani kushikilia hoja ya katiba mpya, mama wa kambo na genge lake wakamwambia asikubali maana atarudisha ccm kwenye wakati mgumu. Hali hii imefanya uhuru wa habari ubanwe tena, japo hali sio mbaya sana kama kipindi cha utawala wa mwendakuzimu. Kwa ujumla uhuru wa habari haujarejea kama uhuru parsee, ila kwakuwa kipimo ni kipindi cha yule dhalimu aliye motoni, basi kuna nafuu ndogo.
Hangaya yupo vizuri sana kuliko yule dhalimu wako.

Mimi anachonifurahisha Hangaya ni jinsi anavyonikemeshea magaidi ambao hata mwendakuzimu wako hakuwahi kuwaona kama ni magaidi.

Kumbe mwendakuzimu wako alikuwa analea magaidi.

Hangaya mikumi tena
 
Dhalimu ni dhalimu hata utake kumsafisha haiwezekani. Mama wa kambo yeye anaiga tu tembo kunya. Bibi ushungi kaingia kichwa kichwa kwenye siasa chafu za dhalimu, sasa ule ushahidi mzito alio nao huko mahakamani imegeuka kuwa aibu. Lile kundi la watu wasiojulikana lililoratibiwa na jiwe la kina Kingai linaanikwa waziwazi.
a yupo vizuri sana kuliko yule dhalimu wako.

Mimi anachonifurahisha Hangaya ni jinsi anavyonikemeshea magaidi ambao hata mwendakuzimu wako hakuwahi kuwaona kama ni magaidi.

Kumbe mwendakuzimu wako alikuwa analea magaidi.

Hangaya mikumi tena
 
Dhalimu ni dhalimu hata utake kumsafisha haiwezekani. Mama wa kambo yeye anaiga tu tembo kunya. Bibi ushungi kaingia kichwa kichwa kwenye siasa chafu za dhalimu, sasa ule ushahidi mzito alio nao huko mahakamani imegeuka kuwa aibu. Lile kundi la watu wasiojulikana lililoratibiwa na jiwe la kina Kingai linaanikwa waziwazi.
Mama siyo dhalimu kabisa!

Ndio maana kaona magaidi yanaranda randa tu mtaani!

Dhalimu wako alikuwa hawaoni kabisa haya magaidi
 
JE UHURU WA KUTOA MAONI KWA WATANZANIA UMERUDI?

Kwa Mkono wa, Robert Heriel,
Yule Mtibeli.

Hakuna ubishi katika hili, Uhuru wa kutoa maoni kwa watanzania umerudi kwa kiasi kikubwa sana, kama nikaambiwa niseme kwa asilimia ngapi basi naweza kusema umefikia uhuru wa asilimia 80. Unajua bhana sisi wengine ni wale watu dizaini ya wafukunyuku, watu ambao tunapenda kufukunyua hasa kwa watu wasiopenda kufukunyuliwa.

Ninaposema Uhuru umerejea kwa asilimia kubwa ninamaanisha kwa yakini kwani nimeshafanya uchunguzi kwa sehemu, mtu fulani anaweza kuniuliza, kwani uhuru haukuwepo? Jibu ni kuwa uhuru ulikuwepo sema kwa kiwango cha chini kabisa ambacho kiliwafanya watu waishi kwa hofu na mashaka, hii ilifanya baadhi ya watu kuwa miungu watu.

Maeneo niliyoyatembelea kupima kiwango cha uhuru wa kutoa maoni ni maeneo Yafuatayo;

1. VIJIWENI
2. VYOMBO VYA USAFIRI
  1. MADEREVA BODABODA
  2. KWENYE DALADALA
  3. KWENYE MWENDO KASI
  4. KWENYE MABASI YA MKOANI
3. KWENYE SIMU
4. KWENYE MITANDAO YA KIJAMII.

1. VIJIWENI.
Kwa ambao ni wafukunyuku, mtakubaliana na mimi kuwa kwa sasa vijiweni kuna uhuru mkubwa wa watu kutoa maoni, watu wanaouwezo wa kubishana mambo ya siasa kama mpira vile pasipo hofu yoyote ile, unajua ukitaka kujua nchi fulani inauhuru wa kutoa maoni kitu cha msingi kinachoangaliwa zaidi ni maoni ya kisiasa, je wananchi wanaouwezo wa kueleza habari za viongozi wao iwe kwa mazuri au kwa mabaya? Ikiwa jibu ni ndio kwa sehemu kubwa basi jua eneo hilo upo uhuru wa kutoa maoni. Mara nyingi viongozi hasa wasiowaadilifu hupenda kubana uhuru wa maoni/kujieleza ili kuepuka mabaya yao yasisemwe. Viongozi wasiowaadilifu mara nyingi hujikuta katika udikteta wa kupanga au wa bahati mbaya.

Vijiweni kwa sasa, unaweza ukafika hata kijiwe kipya wasipokujua na ukauliza maswali ukajibiwa pasipo hofu yoyote.; Unaweza kuuliza Unauzungumziaje utawala wa Rais Samia, mtu akafunguka, akaupondaa weee! Au mwingine akausifia weee basi ilimradi.
Kumbuka hawakujui, hawajawahi kukuona, lakini hawana wasiwasi.
Vipimo vyangu vinaonyesha kuwa watu wote wa vijiweni niliowauliza maswali walinijibu, asilimia ndogo sana isiyofika 5% ndio walisema hawajihusishi na siasa.

Hii ni tofauti na awali kabla hajatawala Rais samia ambapo vipimo vyangu vilinipa majibu yafuatayo kutoka kwa niliowauliza;
1. Mimi sio mpenzi wa siasa. Kundi hili lilikuwa kubwa
2. Walinihofia., Kuwa huenda majibu yao yakawaponza
3. Walisifia hata kwa mambo ambayo yalionekana hayaendi sawa.
4. Walikosoa. Kundi hili walikuwa wachache wasiofika asilimia 2%

2. Vyombo vya Usafiri
Katika vipimo vyangu, niliamua kupima uhuru wa maoni wa watu wawapo kwenye Mabasi ya mwendokasi, unajua mambo ya kufukunyua yanahitaji moyo, kwa maana unakuta gari lote liko kimya, alafu unapenyeza kimada mshenzi kuibua mjadala ndani ya Basi wakati safari inaendelea. Hivyo unapaswa uulize yale maswali chokonozi yanayoamsha kwa haraka hisia za wasikilizaji. Kwa mfano unaweza kuuliza; umebeba barakoa mbili hapo uniazime moja? Hapo unamuuliza jirani yako aliyevaa barakoa. Atakujibu, akimaliza, unaendelea, nasikia serikali inampango wa kugawa barakoa bure kama chanjo, atajieleza wee! hapo yatatokea makundi mawili, watakaosifia na watakaopinga, utahamisha mada kwenda kwenye matangazo ya uinjilisti yaliyobandikwa mji mzima, mtajadili kwa dakika kadhaa kisha utawarudisha kwenye mada ile ile, "jana nimeenda kupata chanjo ya Corona hospitali nimekuta imeisha, inaonekana watanzania wengi wanamuitikio mzuri sana wa kuchanjwa, nimeambiwa niende kule mikocheni. Vipi wewe umechanjwa?" Unasikilizia moto.

Hapo wengine wakawa wanaiponda chanjo na serikali, wengine wanaipongeza serikali, mada za tozo na kukatika umeme zikazuka, mada za machinga nazo humo humo basi ilimradi watu wako huru kujadili. Sasa kwa ujanja penyezea mada ya vyama vya upinzani kwa namna ya wasikilizaji wasielewe unaagenda ipi. Hapo pia utagundua kuwa kwa sasa nchi ipo huru, kisha jaribu kumsifia Rais Samia baada ya kujua unaoongea nao hisia zao zimekaaje baada ya muda mchache walivyokuwa wanachangia. Kama umeona hawampendi Rais Samia, jifanye unampenda na msifie, na kama wengi wao wanampenda basi wewe jifanye humpendi na mkosoe vilivyo ili uone watakupa uhuru wa kutoa maoni yako wewe kama muwakilishi wa wasiompenda au wanaompenda Rais Samia.

Vipimo vyangu vinaonyesha kuwa, kwa sasa hakuna kutishiana, watu wako huru kujadili siasa hata kwenye daladala tofauti na kipindi kilichopita ambacho mpaka tangazo lilitoka kuwa hakuna kujadili siasa ndani ya vyombo vya usafiri.

3. MITANDAO YA KIJAMII
Huku ndio watu wako huru mpaka wanapitiliza, niliingia Facebook, Instagram, makundi kadhaa ya WhatsApp, hata hapa Jamii Forum, watu wako huru kujadili mambo mazito na kuwasema viongozi pasipo hofu.
Mtaungana na mimi hasa mnaotembelea Mtandao wa Facebook kuwa watu wengi sasa wapo huru kumkosoa Mpaka Rais tofauti na kipindi kilichopita.
Nimeshuhudia matusi kwa vijana wengi wakitukana utawala na serikali, japo huo sio uhuru mzuri na unavunja sheria lakini watu hivyo wanafanya, wakosoaji wanakosoa pasipo hofu yoyote. Watu wapo huru kwa sehemu kubwa.

4. KWENYE SIMU.
Kwa sisi tunaoandika andika mitandaoni hasa kutoa maoni yetu iwe yakusifia au kukosoa ilikuwa kawaida kupigiwa simu au kutumiwa SMS na watu za vitisho na kutukanwa. Lakini tangu aingie Rais Samia nafikiri kwa wengi hali hiyo imepungua na wengine haijawahi kutokea tangu Samia aingie.

Kwa hili naipongeza serikali, uhuru umerejea kwa sehemu kubwa.

Sehemu ndogo iliyobakia ni CCM kujifanya wao ndio watoa uhuru kwa vyama vingine jambo ambalo sio Haki.
Nafikiri msingi wa Katiba mpya upo hapo, hasa kwa wanaoitafuta, ingawaje yapo mambo mengine.

Robert Heriel
Dar es salaam
Kuna boda boda juzi nilipanda alinambia mambo makubwa sikuamini. Tanzania tumeamka.
 
  • Thanks
Reactions: G4N
Back
Top Bottom