Je, uhuru wa habari na uhuru wa kutoa maoni umerudi rasmi?

lendila

JF-Expert Member
Sep 26, 2012
5,806
4,370
Wana wa Tanzania,

Je, uhuru wa wa vyombo vya habari na uhuru wa kutoa maoni ndio umerudi rasmi nchini Tanzanai?

Watanzani wa huku kitaa wanamwita rais wetu mpya kwa jina maarufu kuwa ni mama faraja.

Kitaa wanamtambua mama yetu na rais wetu kama mama faraja.

Wengine wanasema mama ni mpenda demokrasia hawezi kuwa anapiga mawazo ya watu wengine rungu.

Je,wananchi wanawaza mawazo sahihi?

Hongera sana rais wetu mpendwa na mpenda watu.

Endelea na moyo huo huo
 
Hoja sio CCM
Hoja ni ataheshimu demokrasia?
Mbona ameanza vizuri sana
Tatizo wengi wenu mnadanganywa na uanaharakati wa watu wa twitter, ambao wengi ni watoto wa wazito, na wengine wana connection kubwa serikali ni.Bila kujifunza unakuta na watoto wa kimasikini wanataka kushindana serikali,kisa ana smartphone.

Uhuru lazima uambatane na mipaka. Ukijitia mjuaji lazima upotezwe.
 
Upotezwe kwa sababu gani?
 
Kwa Baraza lake la Mawaziri aliloteua sidhani kama kutakuwa na uhuru wa vyombo vya habari. Hili litakuwa kosa kubwa la Mama.
 
Leo kwa Mara ya kwanza baada ya kipindi kirefu sana nimeshawishika kununua gazeti mwananchi
 
Ni mapema sana kusema kwamba uhuru umerudi, ngoja tuone siku 100 za mwanzo zitatupa uhakika wa aina ya utawala tutakao kuwa nao kwa miaka hii minne
 
Mama anaweza akawa hana tabu... Tatizo ni watendaji wake... Je wanawaza na kutaka kama atakavyo Mama
 
Mama anaweza akawa hana tabu... Tatizo ni watendaji wake... Je wanawaza na kutaka kama atakavyo Mama
Uhuru siyo hisani ya rais ni haki ya kikatiba mama kwanini aendelee kufanya kazi na watu wanaovunja katiba ?
 
Uhuru siyo hisani ya rais ni haki ya kikatiba mama kwanini aendelee kufanya kazi na watu wanaovunja katiba ?
Nadhani ni mfumo mbovu walionao CCM, wa kubebana katika masuala ya kitaifa... Kuna muda unashindwa kumwajibisha mtendaji wako kwasababu tu ni mtu fulani... Ama utaonekana sivyo ndani ya chama...
Na hili linapelekea watendaji wa chini kufanya mambo ambayo yanakinzana na katiba...
 
Back
Top Bottom