Je, Ugoro upo kwenye orodha ya madawa ya kulevya?

Mnyongeni Mnyonge

JF-Expert Member
Mar 13, 2015
628
727
Msaada hivi ugoro ni nini nliwahi kusikia ni tumbaku je ni kwel ni tumbaku?

Inatengenezwaje na je ugoro upo kwenye kundi la madaw ya kulevya? Dubai na viwanja vya ndege unapita bila wasiwasi na nasikia ni fursa nzuri kwenda kuuza dubai nataka nianze biashara hiyo mwenye kuelewa anipe msaada.

Ahsante JF family.
 
Daaah maswali yako mengi mpaka nachanganyikiwa
Ugoro ni mabaki ya tumbaku
Haupo kwenye kundi la madawa ya kulevya
Hio biashara huwezi kuifanya coz products za tumbaku za huko dubai ni zile ziko packed kutoka manufacturer wakubwa
 
Hand made only from Tanzania, muulize Masai Dada kwa ufafanuzi zaidi.
 
Ugoro unatokana na tumbaku!zamani ulikuwa unatumiwa Sana na vibibi na wazee,ila kwa sasa kijana kuanzia miaka 17 hadi 40 ndiyo wanaoutumia had I mabishooo na mabrazamen wanaugonga!

Una faida gani sasa.....?.......stim yake ipo angle gani......?.......
Wachafu sana watu wanaotumia ugoro..............
 
Daaah maswali yako mengi mpaka nachanganyikiwa
Ugoro ni mabaki ya tumbaku
Haupo kwenye kundi la madawa ya kulevya
Hio biashara huwezi kuifanya coz products za tumbaku za huko dubai ni zile ziko packed kutoka manufacturer wakubwa
Kwan ugoro cwezi nikaupack vzr kwa ubora na nkauuza dubai kaka nipe somo hapo
 
Una faida gani sasa.....?.......stim yake ipo angle gani......?.......
Wachafu sana watu wanaotumia ugoro..............
Kwa sahv ukiwaona watumiaji wa ugoro hutaamini mtu na personality take anaugonga vizuri tu....wenyewe wanasema Una stimu tu ila mm sijawahi itumia hii kitu....mm najua stimu ya bangi,u....,ash ambayo zamani nilivutaaaa
 
Nawachukia sana watumia ugoro mana wananuka midomo kishenzi alafu naona hauna tofauti na dawa za kulevya mana nasikia wanasema una stimu kama mirungi.
 
Ugoro ni unga unaotokana na majani makavu ya mmea wa mtumbaku.

Inakadiliwa ndani ya tumbaku kuna zaidi ya kemikali 700 ambazo ni sumu,lakini kubwa na inayojulikana sana ni nikotini(nicotine).

Mtu anapokula ugoro husambaa haraka sana mwilini,kupitia damu na kuweza kufikia sehemu mbali za mwili kama vile kwenye ubongo,moyo na hata mapafu ndani ya sekunde 7 mpaka 15 tu.

Ugoro unapofika kwenye ubongo unauthiri kwa kuingilia mfumo wa neva za fahamu hali inayopelekea mtu kuhisi raha na utulivu pamoja na kuondolewa maumivu.

ugoro unaweza kusababisha matatizo mbalimbali ya kiafya kama vile kansa ya mapafu,mapigo ya moyo kuongezeka na kadhalika.

Ugoro pia umfanya mtumiaji kunuka harufu mbaya mdomoni na wakati mwingine kuondoa uwezo wa kutambua radha ya chakula.

Ugoro pia husababisha kutokuona vizuri hasa wakati wa usiku kwa mtumiaji.

Tofauti na pombe ugoro hauna kilevi na hivyo hauleweshi.
 
Upete kitu cha ngaramton ctunaitaa dongoo,Nokia yakufunua, gejii au chokolatee Nina miaka sita natumia ninamke na hajawahi gundua wala kuhisi chochote zaid ya washkaji tunaotumia pamojaa na niwatu nashughul zetuu. Ila nikwasiri sanaaa mpaka usanuke inaestimu nzur kwa mzoefuu ila ukiwa form one lazma ukae chin ukate gogo au utapikee ikibid jashoo ndo utasema mvua imekukumbaa
 
Ugoro nitumbaku iliyokaushwa, inatwangwa, na kuchangaywa na maji flani,yanitwa (inabwa) kwa jina la kienyeji, kiswahili sijui, hayo maji hupatikana kupitia maganda ya ndizi mbivu yaliyokaushwa na baadae kuchomwa moto,na kubakia majivu,majivu yale ndo huchukuliwa na kuchanganywa na maji kisha kutengeneza rangi nyeusi, baada ya hapo maji yale huwekwa kwenye kibuyu kama siku tatu hivi,kabla ya kuchanganywa na tumbaku iliyotwangwa na kulainika kabisa. Ugoro una test tofauti kwa wale watumiaji halisi anajua ugoro mkali na ugoro ambao sio mkali kwa kuutaza tu. Wakati nikiwa mtoto nilikaa na babu yangu ambaye alikuwa mkulima mzuri wa tumbaku na mtengenezaji mzuri wa ugoro,ndipo nilipoona namna ya kutengeneza ugoro.
 
Dawa ni kitu chochote kile ambacho kama kitaliwa na kuingia ndani ya mwili hakitokuwa tu na athari za kisaikolojia bali pia na athari za kifiziolojia.

Ugoro ambao una nikotine(nicotene) an addictive drug pia uangukia kwenye kundi la madawa kama vile kokeni(cocaine) heroin au morphine.

Kwa mfano mtu anapokula ugoro nikotini uingia kwenye mkondo wa damu na kwenda mpaka kwenye tezi za adrenali na kuzisisimua kuzalisha homoni ya adrenalini(epinephrine) inayopelekea mapigo ya moyo kuongezeka,kiasi cha sukari kuongezeka kwenye damu,ngozi kujifinya,na kutanuka kwa mishipa ya damu ya ateri hivyo hali ya mwili ubadilika.
 
Back
Top Bottom