Je ufisadi utaisha tukiwa wazi kama Ndugu Mengi?

Mhache

JF-Expert Member
Jun 20, 2008
345
24
Je Mengi alifanya kosa kuwataja mafisadi? Serikali imetamka wazi kuwa Mheshimiwa Reginald Mengi alifanya makosa kuwataja mafisadi hadharani kwani wengi wao matatizo yao yapo mahakamani. Mengi hana mamlaka ya kufanya hivyo. Je mtu kutaja wanaofanya makosa hadharani si haki ya kikatiba? Ninaomba kueleweshwa kuhusiana na hilo.
 
Ukimuona mwizi anaiba, au unajua maovu ya mtu yeyote yule hata kama yupo mahabusu unayo haki ya kutoa taarifa kwa umma au vyombo vya usalama. Hiyo ndiyo haki uliyo pewa na katiba. So, Mengi yupo sahihi.
 
Ishu ya Mengi kutaja watu hadharani, kwa mtu wa kawaida haina tatizo.Unapoanza kuangalia ni nani anafaidika na nani anapata hasara kwa kitendo hiki cha kutaja hadharani ndiyo utajua kwanini Serikali inakuwa na hasira.Mafisadi wameshirikiana na watu ambao wangetegemewa kuweka maslahi ya Taifa mbele kuliko yale ya binafsi.Hao watu watajitahidi kwa nguvu zote kulindana hata kwa kutumia misingi ya Kisheria na technicalities nyingine - kwamba kutaja ni kuhukumu; kutaja majina ya walio na kesi mahakami ni kuingilia uhuru wa mahakama na kutoa hukumu ilhali mchakato ungali unaendelea hoja ambazo zina mantiki na uzito kisheria.
Tutaona na kusikia mengi ya kushangaza maana hii vita dhidi ya mafisadi ni kubwa na ngumu.
Kama vita nyingine, there will be battles won and battles lost.
 
vita dhidi ya ufisadi haina tofauti na vita dhidi ya ukaburu. maana mafisadi wanajiona wao ni bora zaidi ya wananchi hivyo wamejijenga na kujitenga na jamii ilhali waniibia jamii hiyohiyo wanayoibagua.
 
Unategemea nini kama serikali imewekwa madarakani kwa misaada mingi ya mafisadi?lazima wawe nao pamoja. Kama mengi hana ruhusa ya kuwataja mafisadi, je mafisadi nani amewapa ruhusa ya kuiba mali zetu kila upande? Itakuwa ni hao wasimamizi wa utawala bora.
kazi kweli kweli
 
Majina yalipotajwa pale Mwembe yanga na akina Dr Slaa hatukusikia yeyote kutoka Serikalini akitamka kwamba aiyetaja hakuwa na mamlaka ya kufanya hivyo. Tulishuhudia karibu wote waliotajwa wakiwaita waandishi wa habari na kutoa misimamo yao ama wa kuwapeleka mahakamani au kusema wanayapuuzia tu. Sasa, kwa hili la Mengi mbona linapata wa kulitolea kauli wakati waliotajwa wamekaa kimya? Au ndo kusema pilpili iliyo shambani imeanza kuwawasha walio mezani! K U L I K O N I !!
 
Ama kweli ukistaajabu ya Juma wa Manzese utayaona ya Mwagito wa Msewe, ni vita kubwa baina ya watu wenye pesa,vyeo na nyadhifa katika kisiwa kilicho katika tufani cha Tanzania, ni wale wale wanaolumbana,wanaotajana na vijembe kutupiana, Ama kwa hakika ni zama za Papa kulana na Tembo kuumizana, Unajua ni nini? Maslahi,Biashara,Heshima na mengi yapendwayo nao. nafkiri hii vita itatuumiza sana sie kina nanihii na wale kina hewala! JE? Sie hatuwezi?
 
tatizo letu kubwa lipo serikalini,uwajibikaji wa viongozi wetu,tutatafuta mchawi mpaka milele,lakini bila kuwa na viongozi ambao wako accountable kwa serikali yao,itakuwa ni hamna kitu,
kitendo cha mengi kuwataja mafisadi kimekuwa ni issue kubwa kwa vigogo wetu kwa kudai kuwa hiyo sio haki na nini sijui,ili hali kila siku tunasoma na kusililiza kwenye vyombo vya habari na hata kwenye bunge,vigogo wanahamasisha "NDUGU WANANCHI,ISAIDIENI SERIKALI YENU KWA KUTUTAJIA MAJINA YA WAHALIFU,TUTAWASHUGHULIKIA MARA MOJA,SERIKALI HAIWAJUI MAFISADI ILA NYIE WANANCHI NDIO MNAWAJUA,TUPENI MAJINA YAO";nonsense,mengi kawataja majina yao,mawaziri wanalalamika nini sasa,au ndio huwa wanakula nao chaa juu nini?(10%);OBVIOUSLY,itakuwa ni hivyo,manake wasingeanza kulalamika na kuwatetea wahalifu wakati hata mwananchi wa kawaida anawajua kuwa wale waliotajwa na mengi ni miongoni mwa mafisadi wakuu katika nchi hii!
i can't real get what these ministers are sicking to accomplish on this issue,au kwa vile uchaguzi umekaribia na hao ndio huwaga wanawadhamini kwenye kugombea ubunge;
ANYWAY,theres so much to be done in this poor country!!!!!
 
Je Mengi alifanya kosa kuwataja mafisadi? Serikali imetamka wazi kuwa Mheshimiwa Reginald Mengi alifanya makosa kuwataja mafisadi hadharani kwani wengi wao matatizo yao yapo mahakamani. Mengi hana mamlaka ya kufanya hivyo. Je mtu kutaja wanaofanya makosa hadharani si haki ya kikatiba? Ninaomba kueleweshwa kuhusiana na hilo.

Ufisadi hauwezi kwisha kwa watu (mafisadi) kutajwa hadharani. Kuna haja ya kubadili mfumo wa elimu na kufundisha watu maadili (moral /ethics) tangu wakiwa wadogo. Masomo yahusuyo maadili yawepo katika mitaala yetu tangu shue ya msingi. Wanafalsafa wanasema ukimfundisha na kumwonya mtu kuhusu jambo baya anaweza akaogopa kulifanya, ingawa pia kuna school of thoughts zinapinga hiyo dhana.

Jambo lingine la msingi ni kuunda miundo mbinu (sheria na taasisi) ambayo itafanya ufisadi uwe mchezo wa hatari tofauti na ilivyo hivi sasa, mfano mdogo tu, huko China kiongozi wa umma akiamua kula rushwa ni sawa na kujitoa mhanga, kwasababu akipatikana tu kwisha habari yake, sio hapa kwetu, unakuta mtu anatuhumiwa kwa rushwa anakwenda mahakamani huku anatabasamu. Kuwe na sheria kali ambazo kila atakayetaka kufanya ufisadi lazima ajiulize mara mbili mbili, pia kuwe na vyombo vya utekelezaji na kusimamia hizo sheria.

Jambo lingine la msingi ni kuwa na utaratibu mzuri wa kuwaenzi viongozi waadilifu waliomaliza muda wao kuutumikia umma, tuwe na namna ya kuwatunza na kuwajali, mara nyingine ufisaadi na rushwa unajengewa mazingira na utawala, just imagine kiongozi aliyefanya kazi kwa uaminifu mkubwa baada ya kustaafu unamkuta mtaani anasota, this is not fair.
 
Back
Top Bottom