Je, ufanyeje kuepuka kifo ukiwa katika hali ya maono ya ndotoni?

Undava King

JF-Expert Member
Aug 11, 2017
3,181
5,314
Leo nazungumza na wale ambao mara tu wafumbapo kope zao aidha ni mchana au usiku basi utalii katika ulimwengu wa ndoto kujionea yaliyofichika zaidi.

Mara nyingi manabii hawa ukosa majibu ya vitu wanavyopitia ila ujikuta pia kuwa hawana pa kuuliza kupata ufafanuzi ama pengine kujua namna ya kukabiliana na hali hii ikiwatokea.

Tumekuwa mara kwa mara tukiwasisitiza wafanye taamuli tu kama suluhisho lakini je wajua katika ulimwengu huu tuishio tuna watu ambao wanauwezo wa asili wenye nguvu kubwa usiyo na uhusiano na taamuli?

Nitajikita kwa watu hawa ambao nitawaita wateule/walokwishavuka ng'ambo ambao katika jamii yetu uibuka aidha mmoja kati ya watu elfu makumi kenda. Ila kwakuwa wapo na wanaexist tulipo basi nivyema nao tuwaongelee.

Unajitambuaje kuwa upo kwenye kundi hili, cha kwanza; Unalala muda mfupi kwa siku kuliko watu wengine, japo ni mwingi wa mazungumzo na imagination ya kichwani(unazungumza ndani kwa ndani peke yako kuliko ufanyavyo kwa njia ya mdomo hivyo kujikuta huna muda wa kulala usingizi wa kutosha)

Japo jamii inakudefine kama mtu anayelala sana na muda mwingi unakuwa ukijifungia mahali pa peke yako kutokana na tabia yako ya kuangalia muvi/kucheza game/makala/kuchora/kuimba n.k,kujisomea nakufatilia mambo mbalimbali unayoyachunguza na kutaka kujua undani au siri iliyojificha ndani yake.

Pili; Unajikuta tu automatic umevutiwa na jambo fulani ambalo ni nje ya upeo wa kawaida na unaamua kudeal nalo pasipo ufahamu wako kung'amua unachofanya,

baada ya muda unashangaa kwenye kila njia ikupayo utambuzi au vyanzo vya maarifa yako iwe ni simu unapogoogle unajikuta umeshazama/kupata display ya mambo hayo unabaki kujiuliza hii inakuaje,

Pengine unapojisomea vitabu au kuangalia muvi ni rahisi kwako kugundua taswira ya picha iliyofichwa na muandishi/alama/ishara/jumbe ziwe za siri au za wazi kwa walengwa watazamaji

kwako wewe unaona vyote at the sometime kiasi cha kuzalisha maswali au logic ambayo wakati mwingine ukijaribu kuwaeleza wenzako wanakuona kama unazingua cha zaidi watakuita 'machinoo..'au 'kajamaa kanakera aka na mambo yake yasiyoeleweka..'au 'jamaa yeye kila kitu freemason au uchawi' n.k

pili unapolala/kujituliza ukitafakari jambo uwa linakuwa linaappear kila mahali na ni rahisi kwako kulitafakari na chakushangaza majibu unayapata katika mtiririko wako wa fikra kirahisi pengine nikupitia kutengeneza ideology zako ngumu hili zikubaliwe na watu unajikuta umejijibu jambo ulilokuwa ujawa na uhakika nalo.

Tatu; Unandoto ambazo unaziota kwa muda maalumu ikitokea umelala katika nyakati hizo katika muda maalumu mara nyingi kama muda wako ni mchana basi wewe ni mchana na kama ni usiku vivyo hivyo. Ila nje ya hivyo katika nyakati za usingizi wako wa kila siku wa kawaida unaendelea kuota ndoto za kawaida kama watu wengine.

Nne; Unatambuaje kuwa uko kwenye maono; mara nyingi tunapoota kawaida uwa hatuna hiyari ya kile kinachotokea na tunazinduka ndipo tunagundua ni ndoto mara inapoisha, unapoota nakuwa lucid unaanza na ndoto kwanza then unagundua kuwa sasa naota ngoja niendelee au niishie hapa,

Ila ndoto hii kwa njia ya maono ni ndoto deep kiasi cha kwamba hata nguvu ukuishia huku mwili ukiongozwa na pumzi tu mithili ya jinamizi la usingizini , ni scary kwa maana ya kile unachokishuhudia,distances na display size yake ni beyond upeo wa mwanadamu na inastaajabisha kuviendea kwa kasi isiyo na kifani, kuzoom taswira iliyo umbali usiopimika kwa kasi zaidi ya mwanga nakuona kila kitu nakupata maana au jina lake na maelezo hukohuko ndotoni

au kuingia katika objects hizo iwe ni katika anga hewa, chini ya dunia, juu ya mbingu, ndani ya maji,kupenya katika mioto au mwanga mkali mithili ya jua au giza totoro n.k

Ndoto hizi tofauti na zingine normally ukuijia ukiwa aware kabisa na milango yako ya fahamu isipokuwa kuna nguvu kubwa inayokusukuma beyond uwezo wako wa kuamuru mgomo wa kwenda unapotakiwa kwenda au kutokuona unachooneshwa.


Tano; Kadri unavyozidi kuyapata maono haya mara kwa mara upeo wako unazidi kupanuka zaidi juu ya mambo mengi ya sirini ni kama mtu ambaye amefunguliwa pazia la kila lifanyikalo ulimwenguni liwe jema au baya analiona live nakuling'amua na maana yake pasipo kufundishwa au kulisoma mahali na ukumbuka details zote za yale ayaonayo mpaka feelings zake.


Naomba nikomee hapa kwanza kwani hapo nimetaja baadhi tu ya mambo ambayo kama ni maelezo ya kina basi nikitabu na siyo uzi tena, tuangalie sasa ni namna gani mtu wa namna hii anaweza kuepuka matatizo ya kufia usingizini kwa mshtuko wa moyo, presha,kuzimia au kukata kwa pumzi kabisa

kutokana na mazingira ya kuyapokea maono hayo kumjengea muhusika tension kubwa kupita kipimo cha uimilivu wa nafsi, roho kuama nakufata nguvu kubwa zaidi/kukwamia huko nakushindwa

kurudi,kuwahi kabla ya muda(kuamishwa katika plane nyingine pasipo mategemeo au maandalizi) hii ni kutokana na kuwa mtu huyu hapaswi kuendelea kuishi tena katika maisha haya ya duniani kwa maana alishayagraduate tiyari.

Hivyo nguvu hizi daima ujidhihirisha kwake kwa minajili mikubwa ya kumjulisha time is near ajiandae na after life maana hata hizo siri anazoziona ni kwa kuwa tiyari sehemu ya roho yake nyingine imeshahamia another plane hivyo uwepo wake duniani bado unaweza leta disaster au ukasaidia (hili ni somo lingine ngoja niachie hapo)

Kikubwa ukiwa ni muhusika njia ya kwanza nikujua kipi hasa kwako katika maono ni your favourite kuliko vyote na huwa nguvu yake inakuwia vigumu kuimudu hata kwa sekunde, dawa ni kila utakapojikuta katika hali hii (bahati nzuri unajitambua)

Kama ni kuoneshwa au kwa kuvutwa kwenda kataa kwa kupotezea kama vile uoni au umesahau kama unatakiwa kwenda kimawazo then kwa kuwa ni ngumu sana kuignore jambo katika hali kama hii anza kusali kwa dhati kwa Mungu wako peke yake narudia tena Mungu peke yake nazo zile nguvu zitayeyuka na Israeli atakuwa amepitia mbali, njia nyinginezo ni pamoja na kufanya meditation ya kucontrol nguvu zako, kushirikiana na viumbe wengine au miungu kwa kutupia mipete,mawe,makafara n.k

"TAMATI."
 
Pastor nina swali?
Ulimwengu wa kiroho ni upi na naweza vipi kuingia?
 
Umeeleza vizuri Ila kuhusu kufa Ina depends mfano Kama mimi ni mkristo ninapokuwa na Roho mtakatifu uniongoza na kuweza kuyaona yote yaliyofichika ili nipate maarifa Fulani na kujua there is life after death mfano Nabii joeli sura ya pili na matendo ya mitume 2:17 unaweza Soma Ila mimi binafsi nimeshudia mengi Sana miujiza Ila ni katika ulimwengu wa Roho
 
Umeeleza vizuri Ila kuhusu kufa Ina depends mfano Kama mimi ni mkristo ninapokuwa na Roho mtakatifu uniongoza na kuweza kuyaona yote yaliyofichika ili nipate maarifa Fulani na kujua there is life after death mfano Nabii joeli sura ya pili na matendo ya mitume 2:17 unaweza Soma Ila mimi binafsi nimeshudia mengi Sana miujiza Ila ni katika ulimwengu wa Roho

Hongera Mkuu kwa usomaji mzuri wa kitabu chako cha imani, katika reference uliyoitoa yaani matendo ya mitume 2:17 nilivyoielewa nikana kwamba inazungumzia zile nyakati za mwisho wa dunia/kurudi kwa Yesu na siyo maono ya after your own death ila ni rhuksa pia kunikosoa kama sivyo.

Je, unatambuaje kuwa kinachokuongoza ni roho mtakatifu na siyo roho mwovu?
 
Kwanini nikilala chali naota mandoto yakutisha ila nikikemea nazinduka huju nahema
 
Haya yananitokea sana halafu najikuta sehem kama nilishawahi kuwepo lakin sikumbuki ni mwaka gani Ila ndio nagundua nilishawahi kuota nipo hapa.
 
nikiwa kwenye lucid dreams, je naweza ichange ndoto yangu nkahama kwenda kwenye dimension nyingine na nkajua siri za universe?
Inawezekana ila si rahisi kiivyo maana mara nyingi lucid huwa nikujipa furaha tu na mara nyingi muotaji upenda ndoto iendelee hasa anapojihisi ndani ya ndoto anahisia za furaha,ushindi, sifa, mafanikio,mapenzi n.k ila kinyume na hapo jambo lolote liogopeshalo,liletalo simanzi,sintofahamu,uoga, lakushangaza, linaloitaji ujasiri kusonga umtoa mapema mchezoni mwanalucid labda awe tu amedhamiria liwalo na liwe.
 
Haya yananitokea sana halafu najikuta sehem kama nilishawahi kuwepo lakin sikumbuki ni mwaka gani Ila ndio nagundua nilishawahi kuota nipo hapa.
Fuatilia mada za reborn au reincarnation nakadhalika ndani ya jukwaa hili kuna majibu ya kutosha kuhusiana na hili.
 
Back
Top Bottom