Je udhaifu wa serikali ya JK ndio unaomfanya Lowassa kuonekana lulu kwa Watanzania? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Je udhaifu wa serikali ya JK ndio unaomfanya Lowassa kuonekana lulu kwa Watanzania?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MNYISANZU, Jan 21, 2012.

 1. MNYISANZU

  MNYISANZU JF-Expert Member

  #1
  Jan 21, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 7,056
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Warning: No facts,no right to contribute ! Edward Lowassa alipoenda UDSM pamoja na JK kwenye maadhimisho ya miaka 50 ya UDSM wanafunzi wa UDSM walimzomea sana JK na pia walimwonyesha mabango yenye ujumbe kuhusu madai yao mbalimbali. Lowassa hakuzomewa hata kidogo licha ya baadhi ya watu ikiwemo some members wa JF kudai ni fisadi. Cha kushangaza wakati Lowassa anatoka kwenye ukumbi wa Nkrumah wanafunzi hao wa UDSM a.k.a The home of intellectuals walimshangilia sana Lowassa na hata kufikia hatua ya kumwomba awasaidie ktk kutatua kero zao. Swali linalokuja hapa ni je kwanini EL alishangiliwa? na je hii inaleta picha gani kwa jamii ya Kitanzania? na je hawa wasomi ni mazuzu na hawaelewi kitu? je wapo kwenye pay roll ya Lowassa?. Tukio lingine ni pale alipokuwa anaelekea Mwanza kwenye harambee ya kanisa katoliki. Lowassa alipofika Shinyanga wakazi wa kule waliuzuia msafara wake na kutaka kuongea nae japo kidogo. Wakazi wa eneo husika walifikia hadi hatua ya kutaka kulisukuma gari lake! ila jamaa kwa busara zake aliwasihi wananchi wauache msafara wake uendelee kwani alikuwa na haraka na safari yake. maswali mengi sana yanazaliwa hapa lakini kuu zaidi ni je kwanini Lowassa anakubalika sana kanda ya ziwa[ evidence zinazothibitisha hili zipo]. Na pia kwanini huyu jamaa anakubalika sana miongoni mwa viongozi wa dini na wafuasi wao? Na je ni upi umuhimu wa kanda ya ziwa katika kuamua rais awe nani katika uchaguzi mkuu? Matukio ni mengi yanayoonyesha kukubalika kwa huyu mtu anayeitwa na Nape na pia baadhi ya members wa JF kuwa ni fisadi. Facts only is required here, kama huna point soma tu na upite zako.
   
 2. a

  adobe JF-Expert Member

  #2
  Jan 21, 2012
  Joined: May 6, 2009
  Messages: 1,666
  Likes Received: 290
  Trophy Points: 180
  ngoja niweke pumba zangu ni sepe.kwanza jamaa ni mchapakazi mahiri hachekicheki ovyo kama jamaa yetu,pili shy na mz wamenufaika na utendaji wake kwa kupata maji,tatu ndiye next presdaa so lazima wajikombe ili atakapochukua nchi awakumbuke.bye
   
 3. Ndumbayeye

  Ndumbayeye JF-Expert Member

  #3
  Jan 21, 2012
  Joined: Jan 31, 2009
  Messages: 4,806
  Likes Received: 1,053
  Trophy Points: 280
  mzee bado unarandaranda tu na story za Lowassa! Tanazania ina watu milioni 40..
   
 4. J

  JACADUOGO2. JF-Expert Member

  #4
  Jan 21, 2012
  Joined: Dec 13, 2010
  Messages: 930
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  1. Lowassa siyo lulu kwa watanzania!
  2. Wewe mtoa mada ni mfuasi wa Lowassa!
  3. Lowassa na CCM hawana chao kanda ya ziwa!
  4. Lowassa hakuzomewa UDSM kwa sababu hakuwa mhusika wa zomea zomea!
  5. Wanaojaribu kumsafisha Lowassa hawana hoja ila wako kimaslahi zaidi.
  6. Lowassa ni fisadi aliyekubuhu na hatokuwa rais wa Tanzania kamwe!
   
 5. doctorz

  doctorz JF-Expert Member

  #5
  Jan 21, 2012
  Joined: Aug 10, 2010
  Messages: 907
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Nakubaliana na JACADUOGO2
   
 6. K

  Kubingwa JF-Expert Member

  #6
  Jan 21, 2012
  Joined: Apr 23, 2010
  Messages: 502
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Ngoja wengine upite,tukichngia utasikia watu wanaanza ooh katumwa mara sijui nini! Napita tu mkuu kama ulivyosema.
   
 7. MNYISANZU

  MNYISANZU JF-Expert Member

  #7
  Jan 21, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 7,056
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  JACADUOGO2, wewe ulichofanya ni kukanusha tu bila evidence!
   
 8. Shine

  Shine JF-Expert Member

  #8
  Jan 21, 2012
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 11,514
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Unaposema El anaonekana ni lulu kwa waTZ unakosea kwani mm ni mmoja wa waTz na simwoni kama ni lulu bali ni mnyonyaji na fisadi aliyeshindikana hata ndani ya chama chake
   
 9. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #9
  Jan 21, 2012
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,986
  Likes Received: 443
  Trophy Points: 180
  I hv smelt something here!
   
 10. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #10
  Jan 21, 2012
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,986
  Likes Received: 443
  Trophy Points: 180
  EL ameshauvamia mtandao huu. wameanza kumsafisha mapema!
   
 11. H

  HByabatto jr Senior Member

  #11
  Jan 21, 2012
  Joined: Dec 23, 2011
  Messages: 142
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Narudia tena kusema kwamba enzi za kutawaliwa na wahuni hazitajirudia tena. Namshauri LOWASA bora akawe headmaster kwenye hivyo vijiwe vya kata alivyoanzisha a.k.a madanguro ya kata.
   
 12. MNYISANZU

  MNYISANZU JF-Expert Member

  #12
  Jan 21, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 7,056
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Jibuni hoja sio mnatoa mere claims with no supporting evidence!
   
 13. H

  Honolulu JF-Expert Member

  #13
  Jan 23, 2012
  Joined: Jan 20, 2012
  Messages: 5,654
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Hivi ninyi watu mnalipwa shillingi ngapi ili kumpiga Lowasa debe? Mbona hata watoto wadogo vijijini wanajua kuwa maadui wa jamii sasa hivi ni wanne: Ujinga, maradhi umaskini na Lowasa!
   
 14. RaiaMbishi

  RaiaMbishi JF-Expert Member

  #14
  Jan 23, 2012
  Joined: Jan 18, 2012
  Messages: 252
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Walimshangilia sana Lowassa kwasababu wanafunzi wote kuanzia sekondari hadi chuo kikuu malengo yao ni kupata elimu ili wapate ajira na kubadilisha maisha yao wakilenga ndoto zao zaidi kwenye vitengo vyenye maslahi kama vile TRA n.k. Ni dhahiri kwamba kwa wale wanaosoma ili waje kuitumikia jamii hawakumshangilia, na hawa ni wachache sana; vinginevyo hizi vurugu za vyuo vikuu kuhusu ada n.k ni hasira za kucheleweshewa muda wa kumaliza elimu wakakamue, vinginevyo tungewaona waliomaliza miaka ya nyuma wakifanya ya wenzao mitaani kama kule egypt, tunisia n.k; Kuhusu Lowassa kukubalika kanda ya ziwa, ni kweli, lakini amewanunua umoja wa vijana na uongozi wa CCM Shinyanga, Mara, Mwanza na Bukoba (bukoba pia ana ranchi moja ya kufa mtu); Lowassa hakubaliki na wananchi wa kanda ya ziwa (mfano tuliona alivyoabishwa kwenye uchaguzi wa jimbo la nyamagana alipoenda kujaribu kumuokoa rafiki yake - Masha akiwa na mkoba wa shillingi milioni 800 za kumhonga Wenje etc). Lowassa anapenda na wana ccm wa kanda ya ziwa, sio wananchi; na kwa vile ni wana ccm ndio wanaenda dodoma kupigia kura jina la mgombea wa CCM, safari yake mwaka 2015 itakuwa ni kuteleza tu bila juhudi kubwa sana; Mbali ya Kanda ya Ziwa, pia anakubalika sana Zanzibar miongoni mwa wana CCM. Kule watu wake ni Bilal na Karume, lakini pia amewanunua UVCCM; haipiti mwezi bila ya Lowassa kutuma milioni 15-20 kwa UVCCM mikoa mbali mbali, mwezi huu mara, mwezi ujao ruvuma, mwezi uliopita Kigoma; Kuhusu Lowassa na Makanisa, kuna udini wa chini kwa chini unaendelea, waislaamu wana mchakato wao kuelekea 2015, na CCM wa kwao; Tofauti kuu iliyopo baina ya wakristo na waislamu ni kwamba waislamu wanafanya chini kwa chini, huku wakristo wakifanya nje nje;
   
Loading...