Je uchifu umerudi Tanzania ?Je kuna ubaya tukirudisha uchifu ? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Je uchifu umerudi Tanzania ?Je kuna ubaya tukirudisha uchifu ?

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by fige, Aug 1, 2010.

 1. fige

  fige JF-Expert Member

  #1
  Aug 1, 2010
  Joined: Jul 4, 2010
  Messages: 376
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  'siamini hata kidogo kuwa watoto wanaozaliwa na mama au baba fulani ndio wana uwezo au kipaji cha kuwa viongozi '
  Hayo si maneno yangu bali maneno ya Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere.Nimenukuu maneno hayo kwa sababu ya wimbi la watoto wa viongozi wanaotaka uongozi.Wanajamii tunaonaje ,je hawa watoto wanachaguliwa kwa sababu wanafaa,ni kwa nguvu ya wazazi,au ujinga wa wananchi ?Je kuna athri yeyote kijamii kwa wimbi hili kuendelea ?
   
 2. A

  Akili Kichwani JF-Expert Member

  #2
  Aug 1, 2010
  Joined: Jan 7, 2010
  Messages: 1,504
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  tupe mifano ya kuaminika....
   
 3. Swahilian

  Swahilian JF-Expert Member

  #3
  Aug 1, 2010
  Joined: Apr 28, 2009
  Messages: 585
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Hili suala la urithishaji limekuwa likijitokeza siku hadi siku na sie wenyewe kwa njia moja au nyingine tume/tuna likubali.

  Je unataka kujua ni kwa vipi?

  1. Hawa watoto wa viongozi walio madarakani au wastaafu nani huwapeleka kugombea?

  2. Hata kama ni kwa nguvu ya Baba zao je hugombea wapi? Na tunao/wanao wapigia kura za ndio/hapana ni sie au kina nani?

  3. Je ni kweli hawa watoto wa vibopa hawaziwezi/mamluki katika nafasi hizo, wanabebwa au tunawabeba sie?

  4. Tufanyeje sie tuso na nafasi hizo, kwani si watoto wa vigogo au wenye pesa, je tuzidi kuangalia na kuvumilia hali hii?

  5. Iwapo hatuna uwezo wa mmoja mmoja, Je? Tuunganishe nguvu ili tumchangie mali, pesa na sera ili aweze kuwashinda tusowapenda?

  6. Ipi hatima ya Wagombea wetu masikini baada ya kuchaguliwa, je watabaki kuwa wenzetu na tukajumuika pamoja kama zamani? Au watajitenga na kujificha katika majumba yao?

  7. Tukiwa makini hayo yatawezekana lakini je? We uko tayari kugombea/ kuchagua au kuchaguliwa na baadaye kutetea jamii yako ilokuchangia?
   
 4. Lukolo

  Lukolo JF-Expert Member

  #4
  Aug 1, 2010
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 5,137
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  January Makamba, Binti Pinda, Amani Abeid Karume, Vita kawawa, Hussein Mwinyi, ......
   
 5. Anko Sam

  Anko Sam JF-Expert Member

  #5
  Aug 1, 2010
  Joined: Jun 30, 2010
  Messages: 3,216
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Akili Kichwani kumbe hata hufuatilii mambo ya nchi hii. Kama huwajui watoto wa vigogo wanao wania madaraka kwa migongo ya wazazi wao, basi hata kura utapiga bila kujua ni kwanini unapiga kura, inaonyesha utapiga kura kwa sababu ni kipindi cha uchaguzi. Pole sana AK !
   
 6. Kituko

  Kituko JF-Expert Member

  #6
  Aug 1, 2010
  Joined: Jan 12, 2009
  Messages: 9,366
  Likes Received: 7,008
  Trophy Points: 280
  Mkuu sio Tanzania tu, hiyo ni Hulka ya Binadamu

  Kenyata, Mabutu, Kabila, Castro, Bush, na wengie wengi tu
   
 7. MchunguZI

  MchunguZI JF-Expert Member

  #7
  Aug 1, 2010
  Joined: Jun 14, 2008
  Messages: 3,623
  Likes Received: 590
  Trophy Points: 280
  Kwa afrika ni siasa za kuanzia miaka ya 80, tulipoanza kuzuiwa kupindua serikali kwa kutengwa na vikwazo.
  Kabla ya hapo kila kiongozi alikimbizia watoto wake nje ya nchi ili mambo yakigeuka, wapone. Ndo maana akina Karume jr hatukuwasikia, wakajidai kupelekwa ubalozini na hata shule kusomea nje.

  Sasa leo hii mapinduzi yakazuiwa kwa nguvu zote bila kufahamu kwamba nchi zetu bado tuna wapuuzi wakishika nchi!
   
 8. J

  JokaKuu Platinum Member

  #8
  Aug 1, 2010
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,805
  Likes Received: 5,098
  Trophy Points: 280
  ..lakini Baba wa Taifa naye si alikuwa mtoto wa Chifu?

  ..viongozi wengi wa tangu Uhuru ni wazazi wao walikuwa na "nafasi" fulani wakati wa ukoloni.
   
Loading...